Waziri Ngeleja wilaya zenye migodi lazima zipewe sehemu ya mrahaba!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Ngeleja wilaya zenye migodi lazima zipewe sehemu ya mrahaba!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Magezi, Apr 24, 2010.

 1. M

  Magezi JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Ndugu wananchi, inashangaza kuona eti wilaya, vijiji na hata mkoa kwa ujumla ambapo migodi ya dhahabu ipo bado hakuna shule nzuri, hakuna maji, hakuna umeme, hakuna hospitali, hakuna barabara za lami n.k.

  Serikali kuu hiyo pesa mnapeleka wapi? Kwa nini wilaya na vijiji husika visifaidike na raslimali ili ktk maeneo yao? Lazima 10% ya mrahaba ibaki ktk wilaya husika na wilaya zigawie vijiji kwa kujenga miundo mbinu muhimu na kuweka huduma za jamii zenye ubora.

  Hata kama serikali ya CCM imejawa wahuni na wezi tunataka haki yetu.
   
 2. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  haki haiombwi inadaiwa, na haki nzuri kama hii usitegemee kuipata kwenye blackberry, dell, toshiba au HP, ukiwa kwenye kiti cha ngozi kinachozunguka, ukipata ubaridi wa AC. Something more to that has to be done.
   
 3. M

  Magezi JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mbona Jf members wengi siku hizi wanapenda thread za mapenzi na umbea?
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Apr 25, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kwa sababu siasa zimetushinda.
   
 5. P

  PELE JF-Expert Member

  #5
  Apr 25, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 229
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Umeuliza swali zuri sana na hili ni moja ya sababu kuu ambazo wale wachangiaji wazuri siku za nyuma katika mambo mbali mbali ya muhimu kuhusu nchi yetu wameamua ama kuondoka au kukaa kimya. Zamani ukifungua hapa jumbe nyingi zilikuwa ni za mambo ya siasa, lakini siku hizi ni za mambo ya mapenzi, umbeya na mambo mengine ambayo hayaongezi tija yoyote katika maisha ya kila siku kwa Watanzania walio wengi. Wenyewe wanasema siasa zinaumiza kichwa!!!! lakini hawaishi kulalamika kwamba nchi haiendelei na maisha yanazidi kuwa magumu na wakati huo huo hawataki kuongelea siasa!!! go figure!!!!! Jamii forums is in the dog's house. I don't know for how long, but something must be done immediately to rescue this forum from falling apart for good.
   
 6. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #6
  Apr 25, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Simple! Hii sio sera ya CCM. CCM wanaamini kuwa rasilimali zaote ni za taifa na zinagawanywa kwa utaratibu huo.
  Labda muijaribu CHADEMA ambayo ndiyo yenye sera ya majimbo, wanaweza kulipatia jibu zuri zaidi kwa kuwa hapa ndipo imani yao ilipolala
   
 7. M

  Magezi JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Lakini mkuu hivi sera huwa haziboreshwi? Kama sera za CCM zinaonekana kutokidhi haja kwa nini wahusika akina JK wasizibadilidhe/kuziboresha?
   
Loading...