Waziri Ngeleja na hatua sita za kuzuia mgawo wa umeme | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Ngeleja na hatua sita za kuzuia mgawo wa umeme

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Manyanza, Feb 16, 2011.

 1. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Serikali imetolea tamko tatizo la mgawo wa umeme nchini na kutaja hatua sita za dharura ilizochukua katika kukabiliana na tatizo hilo sugu.

  Akizungumza bungeni jana, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alitaja utekelezaji wa miradi ya umeme katika kipindi kifupi na cha kati kuwa moja ya hatua hizo zilizochukuliwa kumaliza tatizo hilo.

  Waziri Ngeleja alitoa tamko hilo baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda, kumtaka afanye hivyo ili kumaliza kiu ya wabunge wa upinzani walioitaka Serikali itolee kauli suala hilo ili wananchi wajue hatima yake.

  Februari 11 mwaka huu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe katika swali la nyongeza, alimtaka Waziri Ngeleja kutolea kauli tatizo la umeme, lakini Spika Makinda aliizima hoja hiyo akisema haingekuwa rahisi kwa Waziri huyo kuzungumzia suala hilo muhimu katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo.

  Na jana baada ya kupata fursa ya kuzungumzia tatizo hilo la mgawo wa umeme Ngeleja alisema Serikali kwa kushirikiana na Tanesco imechukua hatua sita tofauti.

  Ataja hatua hizo za dharura kuwa ni pamoja na kuhakikisha fedha za kununulia mafuta ya kuendeshea kituo cha kuzalisha umeme cha IPTL zinaendelea kupatikana kwa wakati ili kizalishe kiwango cha Megawati 80 ambacho ni cha juu.

  Pia kuharakisha mchakato wa kukodi mitambo ya dharura yenye uwezo wa kuzalisha zaidi ya megawati 260 endapo mvua za kutosha hazitanyesha kuwezesha ongezeko la umeme
  unaotokana na maji na kutekeleza mpango wa kupanua miundombinu ya kusafuisha na kusafirisha gesi asilia kutoka visima vya Songosongo hadi Dar es Salaam.
  Nyingine ni kuhakikisha miradi ya kudumu ya kuzalisha umeme ya Megawati 100 itakayofungwa Ubungo, Dar es Salaam kwa kutumia gesi asilia na mitambo ya megawati 60 itakayofungwa Mwanza kutumia mafuta mazito inakamilishwa kama ilivyopangwa Desemba 2011 na Januari 2012.

  Ngeleja alitaja hatua nyingine kuwa ni kuendelea kutekeleza miradi ya kupunguza upotevu wa umeme kutoka asilimia 21 ya sasa hadi asilimia 15 kati ya mwaka 2011 na 2015, pamoja na Tanesco kusimamia mgawo wa umeme kwa umakini zaidi na kuhakikisha upatikanaji wa umeme katika shughuli za uzalishaji, sehemu nyeti za huduma za jamii, ulinzi na usalama.

  Alisema kuwa wizara yake kwa kushirikiana na Tanesco inaendelea kusimamia utekelezaji wa programu ya kuongeza uwezo wa kuzalisha umeme katika kipindi kifupi cha 2011 hadi 2015 ili kuepusha tatizo la mgawo wa umeme siku za usoni ambapo alitaja miradi tofauti saba
   
 2. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Huyu Mheshimiwa, wizara ya Nishati na Madini sio saizi yake, haingii akilini kwa waziri ngereja kuendela kutoa taarifa zake zile zile za tunafikiria..., tutaanza utekelezaji karibuni..., upembuzi yakinifu unafanyika.., tumeshatandaza nyaya, tumefunga nguzo... na rongo rongo nyiingi... ukisoma hiyo hotuba yake ya jana bungeni utaona ni jinsi gani anavyoendelea kukatisha tamaa wananchi maana ni mara nyingi amekua akitoa taarifa ambazo hatuona positive effect hata moja....
  Jamani am out
   
 3. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Ngeleja hafai hata kidogo kuwa kiongozi.
   
 4. Keynes

  Keynes JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 499
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Mi naona dawa ni kuandamana kama middle east tu.
   
 5. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #5
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kila siku ripoti zilezile zenye solution zilezile ambazo hazitekelezeki... yaani watu wasubiri mpaka december na january next year????? Huyu waziri ni bogus hafai hata kuwa katibu kata!!!
   
 6. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #6
  Feb 16, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 852
  Trophy Points: 280
  Mi nataka hao wabunge wanaouliza maswali wawe wanaweka neno "deadline" ili anayejibu atupe jibu la uhakika kuwa umeme mw 50 tunapata tarehe kadhaa and on dot tunapata, sitaki kusikia ujinga wa mtu anayetoa majibu vague yasiyo na mshiko, unasema serikali haijatoa hela kwa iptl be specific ni billions ngapi tunawalipa za mafuta na malipo yao? Acheni ujinga wa kufanya kazi kwa mazoea, swala la msingi kwa nini iptl hawalipwi? Serikali au tanesco ndo hawana hela? Kwa nini? Taifa hili lina janga la viongozi na wafanyakazi wapiga kazi ki kweli kweli, kuanzia rais mpaka shinani, ktk 100 labda ni 10% ndo wanaweza kuwa exceptional. Makampuni ya kigeni ndo yanaongoza kwa ufanisi kwa nini?
   
 7. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #7
  Feb 16, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  anapiga piga manoenio hovyo hana jipya kabisa huyu
   
 8. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kweli mkuu, hii serikali imezidi, masikhara....
   
Loading...