Waziri Ngeleja asema Dr. Slaa apuuzwe kuhusu utoroshwaji wa madini yetu

Kama meli tu zinaondoka na magogo bila vibali na magogo ni makubwa yanaonekana kirahisi mpaka yanakamatwa huko nje,mabasi tu ya kwenda mikoani issue kuyakagua yanabeba vitu haramu kila kukicha iweje ndege za wageni tena wanaotukuzwa na serikali ya ccm ambayo ikotayari kuua watu wake iliwageni wachukue rasilimali watakavyo leo hii serikali hiyo iwe na ubavu wa kukagua hizo ndege zinazobeba madhahabu magunia kwa magunia kama hayana mwenyewe Ngeleja ni muongo amewekwa pale kwa kazi maalumu.
 
Ndege ya waarabu walionunua loliondo hupita dar?aache upuuzi.kontena ngapi za pembe ndovu hupita dar kwenda china?
 
Ndege ya waarabu walionunua loliondo hupita dar?aache upuuzi.kontena ngapi za pembe ndovu hupita dar kwenda china?

Asitukumbushe mengine huyu mzee asiyejua kiswahili! So na wale twiga wetu nao walipita Dar wakakaguliwa then wataalamu wakapitisha kwamba waendelee na safari? Ngeleja sio watz wote ni wajinga kama unavyodhani wewe. Kwangu mm mpaka sasa ninashangaa ni kwanini wewe bado ni waziri.
 
Ni kweli Mzizi dawa,wenye dhamana ya udhibiti wa madini yetu ndio kwanza wako bize na silaha za kivita tena hoterini teh,teh,teh umenifurahisha sana kwani pale aliambiwa ni uwanja wa mapambano ndio ujue hizo zilikuwa ni kwa ajili ya kulindia rushwa kubwa toka kwa hao wenye migodi.
 
Nimesoma hiyo habari kwenye gazeti la mwananchi na Ngeleja anasema ndege zote huwa zinaingia na kutoka kwa vibali. Ina maana ile iliyotua KIA na kuondoka na wanyama hai nayo ilifanya vile kwa vibali? Nauliza tu.

Habari yenyewe ni hii hapa chini.

WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja, amesema wananchi wanatakiwa kupuuza madai yanayotolewa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa, kuwa Rais Jakaya Kikwete na Benjamin Mkapa waliruhusu ujenzi wa viwanja vya ndege kwenye migodi ili wawekezaji waweze kupora raslimali za nchi.Akizungumza Dar es Salaam jana, Waziri Ngeleja alisema taswira anayotaka kujenga Dk Slaa mbele ya umma ni uchochezi unaojengwa kwa hoja za uongo, kwa sababu anajua ukweli halisi.
“Dk Slaa ni muongo, mchochezi anatakiwa kupuuzwa kwa sababu anachosema siyo kweli...anajua vizuri ukweli halisi lakini anataka kupotosha umma na wananchi wachukie Serikali yao,” alisema Ngeleja.
Alisema duniani kote wawekezaji wanaruhusiwa kujenga viwanja vidogo vya ndege kwa ajili ya kusafirisha vifaa vyao na kuwarahisishia kufika maeneo yao, lakini haviruhusu uporaji wa rasilimali za nchi.
“Labda tukizungumzia usimamizi, lakini kuna maofisa wa Wizara ya Nishati na Madini, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Idara ya Uhamiaji na pia vinasimamiwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, sioni mwanya wa wizi kutokea,” alisema.
Ngeleja alisema kwa mujibu wa sheria za nchi, hakuna ndege inayoruhusiwa kwenda nje bila kibali kutokea kwenye viwanja hivyo, lazima ifike Dar es Salaam ili maofisa wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), waweze kuchukua takwimu.
Alitoa mfano wa wizi uliotokea Mgodi wa Geita, mzigo ulikuwa ukipakiwa kuletwa Dar es Salaam ili kufuata taratibu na kwamba, Dk Slaa anaelewa vizuri lakini anachojaribu kufanya ni kupata umaarufu wa kisiasa kwa kudanganya umma.
Akihutubia Kongamano la wanafunzi wa Chuo Kikuu cha St Augustine (Saut) na baadaye mkutano wa kampeni za udiwani kwenye Uwanja wa Kabohoro, Kata ya Kirumba, Dk Slaa aliwashambulia Rais Kikwete na Mkapa kwa kuruhusu ujenzi wa viwanja hivyo vinavyotumika kupora rasilimali za nchi.
Dk Slaa alisema uwapo wa viwanja hivyo umetoa ruhusa ya mali za nchi kuibwa kwa urahisi, kwa sababu viongozi waliopewa madaraka hawana uchungu na rasilimali hizo.

Huyu Ngereja hajui anachokisema. Hana uhakika na anachokisema. Wala hajui kama ndege zinaruka moja kwa moja nje ya nchi. Ni waziri wa namna gani huyu? Hatakufikiri kidogo hawezi? Ni mara ngapi amewashuhudia maofisa wa BOT wakikagua dhahabu JNIA? Je BOT ni wataalam wa dhabu mpaka wakague wao? Ameshindwa hata kutumia simple logic kuweza kulijua hili? Kama Dk. Slaa ni mchochezi wanangoja nini kumfungulia mashtaka? Shame on you Ngeleja na ccm yako.
 
Hivi hii tabia ya mawaziri kuwaona watanzania hawajui kitu itaisha lini? Hili swala la madini ya nchi kusafirishwa nje ya nchi kwa ndege bila ukaguzi wowote limekuwepo siku zote, mbona tunaofanyakazi kazi katika migodi hii ni sisi watanzania na tunashuhudia haya siku zote!! Waziri ni bora akae kimya katika hili!! inauma sana!!!.

Unajua kuna kama kaujinga fulani hata katika mfumo huo. Mzigo upakiliwe Nyamongo, ukaguzi ufanyike Dar? Kwani wakaguzi wakifanya kazi hii wakati wa kupakia mzigo si ndo ingekuwa rahisi zaidi? Chukua mfano wa mgodi wa Nyamongo ambao uko karibu zaidi na Kenya kuliko Dar. Nani anaweza kusema kwa uhakika kwamba ikiruka ndege pale lazima ije kwanza Dar na si vinginevyo! Walioutengeneza utaratibu huo wananufaika nao sana ndo maana hawana hata aibu kuutetea kama una uwezo wa kudhibiti utoroshwaji wa madini!
 
Sio kiwanja cha kanisa hicho? maana nasikia kuna makanisa yana viwanja vya ndege, vyanini?

Je kuna ubaya kwa kanisa kumiliki viwanja mahali ambapo Serikali imeshindwa kuwekeza? Unataka kututoa kwenye mada. Cha msingi ndege zinatua na kuondoka na hicho kinachodhaniwa ni madini ya urani! Wizara mnajua hilo au bize na machangu wa Moro?
 
Mupi iyo ya Namtumbo dah moja niliwai shuhudia kidogo nifaint!
Ngeleja amesahau hawa jamaa wa dhahabu waliconfirm kuwa kuanzia sasa wataanza safairisha madini kwa ndege hasa baada ya ule mkasa wa kutaka kuibiwa!
Ivi haiwezekani wananchi kuandamana ili Ngeleja ajiuzuru maana majibu na vitendo vyake kwa hii wizara ni janga kwa Nishati na madini ya Tz
 
Kama kweli hiyo mgodi inakaguliwa sawasawa na kulipa USHURU na KODI zake vizuri basi katika ile orodha ya walipa kodi wakubwa aliyoitoa Mizengo Pinda bungeni July 2011 nao wangekuwemo.
 
Madini yanaondoka moja kwa moja asidanganye watu, hata watu wa TRA mzigo wanauonea kwa mbali tu. Huyo Ngeleja mwenyewe anajua na ndio deal zake, asituambie kitu, wameshakula sana na wanaendelea kula kwa sana

Ndani ya ccm iliyoanza kuongozwa na Nkapa na hatimaye Kikwete sijawahi kumuona mkweli hata mmoja,labda kidogo sana Tambwe Hizza alijaribu kuwa mkweli kuliko wote!
 
BOT wana ofisi kila kanda,TRA wapo kila mkoa hana imani nao mpaka ndege ije dar?aende zake night club ndicho ajuacho
 
wa kupuuzwa ni yeye Ngeleja, sijui anapata wapi huu ujasiri wa kutuambia haya ilhali tunajua kuwa huu uovu ni wa kawaida sana!
 
Ngeleja ni kupe la kutisha. Linahongwa na wezi wetu wa madini halafu linatulia. Kwanini Mungu asiliue hili limtu?
 
swali rahisi kwa ngeleja atupe data ni kg ngapi za almasi,gold,tanzanite zimepita dar february 2012?ndege gani & namba
 
huyu kijana ana matatizo yake tutamlipua na mambo yake na ufisadi wake ajui kuwa tunajua mengi anayofanya na miradi yake uko buhemba mgodini tuna mengi tunayo yajua kuhusu yeye
 
ngeleja ni pandikizi.. nakwambia atakuja kufa mdomo wazi............ wakati barick na Tanzaniate one wanaviwanja vya ndede kutoka migodini hadi South Africa yeye anabisha nini sasa vitu vipo wazi? Majuzi ndege ilivamiwa na majambazi kule Geita na ilikuwa na vitofali vya dhahabu 24 police walibaini na wakasema .. matokeo yake Mkaguzi wa TRA akakanusha na kusema police ni waongo vitofali vya dhahabu vilikuwa vi4 tuu na si 24 kama police walivyosema......... sas hapo nani mkweli? halafu ndege ilikuwa inaruka kuelekea S. AFRICA!!!!!!!!!!!!!! acheni wizi nyie ngombeeee... halafu Ngeleja emeanza kutuletea mgao wa kisirisiri bila hata kutufahamisha wananchi kuna tatizo gani.... hivi wewe ngeleja ni mke mdogo wa JK au? mbona hujiuzulu pamoja na kashfa zote hizii? una roho ya aina gani we punda?
 
Ngeleja anasumbuliwa na utapia mlo wa kichwa chake! Stupid kabisa.. kwani sie bado ni wa kudanganywa????? Stupid tena kwa mara nyingine!
 
Back
Top Bottom