Waziri Ngeleja asema Dr. Slaa apuuzwe kuhusu utoroshwaji wa madini yetu

Lyimo

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,826
2,017
Waziri wa Nishati na Madini Mh. Williuam Ngeleja amewatakawananchi tupuuze madai yaliyotolewa na Dr. Slaa juu ya ujengwaji wa viwanja vyandege ndani ya migodi kuwa vinawezesha utoroshwaji wa madini yetu. Anasemakabla ndege haijasafirisha mzigo ni lazima ipitie Dar Es Salaam ili ikaguliwemzigo na na maofisa wa Benk Kuu (BoT). Source: Nipashe 19/03/2012
http://www.mwananchi.co.tz/habari/49-uchaguzi-mkuu/21227-ngeleja-dk-slaa-mchochezi-apuuzwe

Mbona nilishasikia toka kwa wazalendo mgodini kuwa kunandege huwa zinaruka toka Bhulyanhkulu hadi South Africa. Ndege hiyo ni Dash 8.Mwenye taarifa za uhakika tushirikishane ili tuweze kuihukumu serikali yetu kwamambo halisi.
 
Nimesoma hiyo habari kwenye gazeti la mwananchi na Ngeleja anasema ndege zote huwa zinaingia na kutoka kwa vibali. Ina maana ile iliyotua KIA na kuondoka na wanyama hai nayo ilifanya vile kwa vibali? Nauliza tu.

Habari yenyewe ni hii hapa chini.

WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja, amesema wananchi wanatakiwa kupuuza madai yanayotolewa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa, kuwa Rais Jakaya Kikwete na Benjamin Mkapa waliruhusu ujenzi wa viwanja vya ndege kwenye migodi ili wawekezaji waweze kupora raslimali za nchi.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Waziri Ngeleja alisema taswira anayotaka kujenga Dk Slaa mbele ya umma ni uchochezi unaojengwa kwa hoja za uongo, kwa sababu anajua ukweli halisi.

“Dk Slaa ni muongo, mchochezi anatakiwa kupuuzwa kwa sababu anachosema siyo kweli...anajua vizuri ukweli halisi lakini anataka kupotosha umma na wananchi wachukie Serikali yao,” alisema Ngeleja.

Alisema duniani kote wawekezaji wanaruhusiwa kujenga viwanja vidogo vya ndege kwa ajili ya kusafirisha vifaa vyao na kuwarahisishia kufika maeneo yao, lakini haviruhusu uporaji wa rasilimali za nchi.

“Labda tukizungumzia usimamizi, lakini kuna maofisa wa Wizara ya Nishati na Madini, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Idara ya Uhamiaji na pia vinasimamiwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, sioni mwanya wa wizi kutokea,” alisema.

Ngeleja alisema kwa mujibu wa sheria za nchi, hakuna ndege inayoruhusiwa kwenda nje bila kibali kutokea kwenye viwanja hivyo, lazima ifike Dar es Salaam ili maofisa wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), waweze kuchukua takwimu.

Alitoa mfano wa wizi uliotokea Mgodi wa Geita, mzigo ulikuwa ukipakiwa kuletwa Dar es Salaam ili kufuata taratibu na kwamba, Dk Slaa anaelewa vizuri lakini anachojaribu kufanya ni kupata umaarufu wa kisiasa kwa kudanganya umma.

Akihutubia Kongamano la wanafunzi wa Chuo Kikuu cha St Augustine (Saut) na baadaye mkutano wa kampeni za udiwani kwenye Uwanja wa Kabohoro, Kata ya Kirumba, Dk Slaa aliwashambulia Rais Kikwete na Mkapa kwa kuruhusu ujenzi wa viwanja hivyo vinavyotumika kupora rasilimali za nchi.

Dk Slaa alisema uwapo wa viwanja hivyo umetoa ruhusa ya mali za nchi kuibwa kwa urahisi, kwa sababu viongozi waliopewa madaraka hawana uchungu na rasilimali hizo.
 
Waziri wa Nishati na Madini Mh. Williuam Ngeleja amewatakawananchi tupuuze madai yaliyotolewa na Dr. Slaa juu ya ujengwaji wa viwanja vyandege ndani ya migodi kuwa vinawezesha utoroshwaji wa madini yetu. Anasemakabla ndege haijasafirisha mzigo ni lazima ipitie Dar Es Salaam ili ikaguliwemzigo na na maofisa wa Benk Kuu (BoT). Source: Nipashe 19/03/2012
http://www.mwananchi.co.tz/habari/49-uchaguzi-mkuu/21227-ngeleja-dk-slaa-mchochezi-apuuzwe

Mbona nilishasikia toka kwa wazalendo mgodini kuwa kunandege huwa zinaruka toka Bhulyanhkulu hadi South Africa. Ndege hiyo ni Dash 8.Mwenye taarifa za uhakika tushirikishane ili tuweze kuihukumu serikali yetu kwamambo halisi.

Wanyama kibao waliotoroshwa kwa ndege la Jeshi la uarabuni lilipitia Dar. Ngeleja kaa kimya kwanza mpaka sasa ningelikuwa mimi usingekuwa waziri hata diwani kutokana na ufisadi uliofanya. Lakini kwa vile uko kwenye chama cha mafisadi shukuru mungu unapata hata kufunua mdomo.
 
Hata mimininajiuliza, hivi hata kama itapita Dar Es Salaam. Je huwa wana scan ndege yotekujua kuwa hakuna madini yaliyofichwa humo ndani ama huwa wanahalalishamanifest (list ya mzigo) wanayopewa na wahusika wa ndege/mgodi. Huo ukaguzihuwa ukojeukoje? Bado sijafuta mashaka yangu.
 
Huyu jamaa anatutia sana aibu vijana;sijapata ona waziri mvivu wa kufikiri kama huyu Ngeleja!Kama kila ndege ya wageni inakaguliwa ikiingia na kabla haijapaa ilikuaje basi TWIGA WETU HAI WAKAONDOKA kupelekwa SAUDIA kimagendo?
 
Madini yanaondoka moja kwa moja asidanganye watu, hata watu wa TRA mzigo wanauonea kwa mbali tu. Huyo Ngeleja mwenyewe anajua na ndio deal zake, asituambie kitu, wameshakula sana na wanaendelea kula kwa sana
 
Huyu anajua Megawati tu hana lolote

Hata megawati hajui, mgao mpk juzi hapa huku ulikuwa unashika hatamu. Tatizo la ukibaraka, anajua kusema alivyoambiwa na aliyemuweka ambaye na yeye naye anasema aliyoambiwa na waliomuwezesha kukaa magogoni, poh!

Madini yanaibiwa na hao wanaoitwa BoT si ni vibaraka tu kama yeye. Kwani wizi wa hapa kwetu si ni mtandao. Juzi hapa kamishna wa madini katuambia tusiwe na wasiwasi na mahesabu kwa sababu madini yanayochimbwa kwa sasa ni 10% tu ya rizevu yetu ya dhahabu kwa hiyo hata kama yataibiwa hamna noma.
 
Yaani saa nyingine ni bura kunyamaza kimya kuficha upumbavu!!Ningekuwa Ngeleja,nisingethubutu kufungua mdomo!!
 
mbona wanyama walibebwa? Huyu megawatt vipi?

Huyu yawezekana alibemendwa na Kakobe. Watani zangu hawana mchezo bana..,kiogoma hoyeeeee!

Wamemtia Ngeleja chikiki kwenye ubongo sasa kichwa hakifanyi kazi vizuri. Twiga kwa ukubwa ule alibebwa bila skana za serikali yetu pamoja na RADA aliyonunu CHENGE kuona, leo hii madini ambayo unayahifadhi bila kuhofia yatakosa pumzi yatashindwa nini kusafirishwa kimya kimya.

Hata haya madawa ya kulevya wanaleta wao humu tusitake kuzugana
 
Hivi hii tabia ya mawaziri kuwaona watanzania hawajui kitu itaisha lini? Hili swala la madini ya nchi kusafirishwa nje ya nchi kwa ndege bila ukaguzi wowote limekuwepo siku zote, mbona tunaofanyakazi kazi katika migodi hii ni sisi watanzania na tunashuhudia haya siku zote!! Waziri ni bora akae kimya katika hili!! inauma sana!!!.
 
Huyu jamaa anatutia sana aibu vijana;sijapata ona waziri mvivu wa kufikiri kama huyu Ngeleja!Kama kila ndege ya wageni inakaguliwa ikiingia na kabla haijapaa ilikuaje basi TWIGA WETU HAI WAKAONDOKA kupelekwa SAUDIA kimagendo?
mkuu wale wanyama hawakupelekwa saudia bali Qatar.
 
Waziri wa Nishati na Madini Mh. Williuam Ngeleja amewatakawananchi tupuuze madai yaliyotolewa na Dr. Slaa juu ya ujengwaji wa viwanja vyandege ndani ya migodi kuwa vinawezesha utoroshwaji wa madini yetu. Anasemakabla ndege haijasafirisha mzigo ni lazima ipitie Dar Es Salaam ili ikaguliwemzigo na na maofisa wa Benk Kuu (BoT). Source: Nipashe 19/03/2012
http://www.mwananchi.co.tz/habari/49-uchaguzi-mkuu/21227-ngeleja-dk-slaa-mchochezi-apuuzwe

Mbona nilishasikia toka kwa wazalendo mgodini kuwa kunandege huwa zinaruka toka Bhulyanhkulu hadi South Africa. Ndege hiyo ni Dash 8.Mwenye taarifa za uhakika tushirikishane ili tuweze kuihukumu serikali yetu kwamambo halisi.
kweli we ni noma, yaani mpaka ndege iliyohewani unajua kuwa hii inaenda dar na hii south A. Du!
 
Huku Namtumbo kuna kiwanja kubwa kabisa la ndege madege makubwa makubwa yanakuja na kutoka yanabeba uranium hakuna wa kuhoji.
Ngeleja akija anatulizwa anapewa kitu kidogo, wakiona kuna watu wanachonga sana wote wanahongwa afu wanakuwa wapoleeeeeeeee.
Swali viongozi wa kamati ya madini na nishati hawaoni haya wanaojifanya wazalendo kama akina January Makamba, John Mnyika hamuoni haya?
Dr Slaa akiungana na viongozi wengine na wanaharakati kwa nini wasimuunge mkono ili na sisi wananchi tuungane kupinga haya. Its time to fight for our right.
 
Back
Top Bottom