Waziri Ngeleja: Acha wananchi waumie, lakini ongezeko la umeme ni palepale | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Ngeleja: Acha wananchi waumie, lakini ongezeko la umeme ni palepale

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by chamajani, Dec 24, 2010.

 1. c

  chamajani JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2010
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kauli za kejeli zinazidi kutolewa na viongozi wetu baada ya Waziri ngeleja kuueleza umma kupitia TBC kuwa hata kama wananchi wataumia kiasi gani, gharama za umeme lazima zipande.

  Akazidi kueleza kuwa gharama zenyewe ni kati ya sh. 9-11 na.., so hakuna haja ya watanzania kuhamaki na kuchukua hatua za nguvu umma kwa ongezeko hilo.

  Lakini ni kweli 18.5% ni asilimia ndogo kwa wanaojua mathematics?
   
 2. Gobegobe

  Gobegobe JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 245
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hata kama itakuwa ndogo vyovyote vile, bado ni nyongeza ya mzigo wa mateso kwa watanzania wengi. Hasa ikizingatiwa kuwa kwao hakuna nyongeza yoyote ya kipato, zaidi ni kuzidi kuporomoka kila uchao. YANA MWISHO!!!
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Wacha wafanye madudu kwani hayo ni mambo yatakayowapiga na kuwagaraza 2015,yaani hizo ni kura za ccm zinahama tu ,we wacha tu !
   
 4. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2010
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  Sio swala la kushangaza yaani sioni jipya. Serikali inajulikana kuwa haipo kwa manufaa ya wananchi ila kwa kundi la watu wachache. Kwa ujumla nchi imetekwa. Tunazungwa kwa uchaguzi kisha kikundi kile kile kinarudi kwa kasi, hari na nguvu zaidi. So hayo ndio matunda ya kutoelewa kwa wengi wetu.
   
 5. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #5
  Dec 24, 2010
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Unajua jana wakati namsikiliza Ngeleja na jamaa toka Tanesco na Uwura, nilikumbuka hadith ya mke mmoja wa mfalme huko ufaransa. Wananchi walipokuwa na hali ngumu ya maisha waliamua kufanya mgomo na mke wa mfalme akauliza hawa wanapiga kelele za nini?? Mumewe ambaye ni mfalme akamjibu mkewe kuwa wanalalamika kuwa bei ya mkate imepanda hivyo wanataka ishuke. Mkewe akamwambia si wale keki???. Ndio hii kesi ya jana, Ngeleja anasema bei yenyewe iliyopanda ni sh 9 hadi 28 tu, anaziona ni ndogo saana. Sh 28 kwa uniti moja, kama nina nunua unit 250 kwa mwezi ni sawa na ongezeko la sh 7000/= kwa mwezi. Je hiki kiwango ni kidogo??? yeye anasema ni 28 tu?? Jamani kwa kuwa yeye halipi bei ya umeme ndio maana haoni kama ni ghali. Ngeleja analipiwa kila kitu na serikali, Anausafiri wa umma, mafuta ya serikali, nyumba ya serikali, maji na umeme serikali inalipa mshahara wake ni wa masuala yake binafsi hivyo haoni uzito wa kupanda kwa bei ya umeme. Ni kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa.
   
 6. FORTALEZA

  FORTALEZA JF-Expert Member

  #6
  Jul 10, 2017
  Joined: Jan 1, 2017
  Messages: 702
  Likes Received: 1,313
  Trophy Points: 180
  Shikamoo Ngeleja
   
 7. Yamakagashi

  Yamakagashi JF-Expert Member

  #7
  Jul 10, 2017
  Joined: Sep 19, 2016
  Messages: 4,425
  Likes Received: 7,563
  Trophy Points: 280
  Hahaha dah

  "Tecno Whatever "
   
 8. Z

  ZE NDINDINDI JF-Expert Member

  #8
  Jul 10, 2017
  Joined: Sep 19, 2016
  Messages: 1,482
  Likes Received: 2,999
  Trophy Points: 280
  jamaa mzalendo sana aisee,makonda oyee,ngeleja oyeee,le mutuz coco channel oyee
   
 9. IKOWA

  IKOWA JF-Expert Member

  #9
  Jul 10, 2017
  Joined: Jan 18, 2013
  Messages: 808
  Likes Received: 491
  Trophy Points: 80
  Na ndo maana kwenye kamgawo alikuwemo kwa sababu alitetea kupandishwa Kwa umeme ambapo ilimuongezea percent Bwana Rugemalila
   
 10. s

  scooman JF-Expert Member

  #10
  Jul 10, 2017
  Joined: Mar 21, 2017
  Messages: 2,502
  Likes Received: 2,089
  Trophy Points: 280
  Du nyuzi za 2010 zinarudi humu
   
 11. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #11
  Jul 10, 2017
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  yaani Ngeleja hafai hata kama karudisha milioni 40.4
  tete ndiye aliyeuza dili nzima la ulaji huko PAP & IPTL
  leo anakataa nini pesa ya Ruge?
   
Loading...