Waziri: NEMC saidieni viwanda si kuvifunga

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
WAZIRI Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Ummy Mwalimu, ameliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuwasaidia wamiliki wa viwanda kudhibiti uchafu na kutunza mazingira, badala ya kufunga viwanda vyao na kuwatoza.

Waziri Ummy alisema hayo jana katika ziara yake ya siku moja kukagua viwanda ambavyo vimekuwa vikilalamikiwa kwa utoaji wa vumbi ambayo imekuwa kero kwa wananchi wa jijini Tanga.

Alisema upo mwongozo na kanuni za kufuata katika kudhibiti uchafuzi unaofanywa na viwanda, hivyo NEMC wahakikishe wanafuatilia kwa ukaribu ili kudhibiti hali hiyo.

"Viwanda tunavipenda kwani ni sehemu ya ukuzaji wa uchumi wetu, hivyo niwatake baraza badala ya kufanya kazi kama askari, anzeni kufanya ufuatiliaji kwenye viwanda hasa vile vya saruji na chokaa ili kuhakikisha wanafunga mitambo ya kudhibiti vumbi," alisema.

Alizitaka halmashauri zote nchini kuweka mpango wa utunzaji wa mazingira utakaobainisha shughuli zote zitakazofanywa na udhibiti na utunzaji wa mazingira ili kujipima kila ifikapo mwisho wa mwaka.

Alisema miongoni mwa vipaumbele hivyo, ni ujenzi wa madampo ya kisasa ili kudhibiti uchafuzi na uanzishwaji wa mashamba ya miti ili kufikia malengo ya upandaji miti milioni 1.5 yaliyoelekezwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu.

Mkurungenzi wa kiwanda cha kuzalisha chokaa cha Neelkanth, Rashid Liemba, aliiomba serikali kuweka utaratibu wa kuwatembelea wenye viwanda ili kubaini changamoto zinazowakabili, badala ya kusubiri ziara za viongozi.

Akiwa katika Shule ya Sekondari ya Don Bosco, Waziri Ummy alitoa siku saba kwa NEMC kwenda shuleni hapo kuchunguza athari za kimazingira zinazotokana na uzalishaji wa klinka unaofanywa na Kiwanda cha Saruji Rhino, kilichopo jirani na shule hiyo.

Akitoa malalamiko ya uwepo wa vumbi na makelele yanayotokana na uendeshaji wa mitambo, Meneja wa Shule hiyo, Sebastian Mlacha, alisema wanafunzi wamethirika na kuugua kifua pamoja na ngozi.

"Tunaomba utusaidie waziri kwani hiki kiwanda kilitukuta shule, lakini sasa wanafunzi wanashindwa kujisomea nyakati za usiku kutokana na vumbi linaloachiwa na kiwanda, pamoja na kelele za mitambo," alisema.
 
NEMC ni kikwazo cha maendeleo ya kukua kwa viwanda Tanzania, badala ya kutoa Elimu wao wapo busy kupiga fine tu na kufunga viwanda nchi itaendelea hivyo kweli hapo.
 
Hao NEMC ni pepo la kuzuia maendeleo, ukifika kuomba kufanyiwa environment impact assessment wanakupiga 20 millions. Na Bila wao hupewi leseni ya uwekezaji.
 
NEMC ni kikwazo cha maendeleo ya kukua kwa viwanda Tanzania, badala ya kutoa Elimu wao wapo busy kupiga fine tu na kufunga viwanda nchi itaendelea hivyo kweli hapo.
Kiukweli bila NEMC basi mji kama Dsm ungejaa takataka za kila aina yake
Na maeneo mengi ya migodi ingekuwa ni shida. Mm ninavyo fahamu NEMC sio kikwazo cha maendeleo ya viwanda sio kila Mradi mkubwa unafanyiwa EIA
Kuna hatua kadhaa hufuatwa.
 
Hao NEMC ni pepo la kuzuia maendeleo, ukifika kuomba kufanyiwa environment impact assessment wanakupiga 20 millions. Na Bila wao hupewi leseni ya uwekezaji.
Mara nyingi maendeleo wanayoyahubiri, ni maendeleo ya familia zao sio nchi
 
Back
Top Bottom