Waziri Ndugulile, kwanini redio Stations za Tanzania zinaishia Magomeni na Kirumba?

ram

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
8,370
2,000
Nakumbuka wakati tunakua miaka ile, ikifika jioni radio Tanzania haisikiki vizuri lkn ukitune KBC utadhani mtangazaji yuko hapo nyuma ya nyumba, kwa hiyo hili tatizo ni la enzi
 
Mashimba Son

Verified Member
Dec 22, 2014
989
1,000
Hiki kitu TCRA walishughulikie haraka ukienda Silali,Rombo,Ngara Radio za Tanzania hazisikiki kwa ufasaha bali Radio za nje tu kiasi kwamba hata wananchi wa huko wamekuwa na tamaduni za nje, maana hata matangazo wanasikiliza ya nchi hizo jirani.!
 
Koffi Annan

JF-Expert Member
Dec 23, 2018
775
1,000
Sasa hivi ata nikiwa area tofauti nasikiliza radio za kenya online maana ndizo nimezoea tokea mdogo
 
Darmian

JF-Expert Member
Oct 1, 2017
12,748
2,000
Ni kweli unachosema. Kwa mfano hapa mpakani ,redio za Kenya zipo strong sana mfano redio citizen,kbc taifa, milele fm,kbc english service n.k. hata mtandao kama safaricom wa Kenya huwa una meza sana Vodacom au tigo huku mpakani.. tulio huku wilaya ya rombo tunaelewa hii adha tuipatayo.
Nimesoma advance Rombo,,usiku nilikuwa nakula ngoma za majuu kutoka Capital radio ya Kenya,,mchana naibia kumsikiliza Willy M Tuva Citizen Radio kwa high definition kabisa,,basi hapo ni mimi na muziki + physics tu..Na-feel unachokizungumza hapa
 
Darmian

JF-Expert Member
Oct 1, 2017
12,748
2,000
Rombo radio ya Tanzania inayoshika
Clear n Radio Maria Tanzania pekeake,
Na hii n kwasababu waliweka mnara wao
Pale user kwenye kanisa Catholic
December nilikuwa huko Clouds nao wanafika..nikiwa Mamsera napata mbege pale nilikuwa nawapata clear kabisa
 
makaveli10

JF-Expert Member
Mar 27, 2013
16,810
2,000
Moderators naomba hii kero muifikishe kwa waziri Ndugulile
Kuna kauli ilikuja kichwani nilitaka kusema "moderators wenyewe chawa tu, wanafikishaje huko" ila nikasita, si kauli nzuri kabisa. Kibinadamu sio fresh
 
Mr PJ

Member
Jul 1, 2018
79
150
Mtoa mada umezungumza ukweli sana, nilipo radio za Kenya ndio zenyewe sasa mwaka juzi nikasafiri kwenda Mbeya nikawa pale tukuyu kwa muda aisee kila nikibadili station nyingi napata za Malawi mwanzoni nilidhani ni redio ya kilugha ila nikawa naambiwa ni za Malawi. Radio zaa Tanzania zinazovuka boda ama hata kufika mipakani ni Radio Free Africa tu ila ttzo lake naona hawana stable management umeme ukikatika nayoinakatika na mara nyingine kupotea hewani siku nyingi bila kujua sbb za msingi. Watz tubadilike tupo nyuma sana na smtm huwa tunadanganyana sana.
 
Tachu hano

JF-Expert Member
May 30, 2016
1,277
2,000
Duh kabisa maana huku TARIME zimetawala redio za kenya
kBC taifa
Milele fm
Radio jambo
Citizen Radio
Radio maisha.
Kisumu .

Hizo ni za kiswahili bado kuna radio zinazotangasa kwa vilugha hasa kijaluo
Mfano Radio Ramoghi ( kama nimekosea nisahihishwe).

Hapa nilipo tz inashika redio free tu napo kwa mashaka mashaka
Nyingine ni TBC taifa, Fm na clouds siku moja moja ikijisikia..
 
nkumbison

JF-Expert Member
Sep 22, 2013
1,904
2,000
Hivi kwa nini Tanzania tunafeli sana hata kwa vitu vidogo? Waziri wa habari, Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia anajua kuwa asilimia 90 ya Watanzania wanaoishi pembezoni mwa Tanzania(mpakani) wanasikiliza redio za nchi jirani?

Kwa mfano sisi tunaoishi mpakani na Kenya redio stations za Kenya zipo strong kuliko redio za Tanzania, kwa kifupi Watanzania wanaoishi mpakani na Kenya wanaotumia redio kupata habari wanapata habari za Kenya kuliko za Tanzania.

Redio stations za Tanzania hazipatikani kabisa, Redio iliyokuwa inajaribu ni Radio Free Afrika, lakini ina wiki tangu itoweke hewani,lakini redio zingine zilizobaki za Tanzania ndo hamna kabisa.

Waziri husika miaka 60 ya uhuru na dunia ya sayansi na teknolojia ni mshangao kuwa asilimia 99 za redio za Tanzania zinaishia magomeni ni aibu kubwa.

Siyo redio tu hata simu, mitandao ya nchi jirani inakuwa na nguvu kuliko ya Tanzania, yaani mtandao wa Kenya kuingia kwenye simu yako ni kugusa na ukumbuke upo mita 500 ya mnara wa Tanzania, lakini mnara wa Kenya upo zaidi ya km 50 lakini unavamia wa Tanzania unaingia kwenye simu yako na unakaribishwa na SMS welcome in Kenya na upo Tanzania.

Waziri Ndugulile hili swala linakera na kuudhi na ni aibu kubwa kwa nchi yetu.
Nisoma kwa rafudhi ya Kikurya
 
Cosovo

JF-Expert Member
Jul 8, 2018
376
1,000
Mtoa mada umezungumza ukweli sana, nilipo radio za Kenya ndio zenyewe sasa mwaka juzi nikasafiri kwenda Mbeya nikawa pale tukuyu kwa muda aisee kila nikibadili station nyingi napata za Malawi mwanzoni nilidhani ni redio ya kilugha ila nikawa naambiwa ni za Malawi. Radio zaa Tanzania zinazovuka boda ama hata kufika mipakani ni Radio Free Africa tu ila ttzo lake naona hawana stable management umeme ukikatika nayoinakatika na mara nyingine kupotea hewani siku nyingi bila kujua sbb za msingi. Watz tubadilike tupo nyuma sana na smtm huwa tunadanganyana sana.
Hili ni tatizo mkuu,kama hapo RFA imeisha potea wiki 2 ,kila nikitafuta station ya kusikiliza ni za Kenya ,bila mitandao ya kijamii huwezi ukajua kinachoendelea Tanzania
 
Shoctopus

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
2,862
2,000
Hivi kwa nini Tanzania tunafeli sana hata kwa vitu vidogo? Waziri wa habari, Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia anajua kuwa asilimia 90 ya Watanzania wanaoishi pembezoni mwa Tanzania(mpakani) wanasikiliza redio za nchi jirani?

Kwa mfano sisi tunaoishi mpakani na Kenya redio stations za Kenya zipo strong kuliko redio za Tanzania, kwa kifupi Watanzania wanaoishi mpakani na Kenya wanaotumia redio kupata habari wanapata habari za Kenya kuliko za Tanzania.

Redio stations za Tanzania hazipatikani kabisa, Redio iliyokuwa inajaribu ni Radio Free Afrika, lakini ina wiki tangu itoweke hewani,lakini redio zingine zilizobaki za Tanzania ndo hamna kabisa.

Waziri husika miaka 60 ya uhuru na dunia ya sayansi na teknolojia ni mshangao kuwa asilimia 99 za redio za Tanzania zinaishia magomeni ni aibu kubwa.

Siyo redio tu hata simu, mitandao ya nchi jirani inakuwa na nguvu kuliko ya Tanzania, yaani mtandao wa Kenya kuingia kwenye simu yako ni kugusa na ukumbuke upo mita 500 ya mnara wa Tanzania, lakini mnara wa Kenya upo zaidi ya km 50 lakini unavamia wa Tanzania unaingia kwenye simu yako na unakaribishwa na SMS welcome in Kenya na upo Tanzania.

Waziri Ndugulile hili swala linakera na kuudhi na ni aibu kubwa kwa nchi yetu.
Bado wanjenga ocean road ya pili inayopita baharini

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
usser

JF-Expert Member
Sep 25, 2015
12,730
2,000
December nilikuwa huko Clouds nao wanafika..nikiwa Mamsera napata mbege pale nilikuwa nawapata clear kabisa
Kabsa clouds wanajitahid Ila ukivuka
Mamserea na ukipita pale wilayan rombo
Kwenda mbele hapo ndo kizungu mkuti kinaanzia ina ngumu kuwapata clear
 
Kiyoya

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,613
2,000
Sie wa kigoma tumerahisishiwa maana redio zinaongea lugha ya asili.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom