Waziri Ndugulile, kwanini redio Stations za Tanzania zinaishia Magomeni na Kirumba?

Cosovo

JF-Expert Member
Jul 8, 2018
376
1,000
Hivi kwa nini Tanzania tunafeli sana hata kwa vitu vidogo? Waziri wa habari, Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia anajua kuwa asilimia 90 ya Watanzania wanaoishi pembezoni mwa Tanzania(mpakani) wanasikiliza redio za nchi jirani?

Kwa mfano sisi tunaoishi mpakani na Kenya redio stations za Kenya zipo strong kuliko redio za Tanzania, kwa kifupi Watanzania wanaoishi mpakani na Kenya wanaotumia redio kupata habari wanapata habari za Kenya kuliko za Tanzania.

Redio stations za Tanzania hazipatikani kabisa, Redio iliyokuwa inajaribu ni Radio Free Afrika, lakini ina wiki tangu itoweke hewani,lakini redio zingine zilizobaki za Tanzania ndo hamna kabisa.

Waziri husika miaka 60 ya uhuru na dunia ya sayansi na teknolojia ni mshangao kuwa asilimia 99 za redio za Tanzania zinaishia magomeni ni aibu kubwa.

Siyo redio tu hata simu, mitandao ya nchi jirani inakuwa na nguvu kuliko ya Tanzania, yaani mtandao wa Kenya kuingia kwenye simu yako ni kugusa na ukumbuke upo mita 500 ya mnara wa Tanzania, lakini mnara wa Kenya upo zaidi ya km 50 lakini unavamia wa Tanzania unaingia kwenye simu yako na unakaribishwa na SMS welcome in Kenya na upo Tanzania.

Waziri Ndugulile hili swala linakera na kuudhi na ni aibu kubwa kwa nchi yetu.
 
mcTobby

JF-Expert Member
Feb 16, 2018
458
1,000
Ni kweli unachosema. Kwa mfano hapa mpakani ,redio za Kenya zipo strong sana mfano redio citizen,kbc taifa, milele fm,kbc english service n.k. hata mtandao kama safaricom wa Kenya huwa una meza sana Vodacom au tigo huku mpakani.. tulio huku wilaya ya rombo tunaelewa hii adha tuipatayo.
 
vvm

JF-Expert Member
Jul 18, 2014
4,240
2,000

Aisee umenikumbusha William Tuva, Torome Tirike, Mohamed Juma njuguna wa Citizen na Mwala wa KBC radio capital ya kenya ilikua inapiga mziki wenye quality sana (HD) kupata radio ya Tanzania uliyakiwa uwe na AM radio upandishe Antenna juu ya mti Mkubwa sana na hapo unapata RTD, Radio One na free Africa especially usiku ikifika saa moja mawimbi yanapotea unasikia miluzi ila redio za Kenya zilikua zinashika loud and clear FM tuu... Back in our days hatukulalamika maana Kenya was like part of us hata wakamba walikua wanakuja sana kuleta nyanya bamia na vitunguu na wao wanarudi na ndizi kutoka Tz shopping kubwa kubwa unaenda Mombasa so it wasn't a big deal.
 
Yeap aisee ndio hivyo .hadi sasa redio za Kenya zipo HD sana ukisikiliza. Huku kwetu wamefanya kila kitu ni siasa .kila kitu yaani.
 
Cosovo

JF-Expert Member
Jul 8, 2018
376
1,000
Ni kweli unachosema. Kwa mfano hapa mpakani ,redio za Kenya zipo strong sana mfano redio citizen,kbc taifa, milele fm,kbc english service n.k. hata mtandao kama safaricom wa Kenya huwa una meza sana Vodacom au tigo huku mpakani.. tulio huku wilaya ya rombo tunaelewa hii adha tuipatayo.
Mkuu umeeleza nikahisi upo Tarime,yaani hali ya Rombo ni sawa na Tarime
 
usser

JF-Expert Member
Sep 25, 2015
12,735
2,000
Ni kweli unachosema. Kwa mfano hapa mpakani ,redio za Kenya zipo strong sana mfano redio citizen,kbc taifa, milele fm,kbc english service n.k. hata mtandao kama safaricom wa Kenya huwa una meza sana Vodacom au tigo huku mpakani.. tulio huku wilaya ya rombo tunaelewa hii adha tuipatayo.
Kama nakuona vile hapo tarakea ukinywa zako
Mbege
 
usser

JF-Expert Member
Sep 25, 2015
12,735
2,000
Yaani ndio hivyo mkuu... Huko naona mmepakana na county ya migori huku tumepakana na county ya kajiado. Ila unajua nini mdau, watangazaji 2a redio kenya wanajielewa Sana kuliko hawa wa kwetu..
Bongo wanabana Sana pua na kuigana Sana
Mtangazaji wa kujitambua Tanzania n Millard Ayo pekeake hawa wengine hamna kitu
 
usser

JF-Expert Member
Sep 25, 2015
12,735
2,000
Rombo radio ya Tanzania inayoshika
Clear n Radio Maria Tanzania pekeake,
Na hii n kwasababu waliweka mnara wao
Pale user kwenye kanisa Catholic
 
Chen Hu

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
3,745
2,000
Nakumbuka miaka ya Nyuma kidogo kule Ludewa maeneo fulani tulikuwa tunasikiliza radio za Malawi ambazo hata lugha ilikuwa ngumu. Radio za tz ilikuwaga mpaka usiku.
 
Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
23,092
2,000
Ni kweli unachosema. Kwa mfano hapa mpakani ,redio za Kenya zipo strong sana mfano redio citizen,kbc taifa, milele fm,kbc english service n.k. hata mtandao kama safaricom wa Kenya huwa una meza sana Vodacom au tigo huku mpakani.. tulio huku wilaya ya rombo tunaelewa hii adha tuipatayo.
Hata kule LITUHI, wilaya ya Nyasa, moani Ruvuma, redio za Malawi zipo strong sana kuliko za Tanzania
 
Magabo

Member
May 20, 2021
85
125
Aisee umenikumbusha William Tuva, Torome Tirike, Mohamed Juma njuguna wa Citizen na Mwala wa KBC radio capital ya kenya ilikua inapiga mziki wenye quality sana (HD) kupata radio ya Tanzania uliyakiwa uwe na AM radio upandishe Antenna juu ya mti Mkubwa sana na hapo unapata RTD, Radio One na free Africa especially usiku ikifika saa moja mawimbi yanapotea unasikia miluzi ila redio za Kenya zilikua zinashika loud and clear FM tuu... Back in our days hatukulalamika maana Kenya was like part of us hata wakamba walikua wanakuja sana kuleta nyanya bamia na vitunguu na wao wanarudi na ndizi kutoka Tz shopping kubwa kubwa unaenda Mombasa so it wasn't a big deal.
Kweli na asproooo!!!
 
  • Thanks
Reactions: vvm

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
4,059
2,000
Waziri Ndugulile ana kazi muhimu sana ya kuhakikisha sheria ya kila mwananchi ana laini moja, msimsumbue !
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom