Waziri ndani ya sakata la Muro, ni yupi huyo ?


Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Messages
9,980
Likes
8,314
Points
280
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined May 31, 2008
9,980 8,314 280
Waziri ndani ya sakata la Muro
- na mwandishi wa Gazeti la Raina Mwema
Achunguzwa kwa mahusiano na waliotimuliwa Bagamoyo !!

WAZIRI Mwandamizi katika serikali ya Rais Jakaya Kikwete, anahusishwa na sakata lililomsibu Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Jerry Muro, na sasa uchunguzi dhidi yake unaendelea, Raia Mwema limefahamishwa.
Habari za ndani ya Serikali zimeeleza kwamba vyombo vya dola vimeshitushwa na taarifa za kuhusika kwa waziri huyo ambaye taarifa zake zimekutwa kwa Muro na wenzake wawili Edmud Kapama na Deogratias Mgasa.
Kwa mujibu wa habari hizo, vyombo vya dola vilipowapekua na kuwahoji Muro na wenzake vilipata ushahidi wa waziri huyo kuwa na ‘mahusiano’ na watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, waliotimuliwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Waliotimuliwa madarakani na Pinda ni Mkurugenzi Mtendaji Rhoda Nsemwa; Mweka Hazina, Michael Karol Wage; Ofisa Kilimo, Mifugo na Ushirika, Naftal Rhemtullah; Ofisa Mipango, Aloyce Gabriel na Mkaguzi wa Ndani, Abdul Mwinyi.
“Jerry Muro na wenzake walikutwa na ushahidi unaoonyesha kwamba waziri (anamtaja jina) alikuwa akinufaika na fedha za ubadhirifu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo. Walikuwa na ushahidi wa gari ambalo Waziri huyo amenunuliwa na liko Morogoro katika sehemu ya biashara zake,” kinaeleza chanzo cha habari serikalini.
Raia Mwema limefahamishwa kwamba vyombo vya dola kwa pamoja sasa vinachunguza jinsi waziri huyo (jina tunalo) alivyonufaika na fedha kutoka halmashauri hiyo ya Bagamoyo na sababu za mmoja wa watumishi hao kutoa fedha kwa waziri huyo.
“Unajua wanaangalia mahusiano kati ya Waziri huyo na mmoja wa watumishi waliofukuzwa kazi na Waziri Mkuu, maana lazima Serikali ijiridhishe walitoa fedha kwake kwa maslahi gani na kama wana mahusiano ya binafsi, kibiashara ama ya kikazi kabla ya kuchukua maamuzi na pia kina Muro na wenzake walizipataje hizo taarifa na walikuwa wanazitumia kwa malengo gani,” anaeleza Ofisa Mwandamizi serikalini.
A complete failed system, how sad ! Kwa habari zaidi bonyeza hapa
http://www.raiamwema.co.tz/news.php?d=2037
 
Oxlade-Chamberlain

Oxlade-Chamberlain

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Messages
7,964
Likes
187
Points
160
Oxlade-Chamberlain

Oxlade-Chamberlain

JF-Expert Member
Joined May 26, 2009
7,964 187 160
kazi hipo,"ufisadi" sasa umekuwa tabia ya kawaida na jambo la kawaida kwenye kila kona ya serikali yetu.watu wanafanya ufisadi bila uoga kwa vile wanajua hakuna hatua zozote zitazochukuliwa kwani wachafu wako wengi kama sio wote.
 

Forum statistics

Threads 1,251,745
Members 481,857
Posts 29,783,410