Waziri Ndalichako: Wakuu wa vyuo vyote wawapime wanafunzi wao dawa za kulevya

Kifurukutu

JF-Expert Member
Aug 29, 2013
4,628
6,669
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amewaagiza wakuu wote wa vyuo nchini kuwatambua wanafunzi wao wanaojihusisha na matumizi ya dawa za kulevya na kupeleka taarifa kwake.

Profesa Joyce Ndalichako ambaye ni mjumbe wa Tume ya Kudhibiti Dawa ya kulevya kutokana na wadhifa wake ametoa kauli hiyo leo wakati akifungua kikao cha kazi cha wakuu wa vyuo vya maendeleo ya wananchi (FDCs) kilichofanyika katika ukumbi wa Veta mjini hapa.

Amesema agizo hilo amelitoa kwa wakuu wa vyuo vyote nchini kuona kuwa wanakuwa makini kuhakikisha kuwa kwanza vyuo vyao havigeuzwi kuwa vijiwe vya watu wanaotumia madawa ya kulevya lakini pili kuwatambua vijana wote wanaosoma katika vyuo vyao kama wanatumia madawa ya kulevya.

“Kama serikali tumejiwekea malengo ya kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 kwa kujenga viwanda na rasilimali kubwa tunayoitegemea ni vijana wetu walioko mashuleni, hivyo kama juhudi za makusudi hazitafanyika katika kupambana na madawa ya kulevya malengo yetu hayatafikiwa kwa kuwa madawa ya kulevya yanaharibu vijana wetu,” alisema Profesa Ndalichako.

Amesema vijana wengi walioko vyuo vikuu wameharibikiwa kutokana na madawa ya kulevya hivyo nguvu kubwa inahitajika katika mapambano hayo ili kulinusuru taifa kwa kuwa wizara hiyo ndiyo yenye dhamana kubwa ya kuhakikisha kuwa Tanzania ya viwanda inafikiwa.

“Hii vita ya madawa ya kulevya siyo ya lelemama inatakiwa ujitoe mhanga kwa kuwa tunapambana na watu wenye nguvu,” alisema Profesa Ndalichako.

Mbali na hilo ameviagiza vyuo vya maendeleo ya Wananchi kuhakikisha kuwa vinajitangaza kwa jamii ili vionekane kuwa vipo kwa kuwa vyuo vingi havina wanafunzi wa kutosha huku ikibainika kuwa chuo kimojawapo (hakukitaja jina) kina mwanafunzi mmoja tu
 
Daah! Tanzania nchi yangu. Sidhani kama ni lazima kuongea tu hata kama hauna la maana la kusema, si bora wakae kimya tu. Makamba nae juzi kachukua polisi kwenda kiwanda cha konyagi kukamata viroba just mtu aonekane kasema kitu au kafanya kitu. Hovyo kabisa.
 
(Ndio wanachokiweza)
Watakuja na matamko mengi, nangoja mashinikizo ya kupima;
Ukimwi
Nguvu za kiume
Idadi ya weupe na weusi
Waliosuka nywele.
 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amewaagiza wakuu wote wa vyuo nchini kuwatambua wanafunzi wao wanaojihusisha na matumizi ya dawa za kulevya na kupeleka taarifa kwake.

Profesa Joyce Ndalichako ambaye ni mjumbe wa Tume ya Kudhibiti Dawa ya kulevya kutokana na wadhifa wake ametoa kauli hiyo leo wakati akifungua kikao cha kazi cha wakuu wa vyuo vya maendeleo ya wananchi (FDCs) kilichofanyika katika ukumbi wa Veta mjini hapa.

Amesema agizo hilo amelitoa kwa wakuu wa vyuo vyote nchini kuona kuwa wanakuwa makini kuhakikisha kuwa kwanza vyuo vyao havigeuzwi kuwa vijiwe vya watu wanaotumia madawa ya kulevya lakini pili kuwatambua vijana wote wanaosoma katika vyuo vyao kama wanatumia madawa ya kulevya.

“Kama serikali tumejiwekea malengo ya kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 kwa kujenga viwanda na rasilimali kubwa tunayoitegemea ni vijana wetu walioko mashuleni, hivyo kama juhudi za makusudi hazitafanyika katika kupambana na madawa ya kulevya malengo yetu hayatafikiwa kwa kuwa madawa ya kulevya yanaharibu vijana wetu,” alisema Profesa Ndalichako.

[http://dashboard]

Amesema vijana wengi walioko vyuo vikuu wameharibikiwa kutokana na madawa ya kulevya hivyo nguvu kubwa inahitajika katika mapambano hayo ili kulinusuru taifa kwa kuwa wizara hiyo ndiyo yenye dhamana kubwa ya kuhakikisha kuwa Tanzania ya viwanda inafikiwa.

“Hii vita ya madawa ya kulevya siyo ya lelemama inatakiwa ujitoe mhanga kwa kuwa tunapambana na watu wenye nguvu,” alisema Profesa Ndalichako.

Mbali na hilo ameviagiza vyuo vya maendeleo ya Wananchi kuhakikisha kuwa vinajitangaza kwa jamii ili vionekane kuwa vipo kwa kuwa vyuo vingi havina wanafunzi wa kutosha huku ikibainika kuwa chuo kimojawapo (hakukitaja jina) kina mwanafunzi mmoja tu

Idea ni nzuri lakini utekelezaji naona hauko sahihi.Nilitegemea kuwepo na somesort of a seminar au training wakati wa kuwadahili wanafunzi na kuwapa changamoto hizo pia kuwaomba kama wanatumia wajiongoze wenyewe ili wasaidiwe kuikabili shida yao.

Kwenda kisiasa hatuisaidii jamii,kuna watoto wanaanza wakiwa primary schools au secondary hasa tunazoziita academy au English medium,ni issue ya maelewano kuliko nguvu
 
Awapime walimu wake make wengi akili zao zimejaa Giza ndo maana migogoro mashule haiishi
 
Back
Top Bottom