Waziri Ndalichako tunaomba utoe tamko kuhusu mwongozo wa elimu baada ya shule kufunguliwa, kuna shule wamebuni michango yao

Enzi na Enzi

JF-Expert Member
May 29, 2020
888
821
Katika shule moja iliyopo wilaya ya Magu, ambayo ni Sekondari ya kata watoto wanatakiwa kupeleka kilo kumi za mchele kila mmoja, hayo ni maelekezo waliyopewa watoto kutuambia wazazi.

Shule ina wanafunzi wastani wa 2000×10 = kg 20,000/= na pesa tsh.2000@ mwanafunzi ambazo ni tsh. 4,000,000/=

Huu mchele ni kama tani 20
Na pesa 4ml.
Je, nimaelekezo ya Serikali?

Kuna mchezo siku hizi unatumiwa na walimu na baadhi ya kamati za shule, wanaita baadhi ya wazazi halafu wanadai wazazi walikubaliana,

Naomba Waziri uje na tamko maana sisi elimu bure siku hizi siyo elimu bure kwa kutumia mbinu hizi.

Tunaomba tamko maana naona walimu wanataka kupiga mchele na pesa kwa kigezo cha kuongeza muda wa masomo shuleni.
 
Mkuu usikurupuke kuangalia Jumla inayochangwa,,SIJUI Millioni nne ama tani 20!.. Jambo la kwanza kujiuliza ,,Nini lengo la matumizi ya huo mchele na pesa kama ilivyo ombwa na shule?. kama ni kwa ajili ya chakula cha watoto wawapo shuleni piga hesabu nyepesi,, Je kiasi hicho kinakadiriwa kutumika kwa muda gani?.. Je kipo katika uwiano sawa ie.

1kg watu 4... kisha ndo uje na hoja ya upigaji kwa walimu.. MUDA ULIOPOTEA LAZIMA UFIDIWE JE MWANAO ATASHINDA NJAA SHULENI?.. Mwisho wa Siku sio kesi UNAWEZA usilipe na mwanao akashinda na njaa shulenii,,,,,hili ki malezi tarajia changamoto,,kama ni wa kike na ameivaa watu wataanza kuvuna ili apate buku mbili A chipsi,,,na kama ni dume litatafuta plan B ili lipate kula,,,hapo lolote litatokea,,,,,ELIMU NI GHARI
 
Mkuu usikurupuke kuangalia Jumla inayochangwa,,SIJUI Millioni nne ama tani 20!.. Jambo la kwanza kujiuliza ,,Nini lengo la matumizi ya huo mchele na pesa kama ilivyo ombwa na shule?. kama ni kwa ajili ya chakula cha watoto wawapo shuleni piga hesabu nyepesi,, Je kiasi hicho kinakadiriwa kutumika kwa muda gani?.. Je kipo katika uwiano sawa ie. 1kg watu 4... kisha ndo uje na hoja ya upigaji kwa walimu.. MUDA ULIOPOTEA LAZIMA UFIDIWE JE MWANAO ATASHINDA NJAA SHULENI?..
Tatizo sio kuchangia pesa au chakula kwa mtoto Ila tatizo hivyo vitolewavyo je vitatumika kwa mujibu wa maelezo na dhumuni ya watoaji!!!? Kumbuka vile vile ni muhimu kupata maelezo Kama ni maelekezo ya wizara ya elimu ukizingatia kauli mbiu ni elimu bure kwa kila mtoto wa mkulima wa nchi hii...

Sent from my itel S32 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu jiongeze baas, buku 2 tu zinakutoa mimacho wakati ni beer moja tuu, we vipi mbona uko karne ya nyuma saana. If you think Education is Expensive, try Ignorance.

Ni kweli ELIMU NI BURE,,Ila Serikali haitoi pesa ya chakula kwa shule za kutwa,, Jambo la busara ni Hao walimu kukutana na wazazi,,ama bodi ya shule na waweke KIWANGO Resonable ili kusiwe na wasi wasi wa upigaji,,

Serikali siku zote hasa kipindi hiki cha uchaguzi utaegemea kwa wananchi,,ila mwisho WA siku wanaoumia ni watoto wetu,,,hao mawaziri watoto zao wanasona Private za maana na wanalipa zaidi ya 2Million kwa mwaka ,,,,TUSIRUHUSU KUIBIWA YANAZUNGUMZIKA,,,
 
Tatizo hata vikao/mikutano ikiitwa huwa huendi-Waamini walimu/walezi wenzio, wanahuruma Sana na watoto na wanamalengo ya kishule-Wizara wanayafikia

Tambua waraka huo wa Elimu- bure unfanya kazi nchi nzima lakini mazingira tofauti,

Msiwakatishe tamaa walimu wetu, waache wafanye kazi Yao ya kizalendo
 
Tatizo sio kuchangia pesa au chakula kwa mtoto Ila tatizo hivyo vitolewavyo je vitatumika kwa mujibu wa maelezo na dhumuni ya watoaji!!!? Kumbuka vile vile ni muhimu kupata maelezo Kama ni maelekezo ya wizara ya elimu ukizingatia kauli mbiu ni elimu bure kwa kila mtoto wa mkulima wa nchi hii...

Sent from my itel S32 using JamiiForums mobile app
Mjomba kilo kumi tu za mchele unakuja jf kupiga makelele, na uskute hata kikao cha wazazi hukuhudhuria,
 
Mkuu jiongeze baas, buku 2 tu zinakutoa mimacho wakati ni beer moja tuu, we vipi mbona uko karne ya nyuma saana. If you think Education is Expensive, try Ignorance.
Usipende kuchangia mkuu huku ushatupia vitu vyako kichwani inaonyesha ni mjinga kiasi gani...."buku mbili tu" manaake Nini Kama ingekuwa si pesa wasingeihitaji ualimu ni wito na si biashara....tutahoji tu hata Kama ni shilingi Mia...

Sent from my itel S32 using JamiiForums mobile app
 
Jamani naomba niweke wazi

Mwalimu ni Kama mzazi/mlezi wa mwanafunzi. Kwahyo kuagiza mwanafunzi apeleke mchele kilo 10 na 2000 labda ya kulipa mpishi na kununua mafuta ya kupikia mchele siyo utapeli bali ni kutaka watoto some kwa ubora zaidi wakiwa wameshiba.

Pili, Mwanafunzi hawezi kusoma kwa weledi akiwa na njaa. Hivyo hiyo kilo 10 ni Kama chakula kwanili ya mwanao. Ukitaka mwanao afike mbali ktk elimu lazima ugharamike. Siyo unalilia tu. Hata sisi tulio bahatika kusoma mpaka elimu ya juu wazazi wetu waligharamia kila kitu ikiwemo kutupa hela ya chakula

Acha uchawi wa kutuona sisi walimu kama wezi
 
Usipende kuchangia mkuu huku ushatupia vitu vyako kichwani inaonyesha ni mjinga kiasi gani...."buku mbili tu" manaake Nini Kama ingekuwa si pesa wasingeihitaji ualimu ni wito na si biashara....tutahoji tu hata Kama ni shilingi Mia...

Sent from my itel S32 using JamiiForums mobile app

Ualimu ni wito?
Umechelewa Sana ndugu.
Ni najua Walimu wamesomea na sio wameitwa.
So Ualimu ni kazi kama kazi zingine.

But ukiona hiyo shule inachangisha..... Hamishia mwanao kwa shule isiyochangisha
 
Ha ha ha ! Naona Covid-19 mnataka mponee kwa wazazi!
Hili tundu tutaliandikia waraka kwa waziri wa elimu km atakaa kimya.

Sikila mwanafunzi aliyefanikiwa alikula shuleni!
Tulishinda njaa shuleni na tulifanikiwa km hivi tulivyo.

Shule za kata hamfundishi zaidi ya kuja na mipango hewa.
Hata watoto wanaofauru nikwa juhudi zao na wazazi wao.

Report na matokeo ya kila mwaka inaonyesha shule zakata wilaya ya hii nisawa na zero.

Darasa la wanafunzi 200 wanafauru Div4 34, Div2 wa3 na Div1 zero.

Mnanjaa mnataka kupiga msosi.
Kila mtu apambane na khari yke.
 
just simple solution,, wewe usilipe mwanao ashinde na njaa,,,makelele na assumption za nini?....Kufaulu na kufeli kwa mwanafunzi kuna factor nyingi zinazochangia,,,ofcorse shule za kata hasa za pembezon ni majanga ,,kuna SABABU nyingi sana issue ya walimu inaweza kua inachangia kwa 20%
 
Usipende kuchangia mkuu huku ushatupia vitu vyako kichwani inaonyesha ni mjinga kiasi gani...."buku mbili tu" manaake Nini Kama ingekuwa si pesa wasingeihitaji ualimu ni wito na si biashara....tutahoji tu hata Kama ni shilingi Mia...

Sent from my itel S32 using JamiiForums mobile app
Ewe mzazi buku mbili na kilo mbili za maharage unapiga mawowe , wakati unazaa hawa walimu hukuwashirikisha lakini wamekubali kukusaidia kutoa ujinga wa mwanao, wazazi wengine buana mnatia kinyaa , WEKA MIMBA WEKA PESA ungelialialia hivi .
 
Kilo 1 huku dar Ni tsh 1700... Kwa hiyo umekosa shilingi 17,000 ununue hizo kilo 10 ili mwanao apate elimu Bora.

Leo si tumeambiwa maisha ya watanzania yamepanda tangu kusimikwa kwa awamu ya 5 nini tena mapovu yanakutoka kwa hela ya Castle light 5.
 
Back
Top Bottom