Shibalanga
Senior Member
- Mar 1, 2011
- 178
- 93
Mhe Waziri wa Elimu, sasa ufike wakati serikali ikashirikiana na sekta binafsi ipeleke wanafunzi wa kidato cha tano waliofaulu katika shule zao, ili kuendana na ongezeko kubwa la wanafunzi hasa katika kipindi hiki ambacho serikali imetoa fursa adhimu ya kusoma bure kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne, ninajua gharama za shule binafsi ziko juu ila kama kutakuwa na maongezi kwa shule zisizojiendesha kibiashara, zitengenezewe vigezo na kupewa ruzuku kwa mambo kadhaa kama miundo mbinu nadhani watakubali kuchukua idadi kadhaa ya wanafunzi.
Kama ningeulizwa nipendekeze shule za kuanzia, ningeanza na shule zote zinazomilikiwa na jeshi ziingizwe kwenye mpango huu, maana zipo kwa ajili ya huduma, jeshi lina shule 10, nazo ni kama ifuatavyo:-
1. Jitegemee- DSM
2. Makongo- DSM
3. Airwing- DSM
4. Kawawa- Iringa
5. Unyanyembe- Tabora
6.Nyuki - Zanzibar
7. Kizuka- Moroggoro
8.Pemba- Zanzibar
9. Luwiko- Songea
10. Navy- Kigamboni DSM
Ninapendekeza serikali ishirikiane na sekta binafsi kwa sababu kuliko serikali kung'ang'ania kubadili shule zake kuanza kuchukua kidato cha tano ambazo kimsingi nyingi ya shule hizo huwa duni sana kimuundo na kimiundombinu unakuta wanafunzi wanaripoti kwenye shule hizo mazingira yanakuwa magumu, wanachokifanya wazazi ni kuwaondoa na kuwapeleka shule binafsi, lakini kama serikali itaangalia shule binafsi ambazo ni kongwe zenye vigezo ambavyo wataviweka, shule hizi zikapewa ruzuku maalumu nadhani zikichukua hata darasa moja lenye wanafunzi 50 ni mchango mkubwa sana.
NAWASILISHA!