Waziri Ndalichako: Serikali iweke vigezo, shule binafsi zianze kuchukua wanafunzi wa kidato cha tano

Shibalanga

Senior Member
Mar 1, 2011
179
225
Mhe Waziri wa Elimu, sasa ufike wakati serikali ikashirikiana na sekta binafsi ipeleke wanafunzi wa kidato cha tano waliofaulu katika shule zao, ili kuendana na ongezeko kubwa la wanafunzi hasa katika kipindi hiki ambacho serikali imetoa fursa adhimu ya kusoma bure kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne, ninajua gharama za shule binafsi ziko juu ila kama kutakuwa na maongezi kwa shule zisizojiendesha kibiashara, zitengenezewe vigezo na kupewa ruzuku kwa mambo kadhaa kama miundo mbinu nadhani watakubali kuchukua idadi kadhaa ya wanafunzi.

Kama ningeulizwa nipendekeze shule za kuanzia, ningeanza na shule zote zinazomilikiwa na jeshi ziingizwe kwenye mpango huu, maana zipo kwa ajili ya huduma, jeshi lina shule 10, nazo ni kama ifuatavyo:-

1. Jitegemee- DSM
2. Makongo- DSM
3. Airwing- DSM
4. Kawawa- Iringa
5. Unyanyembe- Tabora
6.Nyuki - Zanzibar
7. Kizuka- Moroggoro
8.Pemba- Zanzibar
9. Luwiko- Songea
10. Navy- Kigamboni DSM

Ninapendekeza serikali ishirikiane na sekta binafsi kwa sababu kuliko serikali kung'ang'ania kubadili shule zake kuanza kuchukua kidato cha tano ambazo kimsingi nyingi ya shule hizo huwa duni sana kimuundo na kimiundombinu unakuta wanafunzi wanaripoti kwenye shule hizo mazingira yanakuwa magumu, wanachokifanya wazazi ni kuwaondoa na kuwapeleka shule binafsi, lakini kama serikali itaangalia shule binafsi ambazo ni kongwe zenye vigezo ambavyo wataviweka, shule hizi zikapewa ruzuku maalumu nadhani zikichukua hata darasa moja lenye wanafunzi 50 ni mchango mkubwa sana.

NAWASILISHA!
 

mpiga dili mzoefu

Senior Member
Dec 28, 2016
123
250
hapo wanakuambia eti bajeti ya bodi ni kusomesha wanafunz 27 elfu .tatzo lao hawaangalii sensa ila wanakurupuka na kuua uchumi leo hakuna mpango wa ajira ,elimu ya juu,nk tupo watu milion hamsin wanatutreat kama tupo milion tano ccm imetushindwa ikubali kukaa pembeni
 

Shibalanga

Senior Member
Mar 1, 2011
179
225
hapo wanakuambia eti bajeti ya bodi ni kusomesha wanafunz 27 elfu .tatzo lao hawaangalii sensa ila wanakurupuka na kuua uchumi leo hakuna mpango wa ajira ,elimu ya juu,nk tupo watu milion hamsin wanatutreat kama tupo milion tano ccm imetushindwa ikubali kukaa pembeni

Binafsi siamini sana katika kulaumu peke yake ndiyo maana nimekuja na ushauri nini kifanyike ili kuondokana na changamoto hii, kulaumu tu sidhani kama ndiyo njiia pekee ya kuleta mabadiliko.
 

mpiga dili mzoefu

Senior Member
Dec 28, 2016
123
250
Binafsi siamini sana katika kulaumu peke yake ndiyo maana nimekuja na ushauri nini kifanyike ili kuondokana na changamoto hii, kulaumu tu sidhani kama ndiyo njiia pekee ya kuleta mabadiliko.
ndg yangu hii serikali utaishauri nn ikiwa wabunge wetu wakisema spika anawatoa nje wafanyabiashara hawapo tena ..na hakuna mwekezaji amekuja toka jamaa aingie madarakan wote hawapo hajapandisha mshahara mkopo vyuoni hakuna sekta binafs hasa mabenki yanaweza sana kukopesha wanafunzi tatzo sera za nchi zinabadilika kila kukicha so ..nothing else
 

Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
49,420
2,000
Serikali ijenge shule za kutosha.
Shule binafsi ada ni kubwa na wana vigezo vyao vya kupokea wanafunzi.
Huwezi kwenda kujaza vilaza shuleni kwao.
 

Jabman

JF-Expert Member
Jul 27, 2016
1,010
2,000
Mnataka watoto wenu wasome st Mary's kwa kodi zetu?
Unafikiri sheria ikipitishwa mtapeleka watoto Wa mkulima kweli?.
Walipieni ada tu huko Feza msitumie pesa yetu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom