markp
Senior Member
- Sep 26, 2013
- 181
- 299
Prof NDALICHAKO YUPO kwenye wizara ya elimu tangu awamu ya hayati Magufuli kama waziri mpaka sasa lakini naona kama elimu haiendeshwi nae inajiendesha yenyewe.
Kuna shule inaitwa NGUVU MPYA SEKONDARY ipo chanika maeneo ya nguvu kazi, kidato cha kwanza pekee wapo 636 nimekwenda wiki iliyopita kuangalia matokeo yao nikakuta wanafunzi karibu 200 wamepata sifuri kwenye hesabu. Na waliobaki karibu wote wana maksi chini ya 10 matokeo yamebandikwa sidanganyi.
Nilipowauliza walimu mbona wanafunzi wamefeli hivi wakasema shule nzima ina walimu 2 tu wa mathematics. Wakasema hao wawili wanaingia zaidi kwenye madarasa ya mitihani.
Mtaani kuna walimu wenye sifa waliomaliza vyou hivi kwanini msiwachukue hata kwa muda wajitolee kwa pesa ndogo isiyo na makato. AJira hamtoi, kukagua hamkagui. Hamjali idadi au uwiano wa walimu na wanafunzi mnatia aibu sana.
Mh Kikwete alikuwa msikivu kwenye elimu alipoona walimu hakuna kabisa akaweka wa haraka. Kweli wana madhara lakini walisaidia sana. Sasa ninyi walimu wapo kibao mtaani afu mnaleta maudhi kweli. Watoto zaidi ya elfu walimu wa mathe 2 dah
Na mwaka huu wanaongezeka form 1 mia 6 ila walimu wale wale. Hapo form four hawakuwa wengi.
Kuna siku nitaandika uozo wa elimu ya Tanzania kwa kutoa mifano hai.
Prof Ndalichako na serikali mnatengeneza bomu . Ila chanzo ni jiwe maana ajira aliweka mfukoni afu wanafunzi akawaongeza.