USSR
JF-Expert Member
- Jul 15, 2015
- 9,895
- 22,659
Wanabodi! Iko hivi
Wakati wa janga la Corona shule na vyuo vilifungwa, wamiliki wa Shule Binafsi wakaiambia Serikali kuwa hawana pesa kwa kuwa wazazi hawakulipa ada na kuwa hakuna aliyejitayarisha kwa janga lile wakaitaka serikali iwasaidie iwape angalau mikopo. Serikali ikakataa na kusema kuwa wao wana pesa za kuwalipa walimu wao ,walimu wa serIkali wakalipwa kwa takribani miezi minne huku hawa wa shule binafsi wakisugua bila hata mia mitaani.
Wengi wakajiingiza kwenye shughuli za hapa na pale kupata pesa watunze familia zao kumbuka hawana mishahara huku wakisubiria Mungu aiondoe Corona.
Mungu si mwanadamu Corona ikaisha mwishoni wa mwezi wa sita shule zikafunguliwa, hapa wamiliki wa shule wakatutoza ada ya mwaka mzima wakisema kuwa utakuwa mwaka wa masomo kama kawaida hakuna kilichoharibika tukalipa ada ya mwaka kama kawaida tukifahamu walimu wanaokaaa na kufundisha watoto wetu nao watalipwa mishahara yao tangu nyuma walipokaa nyumbani maana wao kama watanzania walikuwa na mikopo na madeni ya hapa na pale
Wewe Waziri wa Elimu ukawaelekeza wakusanye ada kwa sisi wazazi ili mwaka wa masomo uendelee na wafundishe mpaka mwezi wa 12 tarehe 18 ikiwa kufidia siku hizi, hapa ina maana tatu:
1. Walimu wamefundisha hadi muda wa ziada ilikukamilisha mwaka wa masomo huku wakifahamu wazazi wamelipa pesa ya mwaka mzima hivyo watalipwa.
2. Wamiliki wa shule walikusanya pesa za mwaka mzima hivyo wanao uwezo wa kuwalipa walimu kama kawaida kama ulivyo elekeza.
3. Sisi wazazi tumelipishwa pesa za ada tena kwa maumivu ila tulijikaza tukijua walimu wa watoto wetu wamelipwa hivyo hawatafanya kazi kwa kinyogo.
Ukweli ni kuwa wamiliki wa shule walikusanya pesa wakatumbua na kuwaacha walimu walihangaika bila kulipwa pesa zao za msimu wa Corona wakati wakiwa wameshakusanya na kutuhamasisha wazazi tulipe.
Kwa kuwa nyie ndio Mawaziri na pia mmekuwa walimu ipo haja ya kutumia mamlaka mliyonayo kuhakikisha walimu hawa wanalipwa pesa zao zote tena bila masharti.
Huu uhuni ulifanywa na wamiliki wa shule wa kuchukua pesa za wazazi na kuwaacha walimu wakihangaika ukomeshwe haraka.
Nitaweka list ya shule zote zilizo na dhuluma hii kadri nitakavyopata taarifa hapa jukwaani ili kuwapa Maafisa Elimu na kazi wilaya kufuatilia kwa ukaribu.
Update