Waziri Ndalichako na Muhagama hili la dhuluma kwa Walimu wa Shule Binafsi linatia doa utendaji wenu

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
5,194
2,000
Wanabodi! Iko hivi

Wakati wa janga la Corona shule na vyuo vilifungwa, wamiliki wa Shule Binafsi wakaiambia Serikali kuwa hawana pesa kwa kuwa wazazi hawakulipa ada na kuwa hakuna aliyejitayarisha kwa janga lile wakaitaka serikali iwasaidie iwape angalau mikopo. Serikali ikakataa na kusema kuwa wao wana pesa za kuwalipa walimu wao ,walimu wa serIkali wakalipwa kwa takribani miezi minne huku hawa wa shule binafsi wakisugua bila hata mia mitaani.

Wengi wakajiingiza kwenye shughuli za hapa na pale kupata pesa watunze familia zao kumbuka hawana mishahara huku wakisubiria Mungu aiondoe Corona.

Mungu si mwanadamu Corona ikaisha mwishoni wa mwezi wa sita shule zikafunguliwa, hapa wamiliki wa shule wakatutoza ada ya mwaka mzima wakisema kuwa utakuwa mwaka wa masomo kama kawaida hakuna kilichoharibika tukalipa ada ya mwaka kama kawaida tukifahamu walimu wanaokaaa na kufundisha watoto wetu nao watalipwa mishahara yao tangu nyuma walipokaa nyumbani maana wao kama watanzania walikuwa na mikopo na madeni ya hapa na pale

Wewe Waziri wa Elimu ukawaelekeza wakusanye ada kwa sisi wazazi ili mwaka wa masomo uendelee na wafundishe mpaka mwezi wa 12 tarehe 18 ikiwa kufidia siku hizi, hapa ina maana tatu:

1. Walimu wamefundisha hadi muda wa ziada ilikukamilisha mwaka wa masomo huku wakifahamu wazazi wamelipa pesa ya mwaka mzima hivyo watalipwa.

2. Wamiliki wa shule walikusanya pesa za mwaka mzima hivyo wanao uwezo wa kuwalipa walimu kama kawaida kama ulivyo elekeza.

3. Sisi wazazi tumelipishwa pesa za ada tena kwa maumivu ila tulijikaza tukijua walimu wa watoto wetu wamelipwa hivyo hawatafanya kazi kwa kinyogo.

Ukweli ni kuwa wamiliki wa shule walikusanya pesa wakatumbua na kuwaacha walimu walihangaika bila kulipwa pesa zao za msimu wa Corona wakati wakiwa wameshakusanya na kutuhamasisha wazazi tulipe.

Kwa kuwa nyie ndio Mawaziri na pia mmekuwa walimu ipo haja ya kutumia mamlaka mliyonayo kuhakikisha walimu hawa wanalipwa pesa zao zote tena bila masharti.

Huu uhuni ulifanywa na wamiliki wa shule wa kuchukua pesa za wazazi na kuwaacha walimu wakihangaika ukomeshwe haraka.

Nitaweka list ya shule zote zilizo na dhuluma hii kadri nitakavyopata taarifa hapa jukwaani ili kuwapa Maafisa Elimu na kazi wilaya kufuatilia kwa ukaribu.

Update

USSR
 

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
8,927
2,000
Pamoja na lawama zinazosababishwa na ubabe wao hizo shule binafsi wajipange sana. Serikali iko kazini muda wote.
 

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
5,194
2,000
Kweli kabisa sisi wazazi tumefanya sehemu yetu ila wamiliki wa shule wanawaonea walimu mwisho wa siku watoto wetu wanabaki hawana la maana kwani wanafundishwa na walimu wenye kinyongo.

Kwa hili mkuu nakuunga mkono walipaswa kulipwa sawa na mkataba. Kibaya zaidi wanaogopa kudai kwa sababu ukidai tu utalipwa ila kazi itaisha. Serikali ingeliangalia hilo. Japo sijui itaanzia wapi maana hawajaenda kulalamika.
 

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
5,194
2,000
Mama D hapa serikali iingilie kati, hii ni dhumla kubwa, wakati wabunge wanamshambulia waziri Ndalichako kuwa serikali ibebe huu mzigo sasa imewarudia wao .wawajibike walipe walimu
Pamoja na lawama zinazosababishwa na ubabe wao hizo shule binafsi wajipange sana. Serikali iko kazini muda wote
 

sweettablet

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
6,339
2,000
USSR unaleta siasa kwenye hoja ya msingi. Huyo mwalimu ameshindwa kujisimamia yeye mwenyewe na kudai haki zake halafu unataka mawaziri waingilie kati? Upumbavu gani huo?

Kama hao walimu wanahisi wameonewa, walianzishe ndio Mawaziri walimalizie. Sasa wao walimu wako maana yake wamekubaliana na hali ilivyo, sasa Mawaziri wanaanzia wapi?
 

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
5,194
2,000
USSR unaleta siasa kwenye hoja ya msingi. Huyo mwalimu ameshindwa kujisimamia yeye mwenyewe na kudai haki zake halafu unataka mawaziri waingilie kati? Upumbavu gani huo? Kama hao walimu wanahisi wameonewa, walianzishe ndio Mawaziri walimalizie. Sasa wao walimu wako maana yake wamekubaliana na hali ilivyo, sasa Mawaziri wanaanzia wapi?
Kazi ya Media ni nini?
 

GanaJr

Member
May 26, 2020
37
95
Mimi ni mmoja wa walimu tuliodhulumiwa hela za malipo ya hiyo miezi wakati wa Corona. Tunaomba Serikali itusaidie maana hatuna serikali nyingine zaidi ya hii serikali ya Mh. Dkt John Pombe Magufuli. Tunaomba Mamlaka husika zitusaidie tupate haki yetu.
 

tamuuuuu

JF-Expert Member
Mar 10, 2014
14,508
2,000
Na walimu siku hizi wanachokifanya kwa watoto Mungu anajua.Ni full kuwatelekeza na hawawajali.Sababu ni maslahi yao. Wa serikalini na binafsi wote they don't care aisee.
 

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
5,194
2,000
Mimi ni mmoja wa walimu tuliodhulumiwa hela za malipo ya hiyo miezi wakati wa Corona.. Tunaomba serikali itusaidie maana na hatuna serikali nyingine zaidi ya hii serikali ya Mh. Dkt John Pombe Magufuli. Tunaomba Mamlaka husika zitusaidie tupate haki yetu.
Pole sana mabosi wenu wanakula kuku kwa pesa hii
 

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
8,927
2,000
mama D hapa serkali iingilie kati hii ni dhumla kubwa ,wakati wabunge wanamshambulia waziri ndalichako kuwa serkali ibebe huu mzigo sasa imewarudia wao .wawajibike walipe walimu

Sijui kwanini hawa wenye shule binafsi waliamua kujitwalia maamuzi yasiyo yao. Hawajawadhulumu walimu tuu ila wamevunja mikataba ya kazi na wameihujumu serikali kwa kutolipa gharama zingine zihusianazo na mishahara pia. Sasa wasubiri kufikiwa na meno ya serikali tu walipe hao walimu pamoja na penalties.

Utawasikia wanarudi hapa wakilialia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom