Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,445
- 3,403
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amebaini mapungufu katika ujenzi wa chuo cha ufundi stadi (Veta) mkoa wa Rukwa na kuagiza kuondolewa katika nafasi yake mkurugenzi wa Veta Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Justine Rutta kutokana kwa madai ya kushindwa kusimamia ipasavyo ujenzi huo.
Pia amemwaagiza katibu mkuu wa wizara hiyo kuunda kamati ya kuchunguza mapungufu yaliyojitokeza katika mchakato mzima wa ujenzi wa chuo hicho, ikiwamo kuangalia kama thamani ya kazi liyofanyika inalingana na fedha ambazo Serikali imetoa hadi sasa.
Waziri huyo amechukua hatua hiyo kutokana na licha mkandarasi kulipwa zaidi ya Sh 2.1 bilioni na Serikali hadi sasa, lakini ujenzi wa mradi huo utakaonufaisha zaidi ya vijana 2,000 kusuasua.
Profesa Ndalichako alitoa maagizo ya kuondolewa mkurugenzi huyo baada ya kukagua ujenzi wa chuo hicho akiwa katika ziara yake ya kikazi mjini Sumbawanga mkoa wa Rukwa.
Katika ukaguzi huo, alibaini kuna ukiukwaji mkubwa wa mkataba baina ya Serikali na mkandarasi wa ujenzi wa chuo hicho kampuni moja ya China, ambapo licha ya Serikali kulipa fedha zaidi ya asilimia 25 kazi ipo kwa kiwango cha aslimia 25 wakati ilitakiwa kuwa imefikia asilimia 61.
Pia waziri huyo alibaini kampuni hiyo kutokuwa na vitendea kazi vya kutosha na muhimu na kutumia kampuni nyingine kuajiri wafanyakazi kinyume cha mkataba.
Awali, Rutta alieleza kuwa: “Mkandarasi huyo amekuwa na changamoto ya ukosefu wa fedha kutokana na Serikali kuchelewa kumlipa hali iliyosababisha ujenzi kusimama kwa zaidi ya miezi miwili.”
Alisema mradi huo ulianza kutekelezwa Septemba mwaka jana na unatarajiwa kukamilika Septemba mwaka huu na una thamani ya Sh 10.6 bilioni.