Waziri Ndalichako aagiza mhandisi, mshauri elekezi ujenzi wa VETA kukamatwa

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,813
4,546
1578306533774.png

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania, Profesa Joyce Ndalichako ameagiza kukamatwa mhandisi wa mradi wa ujenzi wa chuo cha Veta mjini Sumbawanga mkoani Rukwa, Dingi Fubing na mshauri elekezi, Swalehe Kyabega kwa kutosimamia kikamilifu ujenzi huo.

Sumbawanga. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania, Profesa Joyce Ndalichako ameagiza kukamatwa na kuwekwa ndani mhandisi na mshauri elekezi wa mradi ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (Veta) mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.

Mhandisi huyo ni Dingi Fubing raia wa China na mshauri elekezi, Swalehe Kyabega ambaye ni Mtanzania.

Wataalamu hao wa ujenzi wanadaiwa kushindwa kusimamia kikamilifu ujenzi wa chuo hicho huku wakitoa taarifa zisizo sahihi kwa Profesa Ndalichako ambaye leo Jumatatu Januari 6, 2020 amekagua maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho unasuasua.

Ujenzi wa chuo hicho ulioanza Julai 31, 2018 ulitakiwa kukamilika Septemba 2019. Baada ya muda huo kufika mkandarasi aliongezewa siku 100 ambazo nazo ziliishia pasina kumaliza kazi hiyo.

Baada ya kutoa maagizo hayo, polisi waliokuwapo eneo hilo waliwakamata na kuwabeba kwenye gari lao na kuondoka nao kwenda mahabusu ya kituo kikuu cha kati Sumbawanga mjini.

Profesa Ndalichako amewataka polisi kutowaachia watuhumiwa hao lakini amewaruhusu kuendelea kufanya mawasiliano na wenzao ili kukamilisha ujenzi huo ambao hata hivyo waziri huyo hakutoa muda rasmi.

Profesa Ndalichako ameendelea na ziara wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa nchini Tanzania.

Chanzo: Mwananchi
 
Ndivyo mikataba yao inavyosema kwamba wakishindwa kumaliza kwa muda wawekwe ndani au ni upumbavu tu unaoendelea?
 
Naishauri serikali kuwa ili kuleta ufanisi, miradi yote ya ujenzi serikalini na taasisi mbalimbali ibaki chini ya usimamizi wa wizara husika kwani ndio yenye wataalamu. Wizara za kisekta zijikite kwenye kusimamia yale mambo yanayotakiwa kutekelezwa na wizara zao mfano Waziri wa Elimu apambane kutatua tatizo la wa kukosa mikopo wanafunzi kwa kufuatilia wizara husika na haya ya ujenzi wizara ya ujenzi itoe wataalamu wa kumsaidia kusimamia.
 
Point ya kufungulia mwaka.
 
Back
Top Bottom