Waziri Nchimbi na IGP Mwema, Mnasubiri Nini Kujiuzulu?

Orodha ya wanaotakiwa kujiuzulu:1. Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Nchimbi; 2. IGP, Saidi Mwema, mnasubiri nini kujiuzulu ili kusetiri aibu ya serikali?!.3. RPC;4. RCO;5. DCO;6. DC;7. RC
 
Mkuu Tenende, hiki ndicho kilichotokea kwenye ile kesi ya mauaji Mwanza, baada ya waziri na IGP kujiuzulu, RPC, RSO, DPO na DSO walipandishwa kizimbani!. RC na DC walistaafishwa!.
 
Shirika Huru la Habari (Tanpress) limemtaka Rais Jakaya Kikwete amfukuze kazi Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Said Mwema na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi.

Limesema viongozi hao wanatakiwa kuwajibishwa kutokana na mauaji ya mwaandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi yaliyotokea mkoani Iringa.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi wa Tanpress, Mobini Sarya, imeeleza kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda anatakiwa kuwajibika kutokana na amri yake aliyoitoa wakati wa vurugu kati ya polisi na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleoi (Chadema).

Shirika hilo limeitaka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo itoe ufafanuzi kwa kushindwa kutoa tamko na msaada kufuatia kifo cha mwandishi huyo licha ya kwamba polisi wanatuhumiwa kuhusika na mauaji hayo.

“Kuna mauaji ya watu watano yaliyotokea Tarime ambayo yalifanywa na polisi walitoa ubani kwa familia zao.”

Shirika hilo limeziomba nchi wafadhili zinazotoa misaada kuhusu ukuaji wa demokrasia na utawala bora ziangalie kama ina umuhimu kwa sasa kutokana na nchi wanayoifadhili kutoheshimu utawala bora.

CHANZO: NIPASHE

Mchakamchaka kuelekea maisha bora kwa kila mtanzania na haki ya kuishi kuthaminiwa
 
Wanabodi,

Wale wenye kumbukumbu ya Kesi ya Mauaji Mwanza, kilichomtokea Daudi Mwangosi mikononi mwa polisi sote tumekiona, sasa nauliza hivi, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Nchimbi na IGP, Saidi Mwema, mnasubiri nini kujiuzulu ili kusetiri aibu ya serikali?!.

Kama ni kweli polisi mfyatuaji risasi atapandishwa kizimbani, then RPC wake nae ndie amtangulie, huku waziri Nchimbi na IGP Mwema, wao bado wanasubiri nini kuwajibika?.

Hata hivyo, damu ya mtu, haiwezi kupotea bure!, sio damu tuu ya Mwangosi, bali damu za wote zilizo mwagika bila hatia, kwa mujibu wa sheria kubwa kabisa iitwayo The Law of Karma, damu zote hizo lazima zitafidiwa kwa damu au kwa adhabu kubwa zaidi ya damu!. Tatizo la fidia, inaweza kuwa kubwa kuliko tukio lenyewe au hata kuwakumba na wasio husika ili kuisafisha roho ya marehemu!.

Hivyo hata wahusika wasipowajibishwa, then at the end of the day, ni muwajibishaji wa mwisho ndio atakaye lipia the final price!.

Pasco!.
Wana bodi, inawezekana tukio la mauaji ya Kamanda polisi huko mwanza, ni just a "part payment" ya mabaya mengi yanayofanywa na polisi, sio lazima liwe ni payback time ya Mwangosi, not necesarily, bali kwa kila tukio linalotokea chini ya mbingu, ni "pre meditated event".

Kama mwenye jukumu la kuwawajibisha askari hao ni kamanda wao, Saidi Mwema, then kwa mujibu wa sheria hii, his paybavck time yake naye pia ipo, kama Nchimbi anapaswa kuwajibisha Saidi Mwema lakini hamwajibishi, also his payback time yake ipo, and so does the top man!. Its onlt a matter of time!.

RIP Kamanda Polisi!.
 
Wanabodi,

Wale wenye kumbukumbu ya Kesi ya Mauaji Mwanza, kilichomtokea Daudi Mwangosi mikononi mwa polisi sote tumekiona, sasa nauliza hivi, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Nchimbi na IGP, Saidi Mwema, mnasubiri nini kujiuzulu ili kusetiri aibu ya serikali?!.

Kwa mnaokumbuka hiyo kesi, naomba niwakumbushe kwa mujibu wa kumbukumbu yangu, nilikuwa darasa la 4 hivyo baadhi ya facts zinaweza zisiwe right!.

Kwa kawaida askari wale mlio washuhudia wamemzingira Mwangosi, wao walikuwa wanatimiza wajibu wao kwa mujibu wa amri amri halali ya mkubwa wao!. Baada ya kutokea kilucho tokea, huyo mkubwa wao aliyetoa amri, anasubiriwa nini ili hali by now alitakiwa awekwe chini ya ulinzi then and there!, na wakuu wao Nchimbi na Mwema walipaswa by now wawe wameshawasilisha barua zao za kujiuzulu!.

Askari polisi hawezi kushitakiwa kwa kutekeleza amri halali ya mkuu wake, anayetakiwa kushitakiwa kwanza ni aliyetoa amri!.

Kwenye ile kesi ya mauaji Mwanza, iliyotokea mwaka 1976 na kesi kuendeshwa mwaka 1979 baada ya kutokea vifo vya watuhumiwa wawili wa mauaji ya vikongwe, Bw. Masanja Mazengenuka na Isaack Mwana Mkoboko, Waziri wa mambo ya Ndani wakati huo Ali Hasan Mwinyi alijiuzulu, mkuu wa Polisi, Pundugu alistaafishwa kwa manufaa ya umma. Mkuu wa Usalama wa Taifa, Mzena alistaafishwa kwa manufaa ya umma. Walioshitakiwa ni RPC wa Mwanza, Cassian Mkwawa, RS wa Mwanza, Andrew M na DSO, Jemes Ihuya!.

Wakati huo, Peter Kisumo ndiye alikuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza, naye pia aliwajibika!.

Wakuu hao watatu wa polisi walikuwa wakiishi nyumba tatu zilizofuatana zikiwa Isamilo ya chini ikianza ya Ihuya, ikafuatia ya Andew M na ya mwisho ni ya Mkwawa!. Just imagine hali ilikuwaje mtaani wakati vigogo watatu wanene wa mutaa wote wanashitakiwa kwa kosa la mauaji!.

Kama ni kweli polisi mfyatuaji risasi atapandishwa kizimbani, then RPC wake nae ndie amtangulie, huku waziri Nchimbi na IGP Mwema, wao bado wanasubiri nini kuwajibika?.

Hata hivyo, damu ya mtu, haiwezi kupotea bure!, sio damu tuu ya Mwangosi, bali damu za wote zilizo mwagika bila hatia, kwa mujibu wa sheria kubwa kabisa iitwayo The Law of Karma, damu zote hizo lazima zitafidiwa kwa damu au kwa adhabu kubwa zaidi ya damu!. Tatizo la fidia, inaweza kuwa kubwa kuliko tukio lenyewe au hata kuwakumba na wasio husika ili kuisafisha roho ya marehemu!.

Hivyo hata wahusika wasipowajibishwa, then at the end of the day, ni muwajibishaji wa mwisho ndio atakaye lipia the final price!.

Pasco!.

Up Date.
Pay back time imeshaanza.
Haya niliyasema zaidi ya Mwaka mmoja uliopita, kilichomtokea Nchimbi ni hicho kwenye bold ya blue "karma" at work. Sijui Saidi Mwema Asasubiri Nini?!.
Pasco
 
Kukataa kujiuzulu kunahusishwa na uhusika na jeuri hasa katika kupanga. asiyehusika kwa namna yoyote ni rahisi kujiuzulu. rais awafunde wateule wake awape condition kujiuzulu pale makosa makubwa yanapotokea katika wizara zao. viapo vyao viwe na maneno ya kuchukua responsibility
 
Huyu bwana mwema ndiyo huwa ananisikitisha sana huwezo wake mdogo lakini yupo umri umemtupa mkono yupo tu nadhani ndiye igp mbovu kuliko wote waliyopata kutokea toka kuumbwa kwa dunia nahisi elimu yake ni ya mashaka japo anaweza kuwa ameenda shule better quit now sijui nyumbani kwake anaonekanaje kwa watoto wake hajawahi kufanya hata jambo la kukumbukwa
 
Wanabodi,

Wale wenye kumbukumbu ya Kesi ya Mauaji Mwanza, kilichomtokea Daudi Mwangosi mikononi mwa polisi sote tumekiona, sasa nauliza hivi, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Nchimbi na IGP, Saidi Mwema, mnasubiri nini kujiuzulu ili kusetiri aibu ya serikali?!.

Kwa mnaokumbuka hiyo kesi, naomba niwakumbushe kwa mujibu wa kumbukumbu yangu, nilikuwa darasa la 4 hivyo baadhi ya facts zinaweza zisiwe right!.

Kwa kawaida askari wale mlio washuhudia wamemzingira Mwangosi, wao walikuwa wanatimiza wajibu wao kwa mujibu wa amri amri halali ya mkubwa wao!. Baada ya kutokea kilucho tokea, huyo mkubwa wao aliyetoa amri, anasubiriwa nini ili hali by now alitakiwa awekwe chini ya ulinzi then and there!, na wakuu wao Nchimbi na Mwema walipaswa by now wawe wameshawasilisha barua zao za kujiuzulu!.

Askari polisi hawezi kushitakiwa kwa kutekeleza amri halali ya mkuu wake, anayetakiwa kushitakiwa kwanza ni aliyetoa amri!.

Kwenye ile kesi ya mauaji Mwanza, iliyotokea mwaka 1976 na kesi kuendeshwa mwaka 1979 baada ya kutokea vifo vya watuhumiwa wawili wa mauaji ya vikongwe, Bw. Masanja Mazengenuka na Isaack Mwana Mkoboko, Waziri wa mambo ya Ndani wakati huo Ali Hasan Mwinyi alijiuzulu, mkuu wa Polisi, Pundugu alistaafishwa kwa manufaa ya umma. Mkuu wa Usalama wa Taifa, Mzena alistaafishwa kwa manufaa ya umma. Walioshitakiwa ni RPC wa Mwanza, Cassian Mkwawa, RS wa Mwanza, Andrew M na DSO, Jemes Ihuya!.

Wakati huo, Peter Kisumo ndiye alikuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza, naye pia aliwajibika!.

Wakuu hao watatu wa polisi walikuwa wakiishi nyumba tatu zilizofuatana zikiwa Isamilo ya chini ikianza ya Ihuya, ikafuatia ya Andew M na ya mwisho ni ya Mkwawa!. Just imagine hali ilikuwaje mtaani wakati vigogo watatu wanene wa mutaa wote wanashitakiwa kwa kosa la mauaji!.

Kama ni kweli polisi mfyatuaji risasi atapandishwa kizimbani, then RPC wake nae ndie amtangulie, huku waziri Nchimbi na IGP Mwema, wao bado wanasubiri nini kuwajibika?.

Hata hivyo, damu ya mtu, haiwezi kupotea bure!, sio damu tuu ya Mwangosi, bali damu za wote zilizo mwagika bila hatia, kwa mujibu wa sheria kubwa kabisa iitwayo The Law of Karma, damu zote hizo lazima zitafidiwa kwa damu au kwa adhabu kubwa zaidi ya damu!. Tatizo la fidia, inaweza kuwa kubwa kuliko tukio lenyewe au hata kuwakumba na wasio husika ili kuisafisha roho ya marehemu!.

Hivyo hata wahusika wasipowajibishwa, then at the end of the day, ni muwajibishaji wa mwisho ndio atakaye lipia the final price!.

Pasco!.

Up Date.
Pay back time imeshaanza.
@dudus
 
Back
Top Bottom