Waziri Nchimbi na IGP Mwema, Mnasubiri Nini Kujiuzulu?

Nchimbi anatusikitikia tutapata wapi waziri kama yeye akijiuzulu!
Kwani anafanya kazi gani tangu amekuwa Waziri wa mambo ya Ndani? Au amefanya kipi tangu apewe nyadhifa hizo kwenye wizara alizopita??

This is political figure my friend Mawaziri tulionao hadi sasa labda ni wawili wakizidi ni watano; Prof. wa Nishati na madini ndiye Waziri wa kwanza akifuatiwa kidogo na Mwakyembe. Niambie wewe unaowajua wana uwajibikaji

Watu wamewekwa wale ndugu hawajui dhana ya uwajibikaji, we hukumwona kagasheki anaambiwa ukweli na Mhe. Msigwa akakasirika utafikiri kuwajibika ni Dhambi. Tuung'oe huu utawala even before time, tunasubiri nini!!! Mbona waislamu wameweza kuwatoa wenzao jana jamani?? PEOPLES' POWER IS REQUIRED HERE.
 
Ndugu Pasco, Nchi hii ni Ufalme wa Kambale. Baba ndevu,mama ndevu, na watoto ndevu. Ni hivi,Katika familia,Baba kama kiongozi anapokosa "Moral Authority" basi anakosa say and respect kwa anaowaongoza. Hivi unadhani Rais Kikwete angekuwa strong enough with Moral Calibre tungeshuhudia MAZINGAOMBWE haya ya kina Mwema na Nchimbi? Ilikula kwetu,na itatutafuna hadi huyu jamaa na CCM yake watakapopigwa bench. Right now tunapiga kelele tuu.
Hapa Mkuu ukwelikitugani umemaliza yote kwa kumtaja mhusika mkuu. Nilitaka kumwandikia barua ya wazi lakini natumia nafasi hii kupunguza gadhabu zangu.

Binafsi siwalaumu Nchimbi, Mwema, RPC na msululu wote unaofuatia wakati wote hawa ni zao la uteuzi, utendaji na uwajibikaji wa Mheshimiwa Raisi (najisikia vibaya kumwita Mheshimiwa mtu ambaye tayari haheshimiwi sio tu na umma mkubwa wa Watanzania bali hata na wale wale aliowateua, lakini kwa kuwa ni raisi wangu nitamwita Mheshimiwa).

Kama Mhe. Raisi Kikwete angekuwa mtu makini tusingeona madudu yote haya yanayoendelezwa na wateule wake - wanafanya watakavyo, wanasema watakavyo, wanakiuka viapo walivyoapa mbele yake vya kuitetea na kulinda katiba - na Mhe. Raisi anawachekea tu, akiona kero zimezidi (umeme, walimu, madaktari, mimba za wasichana, mawaziri...) huyooooooo! :plane:,
akirejea anakuja na kauli za kejeli kwa wananchi waliomchagua.

Hii ni yako wewe Mheshimiwa Raisi Kikwete: Wateule wako hawakuheshimu na wewe unajua lakini hujali. Wabunge wakiishauri serikali hujali, unasema Ni upepo tu, utapita! Na kweli mengi yamepita, nisingependa kurejea orodha hapa, lakini hili la kuuwawa kwa Watanzania...HAPANA Mhe. Raisi Kikwete ....hili halitapita, damu isiyo na hatia haipiti. Kumbuka, anayeua kwa bomu hufa kwa bomu. Ni msemo tu, wananchi hatuna upanga, seuze mabomu, lakini tuna Mungu, na u/msijidanganye kuwa siku hizi Mungu haadhibu live kama enzi za Manabii. Ule msemo wa Malipo ni duniani, akhera hwenda hesabu bado Mungu unaufanyiakazi

Hawa wanaopigwa risasi na mabomu na wateule wako wana haki yao ya kuishi kiMungu na kikatiba, katiba ambayo wewe na wateule wako mliapa kuilinda. Machozi na vilio vya familia zao, mashaka yanayowasubiri vizuka na watoto wao yatauandama utawala wako milele. . . Zinduka Mheshimiwa Raisi Kikwete, kama unataka raia wako wakuite Mheshimiwa toka nyoyoni mwao na sio kwa woga na kujipendekeza kwako! Iko siku utaondoka sio tu katika utawala bali hata duniani unataka wananchi wakukumbuke kwa lipi? Bado wakati unao wa kuwajibika zaidi wewe mwenyewe kwa kuanza na kuwawajibisha wauwaji hawa!
 
Wanabodi,

Wale wenye kumbukumbu ya Kesi ya Mauaji Mwanza, kilichomtokea Daudi Mwangosi mikononi mwa polisi sote tumekiona, sasa nauliza hivi, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Nchimbi na IGP, Saidi Mwema, mnasubiri nini kujiuzulu ili kusetiri aibu ya serikali?!.

Kwa mnaokumbuka hiyo kesi, naomba niwakumbushe kwa mujibu wa kumbukumbu yangu, nilikuwa darasa la 4 hivyo baadhi ya facts zinaweza zisiwe right!.

Kwa kawaida askari wale mlio washuhudia wamemzingira Mwangosi, wao walikuwa wanatimiza wajibu wao kwa mujibu wa amri amri halali ya mkubwa wao!. Baada ya kutokea kilucho tokea, huyo mkubwa wao aliyetoa amri, anasubiriwa nini ili hali by now alitakiwa awekwe chini ya ulinzi then and there!, na wakuu wao Nchimbi na Mwema walipaswa by now wawe wameshawasilisha barua zao za kujiuzulu!.

Askari polisi hawezi kushitakiwa kwa kutekeleza amri halali ya mkuu wake, anayetakiwa kushitakiwa kwanza ni aliyetoa amri!.

Kwenye ile kesi ya mauaji Mwanza, iliyotokea mwaka 1976 na kesi kuendeshwa mwaka 1979 baada ya kutokea vifo vya watuhumiwa wawili wa mauaji ya vikongwe, Bw. Masanja Mazengenuka na Isaack Mwana Mkoboko, Waziri wa mambo ya Ndani wakati huo Ali Hasan Mwinyi alijiuzulu, mkuu wa Polisi, Pundugu alistaafishwa kwa manufaa ya umma. Mkuu wa Usalama wa Taifa, Mzena alistaafishwa kwa manufaa ya umma. Walioshitakiwa ni RPC wa Mwanza, Cassian Mkwawa, RS wa Mwanza, Andrew M na DSO, Jemes Ihuya!.

Wakati huo, Peter Kisumo ndiye alikuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza, naye pia aliwajibika!.

Wakuu hao watatu wa polisi walikuwa wakiishi nyumba tatu zilizofuatana zikiwa Isamilo ya chini ikianza ya Ihuya, ikafuatia ya Andew M na ya mwisho ni ya Mkwawa!. Just imagine hali ilikuwaje mtaani wakati vigogo watatu wanene wa mutaa wote wanashitakiwa kwa kosa la mauaji!.

Kama ni kweli polisi mfyatuaji risasi atapandishwa kizimbani, then RPC wake nae ndie amtangulie, huku waziri Nchimbi na IGP Mwema, bado wanasubiri nini?.

Pasco!.

Ni ukweli usiofichika kwamba Tanzania viongozi hawana hulka ya kujiuzulu na hii ni kwa sababu wapo pale kimaslahi.
 
kutokuwajibika kwa hawa vigogo ni kuongeza chachu ya ule ukombozi wa usoni

Pasco kumbe hauko kama ninavyokufikilia ndugu, Inawezekana hata kwa Lowasa unapoint Ingawaje bado sijaiona!

pasco ni mtu kutoka kabila makini
 
Wakiondoka hatutapata viongozi wazuri kama wao!!!!!!!!!!!!! Du!!! Hahahahahshhhhhha!!!!!!!!????!!? Yaani kaulinyingine bwana? Amekufa baba mwasisi wa taifa hili na bado lina songa. Itakuwa hawa jamaa? Hapa hamna one man show baba nchimbi chapa lapa ujijengee historia yenye mashiko tusije kufukua maiti yako siku tukiwa madarakani tukapime kama ulikuwa na akili au ulikuwa chizi ogopa aibu.
 
kutokuwajibika kwa hawa vigogo ni kuongeza chachu ya ule ukombozi wa usoni

pasco ni mtu kutoka kabila makini
Mkuu Narubongo, with due respect, kauli yako hii haiwezi kuachwa bila kupingwa kwa sababu ni moja ya zile kauli mbaya kabisa sio tuu za kibaguzi, bali huu ndio ule ukabila mbaya kabisa uliopigiwa sana kelele na Baba wa Taifa!.

Unamaanisha Tanzania tuna makabila makini na makabila yasiyo makini!.
Utawashawishi members kuanza kuhoji Pasco ni kabila gani?, kwa vile humu tunajuana kwa majina tuu tunayotumia, going beyond that kuassume pia unalijua na kabila la member fulani na kulitaja, pia hiyo ni name calling na adhabu yake ni ban!.

Pasco.
 
Pasco,
Nashangaa sana kuona hoja hii inakuja leo. Waandishi wa habari walipaswa waione tangu siku ya kwanza. Nakumbuka hapa Jamvini tumesema mapema sana baada ya kifo. Tuliwaasa watu waachane na askari waliofyatua risasi kwasababu hawana majibu. Tulisema jicho letu na kauli zetu ziwalenge Nchimbi, IGP na Rais Kikwete.

Kwanini watu hawa wanapaswa kuwajibika? Hebu tuangalie kwa uchache maana ya kujiuzulu.
1. Kuonyesha kuwa mtu ameguswa au kusikitishwa na tukio chini ya mamlaka yake.
2. Kuwajibika ili haki itendeke ikiwa ni pamoja na kuachia uchunguzi huru ili kupataukweli.
3. Kumsafisha mtu anayewajibika kwa dhamana na anayeteua wakuu wanaosimamia dhamana hiyo.
4. Kulinda heshima ya taasisi, ushirika, chama au Serikali.

Nchimbi na IGP wanaguswa na vipengele 1-4 kwa namna zote na kuwajibika kujiuzulu ni lazima.
Kwa vile hawakubaliani na 1-4 wananchi wanatakiwa wambane Rais ambaye anaguswa na 3-4.
3-4 ndiyo itakayoweza kumsafisha Rais na 1-2.

Wajibu wa wananchi sasa ni kufanya yafuatyo.
1. Kumbebesha dhamana ya kifo Rais kwa mujibu wa kiapo chake na aliyeshindwa kusimamia 2.
2. Kukibebesha lawama za kifo cha Iringa kwa CCM iliyomdhamini Rais aliyeshindwa kuwawajibisha Nchimbi na IGP katika kusimamia 1-4.

Kifo cha Mwangos kinahusishwa na Rais Kikwete aliechukua dhamana ya kulinda mali na Raia wake kwa muijibu wa kiapo cha kazi yake, aliyeshindwa kusimamia haki ili itendeke na aliyeshindwa kuguswa, aliyeshindwa kusimamia wateule wake na wasaidizi wake na msiba wa Raia asiye na hatia.

Nchimbi na IGP hawawezi kufanya uchunguzi wa tukio linalowahusu kikazi. Siamini waandishi wa habari wamekubali kushiriki katika kamati isiyo na mamlaka kisheria kuchunguza askari wanaopokea amri kutoka kwa IGP na Nchimbi(Duru za siasa-matukio)
Haki haitatendeka hadi pale Nchimbi na IGP watakapokaa pembeni vinginevyo mzigo huu ni wa JK 100%, CCM % na serikali ya CCM%
 
Pasco: KwaniMkuu wa Kaya na Mtoto wa Mkulima wamedokeza lolote kuhusu kujiuzulu kwao? Labda wakuu walazimishe. By the way kuna dhamira ya kuwekwa kwa shinikizo kutoka juu ili kuwakumbusha watendaji kuwa cheo ni dhamana?
 
Pasco,
Nashangaa sana kuona hoja hii inakuja leo. Waandishi wa habari walipaswa waioene tangu siku ya kwanza. Nakumbuka hapa Jamvini tumesema mapema sana baada ya kifo. Tuliwaasa watu waachane na askari waliofyatua risasi kwasababu hawana majibu. Tulisema jicho letu na kauli zetu ziwalenge Nchimbi, IGP na Rais Kikwete.

Kwanini watu hawa wanapaswa kuwajibika? Hebu tuangalie kwa uchache maana ya kujiuzulu.
1. Kuonyesha kuwa mtu ameguswa au kusikitishwa na tukio chini ya mamlaka yake.
2. Kuwajibika ili haki itendeke ikiwa ni pamoja na kuachia uchunguzi huru ili kupataukweli.
3. Kumsafisha mtu anayewajibika kwa dhamana na anayeteua wakuu wanaosimamia dhamana hiyo.
4. Kulinda heshima ya taasisi, ushirika, chama au Serikali.

Nchimbi na IGP wanaguswa na vipengele 1-4 kwa namna zote na kuwajibika kujiuzulu ni lazima.
Kwa vile hawakubaliani na 1-4 wananchi wanatakiwa wambane Rais ambaye anaguswa na 3-4.
3-4 ndiyo itakayoweza kumsafisha Rais na 1-2.

Wajibu wa wananchi sasa ni kufanya yafuatyo.
1. Kumbebesha dhamana ya kifo Rais kwa mujibu wa kiapo chake na aliyeshindwa kusimamia 2.
2. Kukibebesha lawama za kifo cha Iringa kwa CCM iliyomdhamini Rais aliyeshindwa kuwawajibisha Nchimbi na IGP katika kusimamia 1-4.

Kifo cha Mwangos kinahusishwa na Rais Kikwete aliechukua dhamana ya kulinda mali na Raia wake kwa muijibu wa kiapo cha kazi yake, aliyeshindwa kusimamia haki ili itendeke na aliyeshindwa kuguswa, aliyeshindwa kusimamia wateule wake na wasaidizi wake na msiba wa Raia asiye na hatia.

Nchimbi na IGP hawawezi kufanya uchunguzi wa tukio linalowahusu kikazi. Siamini waandishi wa habari wamekubali kushiriki katika kamati isiyo na mamlaka kisheria kuchunguza askari wanaopokea amri kutoka kwa IGP na Nchimbi(Duru za siasa-matukio)
Haki haitatendeka hadi pale Nchimbi na IGP watakapokaa pembeni vinginevyo mzigo huu ni wa JK 100%, CCM % na serikali ya CCM%
Mkuu Nguruvi3, nakubaliana na hoja zako zote kwa asilimia 99.9% isipokuwa moja tuu ya kuiingiza CCM!. Kila ninapoitetea CCM humu jamvini, huishia kuonekana mimi ni mwana CCM, mshabiki au mfuasi, kama jinsi ninavyomsupport EL kwenye uteuzi wa kugombea urais 2015.

Siku zote pmbi langu kuu kwa wana jamvi ni kuwa wakweli ndani ya nafsi zetu, tufanye siasa za staha na sio za kujenga chuki!, kuihusisha CCM kama chama na kifo hiki, sio kukitendea haki!, ni kukijengea chuki isivyo halali!.

Kwenye hili naomba tumtenganishe rais Kikwete na nafsi zake zote tatu.

Nafsi ya kwanza ya rais Kikwete mimi naiita Kikwete JK ni mtu, yaani rais Kikwete as an individual person, ni human being wa kawaida kama mimi na wewe, anakula na kwenye kile kijichumba anaripoti!.

Nafsi ya oili ya rais Kikwete ni Urais wake, hii namuita Kikwete Rais Kikwete (presidential institution), hapa sasa rais Kikwete ni rais wetu na sio yule JK!.

Nafsi ya tatu ya rais Kikwete ni Kikwete Mwenyekiti wa CCM.

Nakuomba sana Mkuu Nguruvi3, tumteganishe Kikwete JK, Kikwete Rais Kikwete na Kikwete Mwenyekiti wa CCM!.

Mfano namfahamu Kikwete JK hakuna ubishi kuhusu muonekano wake (HB) na miongoni mwa tabia zake za enzi hizo, alitake advantage ya huo muonekano kwa kila kilichopita mbele yake na kupendezewa, alikipitia!, na si unaujua udhaifu wa ngozi nyeusi na hawa madada zetu mbele ya (HB), aliwapitia sana tuu!. Huwezi kuutumia udhaifu huu wa Kikwete JK na kuupachika kwa Kikwete Rais, itakuwa sio kumtendea haki!.

Vivyo hivyo huwezi kuyachukua makosa ambayo Kikwete Rais Kikwete anayafanya kama Kikwete Rais Kikwete, na kuyatwishwa kwa Kikwete Mwenyekiti wa CCM, na hivyo kuilaumu CCM kama chama kwa makosa ya Mwenyekiti wake aliyoyatenda, sio kama Mwenyekiti wa CCM, bali ameyatenda kama rais wa nchi!.

Damu ya Daudi Mwangosi, na wengine wote, walipoteza maisha yao mikononi mwa polisi bila hatia yoyote, ii mikononi mwa Kikwete Rais Kikwete, na sio Mikononi mwa Kikwete JK, wala Kikwete Mwenyekiti wa CCM!.

Namalizia kwa kukiri wazi kuwa the deviding line betwen Kikwete JK, Kikwete Rais Kikwete na Kikwete Mwenyekiti wa CCM is very thin!. No matter how thin it is, uwezo wa kuipambanua ndio what matters most ndio maana siku zote humu ndani ya JF, sikuzote nalia na ukweli toka ndani ya nafsi zetu!.

Naamini kiubinadamu, kila aliyeona ona picha za kifo cha Daudi Mwagosi, ameguswa!, hata wale wale polisi wauwaji pale pale eneo la tukio, ukiwa makini kutazama macho yao, wameguswa!, hata wana CCM no matter wanaichukia Chadema kiasi gani kwa sababu ina kila dalili ya kuwapokonya kitumbua chao, mauaji yale yamewagusa!.

Vivyo hivyo Kikwete JK, mauji yale yamemgusa, kumsikitisha na kumhuzinisha, Kikwete JK, yeye ni just a human being, hana uwezo wa kufanya chochote zaidi ya kuomboleza kama binadamu mwingine yoyote!. Na kama kuna binadamu yoyote aliyefurahia kifo kile, hata huyo muuaji mwenyewe then s/he is not normal, s/he must be insane, and that being the case ya insanity, tumsamehe, sio kosa lake!.

Tukija kwa Kikwete Rais Kikwete, huyu sasa ndio mtu mwenye everthing to do na mauaji yale kwa vile huyu ndie mkuu wa nchi na amiri jeshi mkuu. Jeshi linafanya kazi kwa amri, chochote kitakachofanyika na askari wowote wa cheo chochote, anayebeba full resiponsibility ni mkuu wake na in this case, mkuu wao kabisa ni Kikwete Rais Kikwete!, kama walio chini yake wametenda visivyo na yeye ameshindwa kuwachukulia hatua zozote kutokana na udhaifu wake, then Damu za hawa Watanzania ziko mikononi mwake yeye Kikwete Rais Kikwete, na sio Kikwete JK na wala sio Kikwete Mwenyekiti wa CCM!.

Pasco!.
 
Mkuu Nguruvi3, nakubaliana na hoja zako zote kwa asilimia 99.9% isipokuwa moja tuu ya kuiingiza CCM!. Kila ninapoitetea CCM humu jamvini, huishia kuonekana mimi ni mwana CCM, mshabiki au mfuasi, kama jinsi ninavyomsupport EL kwenye uteuzi wa kugombea urais 2015.

Siku zote pmbi langu kuu kwa wana jamvi ni kuwa wakweli ndani ya nafsi zetu, tufanye siasa za staha na sio za kujenga chuki!, kuihusisha CCM kama chama na kifo hiki, sio kukitendea haki!, ni kukijengea chuki isivyo halali!.

Kwenye hili naomba tumtenganishe rais Kikwete na nafsi zake zote tatu.

Nakuomba sana Mkuu Nguruvi3, tumteganishe Kikwete JK, Kikwete Rais Kikwete na Kikwete Mwenyekiti wa CCM!.

Namalizia kwa kukiri wazi kuwa the deviding line betwen Kikwete JK, Kikwete Rais Kikwete na Kikwete Mwenyekiti wa CCM is very thin!. No matter how thin it is, uwezo wa kuipambanua ndio what matters most ndio maana siku zote humu ndani ya JF, sikuzote nalia na ukweli toka ndani ya nafsi zetu!.

Vivyo hivyo Kikwete JK, mauji yale yamemgusa, kumsikitisha na kumhuzinisha, Kikwete JK, yeye ni just a human being, hana uwezo wa kufanya chochote zaidi ya kuomboleza kama binadamu mwingine yoyote!. Na kama kuna binadamu yoyote aliyefurahia kifo kile, hata huyo muuaji mwenyewe then s/he is not normal, s/he must be insane, and that being the case ya insanity, tumsamehe, sio kosa lake!.

Tukija kwa Kikwete Rais Kikwete, huyu sasa ndio mtu mwenye everthing to do na mauaji yale kwa vile huyu ndie mkuu wa nchi na amiri jeshi mkuu. Jeshi linafanya kazi kwa amri, chochote kitakachofanyika na askari wowote wa cheo chochote, anayebeba full resiponsibility ni mkuu wake na in this case, mkuu wao kabisa ni Kikwete Rais Kikwete!, kama walio chini yake wametenda visivyo na yeye ameshindwa kuwachukulia hatua zozote kutokana na udhaifu wake, then Damu za hawa Watanzania ziko mikononi mwake yeye Kikwete Rais Kikwete, na sio Kikwete JK na wala sio Kikwete Mwenyekiti wa CCM!.Pasco!.
Mkuu Pasco, kwanza nikutoe wasi wasi kuwa msimamo wako juu ya EL au CCM hauna tatizo. Kinyume chake wewe umejipambanua kwa kusema kile kinachoonekana sahihi kwa upande wako. Huo ni ukomavu sana na anayekuhukumu kwa msiamamo huo ajiulize ni kwanini usiwe na mtazamo wako

Pili, mada yako inashabihiana sana na bandiko langu la jana kule duru za siasa-matukio ambako nimeeleza yale niliyoyaeleza hapo juu kwa mtazamo wa ushiriki wa kila mmoja.

Nimeeleza kuhusu tukio lilivyo, athari zake katika taswira ya nchi kimataifa, CCM, Chadema na Waandishi wa habari. Nimefanya hivyo kwa kusema nilichoamini mimi ni sahihi.
Sikumuonea huruma mtu, chama au wandishi wa habari. Nimewapa vilivyo kila mmoja na ushiriki wake.
Hii inadhihirisha kuwa sipo hapa kwa ushabiki wa vyama au siasa, labda kaangalie bandiko lile nilivyowahukumu CDM zaidi kuliko hata CCM.

Huko duniani:
Rais Bush ambaye ni udhaifu na katili, akiwa kiongozi wa taifa la watu milioni 300 alikatisha likizo yake Texas kuja DC kusaini mswada wa kuamua hatima ya maisha ya mtu aliyekuwa kwenye msehine ya kupumilia baada ya mvutano wa kisheria. Alikuwa tayari kusaini mswada huo uwe sheria kama seneti ingeamua.

Waziri mkuu Tonny Blair wa UK aliwekwa benchi baada ya chama chake cha Labour kubaini kuwa vita ya Iraq haikuwa ya lazima. Hii ilikuwa kulinda heshima ya chama na matokeo ya Blair ni kuadhibiwa kwa chama katika uchaguzi.

Waziri wa uchukuzi wa Poland alilazimika kujiuzulu baada ya basi kutumbukia mtoni na kuua watu 56. Alifanya hivyo masaa machache baada ya tukio ili kuonyesha kuguswa na kumsaidia Rais wake kwa lolote lile ambalo lingetokea baadaye.

Chama cha ANC kilimuondoa madarakani Thabo Mbeki. Iwe kwa sababu za kihalali au kisiasa bado chama kilitumia nguvu yake kumwajibisha kwasababu ndicho kimeshika hatamu.

Julius Malema aliondolewa ANC baada ya kubainika kuwa kauli zake zinakichafua chama na serikali yake.
Ali Hassan alijuzulu ili kukinusuru chama na serikali yake iliyoamini haki za binadamu.
Hii ni pamoja na kumsafisha Mwalimu ambaye alikuwa mwiba kwa makaburu.

Kikwete hakutoka msoga na kuwa Rais. Alipitia katika hatua za CCM na baada ya kuridhika kuwa anaweza kukiongoza chama wakampa kugombea urais.
Alipokuwa Rais aliapa kusimamia na kulinda katiba ya nchi ikiwa ni pamoja na watu na mali zao.

Serikali iliyopo madarakani ni ya CCM. Ni serikali hiyo iliyopokea maagizo ya chama kuangalia uwezekano wa kupunguza mfumuko wa bei (inflation). Ni kupitia kamati za CC na NEC hali ya usalama wa nchi hujadiliwa na seikali kupewa maagizo.

Kikwete hawezi kuwa Rais kama si mwanachama wa CCM. Kwa mantiki hiyo chimbuko la Urais wake ni zao la CCM.
Kwa bahati, pia ni mwenyekiti wa CCM inayounda serikali.

Nchimbi na IGP wameteuliwa na Rais wa Tanzania anyetokana na CCM. Kwa bahati nzuri Rais pia ni mwenyekiti wa CCM. Hata akiwa ndani ya CC, NEC au mkutano mkuu bado ni Rais ndiyo maana anafanya shughuli za kuimarisha chama kwa kutumia Rasilimali za taifa. Hatuwezi na ni makosa kumtenganisha Kikwete ambaye ni mwenyekiti wa CCM na Rais wa serikali inayotokana na CCM.

Ukinisoma vizuri nimeshauri, kwanza Nchimbi na IGP wawajibike kwa sababu 1-4 hapo juu.
Ikishindikana basi Rais aliyewateua awawajibishe kwasababu 1-4 hapo juu.

Kama anawaonea haya basi chama kilichompa tiketi na dhama ya kukiwakilisha (CCM) kimchukulie hatua kwa kushindwa kuisimamia katiba ya nchi na kukichafua.

Mauaji haya yamefanywa chini ya uangalizi wa CCM na serikali yake inayoongozwa na JK.
Lau kama si hivyo basi CCM ituonyeshe kujali, uongozi na uwajibikaji kwa kuanzia na yule aliyekabidhiwa Ilani ya uchaguzi, katiba ya CCM na Katiba ya nchi ambaye ni JK.
Ni dhima ya JK kupima uzito huo kama alivyofanya Blair au Mbeki.

Nsikitika sana unaposema JK hana la kufanya. Labda nikiulize kwanza kafanya nini ili tusema hana la kufanya?
Analo la kufanya nalo ni kumweka Pembeni Nchimbi na IGP ili tuone kuguswa kwake na ukatili ulioliabisha taifa, unao watesa familia ya Mwangos na unaotishia kuvuruga amani na utulivu na uliochafua taswira ya nchi anayowakilisha.

Sisi wananchi hatumjui Nchimbi kwasababu hawajibiki kwetu, hatumjui IGP au Luhanda.
Tunamjua Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Tanzania aliyetokana na CCM na mwenye dhamana ya usalama wa nchi.

Kukaa kwake kimya na kumwachia Nape apige propaganda ni kukichafua chama, serikali na nchi na huyu pengine ndiye kwanza abebe lawama za kutojali, kutoguswa na kutowajibika kwa serikali inayotokana na CCM.

Kwa jambo hili zito CCM haiwezi kuepuka lawama hadi pale itakapokuwa na wananchi kwa kumuagiza Rais afanye jambo, kama Rais hataki basi CCM ifanye jambo na kama CCM haitaki ikae kimya na donda hili kwni siku harufu ikianza kutoka wananchi wataamua ima kuweka plasta kama kawaida au kukata mguu. Hapo ni CCM si Mwangos (R.I.P)
 
Naamini kiubinadamu, kila aliyeona ona picha za kifo cha Daudi Mwagosi, ameguswa!,

Vivyo hivyo Kikwete JK, mauji yale yamemgusa, kumsikitisha na kumhuzinisha, Kikwete JK, yeye ni just a human being, hana uwezo wa kufanya chochote zaidi ya kuomboleza kama binadamu mwingine yoyote!.

Tukija kwa Kikwete Rais Kikwete, huyu sasa ndio mtu mwenye everthing to do na mauaji yale kwa vile huyu ndie mkuu wa nchi na amiri jeshi mkuu. Jeshi linafanya kazi kwa amri, chochote kitakachofanyika na askari wowote wa cheo chochote, anayebeba full resiponsibility ni mkuu wake na in this case, mkuu wao kabisa ni Kikwete Rais Kikwete!, kama walio chini yake wametenda visivyo na yeye ameshindwa kuwachukulia hatua zozote kutokana na udhaifu wake, then Damu za hawa Watanzania ziko mikononi mwake yeye Kikwete Rais Kikwete, na sio Kikwete JK na wala sio Kikwete Mwenyekiti wa CCM!.

Pasco!.
Hapa Mkuu nitakuwa sikubaliani nawe kwa 99.99% kwa sababu huwezi kumtenganisha Kikwete JK/Mhe. Kikwete Rais Kikwete na Kikwete Mwenyekiti wa CCM.

Siamini kama Kikwete JK kama binadamu limemgusa kwa hali yoyote hili la kifo cha Mwagosi (R.I.P). Kila Mtanzania liliyemgusa amelitolea kauli, wengi kwa kulaani unyama aliofanyiwa na wateule wa Amiri Jeshi Mkuu. Na wale wachache wenye upofu wa moyo wanawatupia lawama CDM kuwa ni chanzo cha kifo cha Mwagosi (R.I.P) na wala hakuna anayesema wala kuwaza kuwa alijitakia mwenyewe. Katika hili, kauli ya Mhe. Kikwete kama raisi iko wapi?

Linapokuja suala zito kama hili tunasahau na ni haki yetu, kutomuona Kikwete kama binadamu bali Mhe.Kikwete kama Raisi na Kikwete kama Mwenyekiti wa CCM. Mimi nilitarajia siku ile ile lilipotokea hili Mhe. Kikwete kama Raisi angelitolea angalau kauli. Nitamshangaa, na kwa kweli nitamtoa maanani kama atakuja kulitoa kauli (ikiwa atalitolea kauli) katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi. Kwake yeye, hili nalo ni upepo tu, utapita!
 
Mkuu Narubongo, with due respect, kauli yako hii haiwezi kuachwa bila kupingwa kwa sababu ni moja ya zile kauli mbaya kabisa sio tuu za kibaguzi, bali huu ndio ule ukabila mbaya kabisa uliopigiwa sana kelele na Baba wa Taifa!.

Unamaanisha Tanzania tuna makabila makini na makabila yasiyo makini!.
Utawashawishi members kuanza kuhoji Pasco ni kabila gani?, kwa vile humu tunajuana kwa majina tuu tunayotumia, going beyond that kuassume pia unalijua na kabila la member fulani na kulitaja, pia hiyo ni name calling na adhabu yake ni ban!.

Pasco.

nikisoma kitu huwa sisahau... Hapo nimekumbushia post yako ya nyuma.
Tufunge mjadala.
 
Matukio ya hivi karibuni ni dira tosha ya ukosefu wa uadilifu na weledi katika jeshi letu la Polisi.

Chombo hiki si cha kisiasa bali nguzo muhimu sana ya Serikali katika uendeshaji wa serikali yenyewe na udumishaji wa amani na mshikamano wa Taifa zima la Tanzania.
Atika miaka ya karibuni Polisi wamekuwa kama mamluki wasiojua kuwa waajiri wao ni Watanzania walipa kodi.

Matukio ya hivi karibuni huko Arusha,Morogoro na majuzi Iringa ni kielelezo kizuri cha mtu kuona kuwa Jeshi sasa halina viongozi mahiri.
Jeshi si paredi tu na magwanda, bali vile vile kujenga heshima katika jamii inayo watumikia.
Kosa la kutoheshimu maisha ya binadamu, na sasa tunaanza kulaumiwa hata na mataifa ya nje, ni kuidhalilisha nchi.
Kama Jeshi la Polisi linafikiri heshima yake itajengwa kwa kupewa sifa na vyama vya siasa, vilivyopo madarakani au vinginevyo, basi limekosa muelekeo.

Kwa matukio ya hivi karibuni, uongozi wa IGP Mwema kwa kweli unapwaya, tena kuliko wakati wowote ule.

Lililo nifanya niandike hii mada ni jambo la kusikitisha la askari polisi bandarini kuhusika na kuiba mali za nchi jirani ya Zambia.

Polisi wamekuwa wezi, tena wezi wa kutisha.

Hapa ndo nasema, Jeshi hili la Polisi linaelekea kumshinda IGP Mwema, he is not in control.
Hapa DSM kubambikwa kesi wananchi, rushwa za kutolewa upepo ni mambo ya kawaida sasa na wananchi wameanza kulidharau jeshi hili.
Mimi nimefuatilia tukio moja ambapo askari wa cheo cha juu Wazo anahongwa kutoekeleza uhalifu.

Tusipoziba ufa tutajenga ukuta, vijana wadogo (askari) wanaona wakubwa wao wanavyotajirika kwa uhalifu.

Mamluki tunawatengeneza sisi wenyewe, IGP aachie ngazi au afukuzwe kwa kushindwa kazi.
 
Jakaya aliwateua kwa agenda ya muslim empowerment, angalia vyombo vya usalama vyote ikiwemo usalama wa taifa wakuu wa vitengo wote wamepachikwa kwa udini ndo maana utendaji wao ni kuua tu!
 
Nafsi ya kwanza ya rais Kikwete mimi naiita Kikwete JK ni mtu, yaani rais Kikwete as an individual person, ni human being wa kawaida kama mimi na wewe, anakula na kwenye kile kijichumba anaripoti!
Nafsi ya oili ya rais Kikwete ni Urais wake, hii namuita Kikwete Rais Kikwete (presidential institution), hapa sasa rais Kikwete ni rais wetu na sio yule JK!.
Nafsi ya tatu ya rais Kikwete ni Kikwete Mwenyekiti wa CCM.
Nakuomba sana Mkuu Nguruvi3, tumteganishe Kikwete JK, Kikwete Rais Kikwete na Kikwete Mwenyekiti wa CCM!.
Pasco!.
Hapana Pasco, hapa ndipo ninapokushangaa kidogo. Kikwete anahusika kwa nafsi zake zote tatu...kama mwananchi wa Tanzania (Raia), kama Kiongozi Mkuu wa serikali (Raisi) na kama Kiongozi Mkuu wa chama tawala, CCM (Mwenyekiti). Kama hili lingekuwa tukio la kwanza, pengine tungempa pass kwamba labda yaliyotokea yalikuwa kwa bahati mbaya...hapo tungeweza kumsamehe kama binadamu na kama mlinzi mkuu wa katiba aliyoapa kuilinda. Kwa bahati mbaya pamoja na matukio mengi ambayo yametokea sasa kwa kipindi kirefu cha wananchi wasio na hatia kupoteza maisha, wote wanaosimamia mauaji hakuna hata moja kati yao aliyewajibika wala kuwajibishwa. Tafsiri hapa ni moja tu, wanaua kwa baraka zake Kikwete! Mkuu wa Polisi, Saidi Mwema, na Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Nchimbi, kwa nyakati mbali mbali wameonesha kiburi cha ajabu na hata kubeza madai ya wananchi dhidi ya uovu wa vyombo wanavyovisimamia.

Kwa mfano, Kikwete hajawahi kuonesha kukerwa na vitendo vya vyombo dola dhidi ya Watanzania wasio na hatia ikiwa ni pamoja na hata kulaani tu kama mwananchi yeyote yule vile. Pili Kikwete kama Raisi haoni taabu katiba aliyoapa kuilinda inaposiginywa na wateule wake kwa kuwa vinara katika kuanzisha fujo badala ya kuzuia fujo kama wanavyotakiwa. Hivi sasa imebainika kuwa polisi ndio wanaanzisha fujo ili wapate sababu ya kuwaua wananachi badala ya kuwalinda. Je, nani kawapa polisi haki ya kutoa roho ya raia hata kama raia huyo inadaiwa hakutii sheria...jibu ni Raisi Kikwete. Tatu Kikwete kama kiongozi mkuu wa chama tawala inakuwaje chama tawala kinaunga mkono na hata kutetea vitendo vya wananchi kuumizwa na vyombo vinavyotakiwa kuwalinda? Tumeshuhudia mara kadhaa hadi wawakilishi wa wananchi kwa mfano Wabunge wakishambuliwa na kukatwa mapanga kwa sababu tu ni wa kutoka upinzani? Sidhani kuna siku hata moja chama anachokiongoza kimekaa na kutoa taarifa yoyote rasmi ya kulaani vitendo hivi vya kishenzi.

Tafsiri ya ukimya wa Kikwete kama raia, Kikwete kama Raisi na Kikwete kama kiongozi mkuu wa chama tawala ni moja tu...kwa nafsi zake zote anabariki vitendo hivyo. Hivi ni kwa nini tunawashuhudia wasaidizi wake mbali mbali wakikebehi juhudi zozote zile zinazofanywa na watu mbali mbali wakitaka vitendo hivyo vya kikatili vikomeshwe mara moja? Watu wanatekwa lakini kafara anatafutwa kichaa tena raia wa nchi nyingine, watu wanauawa lakini lawama zinatolewa kwa watu wasio na uwezo wala sababu ya kufanya hivyo na wakubwa wanatoa amri ya kuua lakini wadogo ndio wanabambikiziwa kesi ya mauaji. Mtuhumiwa anatamba hawezi kuwajibika na hapo hapo yeye huyo huyo anaunda kamati ya kuchunguza tuhuma dhidi yake...hii yote imewezekana tu katika utawala kama wa Jakaya Mrisho Kikwete. Hapana Pasco hakuna mtu yeyoe wa kunyooshewa vidole bali the President, period.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom