Waziri Nchimbi atoa masaa matatu kwa Meneja Tanesco Tabata na wafanyakazi wote! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Nchimbi atoa masaa matatu kwa Meneja Tanesco Tabata na wafanyakazi wote!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yericko Nyerere, May 31, 2012.

 1. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #1
  May 31, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,210
  Likes Received: 3,774
  Trophy Points: 280
  Katika kukithiri kwa rushwa ndani ya shirika la Umeme Tanesco, meneja wa Tanesco Tabata bwana Richard Swai na wafanyakazi wote wapatao 28 wamesimamishwa jana na leo mda huu ndio maamuzi yanasubiriwa,

  Inatajwa kuwa meneja huyo na watendakazi wake walifika nyumbani kwa mama yake na Emanuel Nchimbi Tabata na kumuwekea umeme kinyume na taratibu za Kitaneso bila waziri huyo kujua kuwa umeme aliofungiwa ni wamagumashi, baada ya mda kupitia kikosi maalumu cha Tanesco (RPU) kilifika nyumbani kwa mama huyo na kuukata umeme ambapo waliuomba wapewe pesa ili waurudishe na waziri Nchimbi alikataa na kutaka kulifuatilia suala hili yeye mwenyewe makao makuu ya Tanesco,

  Kwakuwa Waziri huyo haishi hapo, bali hushi Masaki, wiki iliyopita alikwenda kumjulia hali mama yake na ndipo aliposhangaa kuona umeme unawaka, akawahoji ndugu zake wakasema walijichanga pesa na kuwapa tanesco wakarudishiwa umeme,

  Hapo waziri ndipo alipocharuka na kumuona mojakwamoja Mkurugenzi wa Tanesco ndugu Mhando, kufumba na kufumbua jana Mhando amekisimamisha kazi kituo kizima na leo tangu asubuhi kikako cha dharula na wafanyakazi hao chini ya Katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na madini, Mkurugenzi wa Tanesco na maafisa wote watanesco kimekuwa kikiendelea na ndipo sasa wamepewa mda mpaka saa kumi jioni wawe wametoa maelezo kwanini wasiwajibishwe (wafukuzwe) kwa kosa hilo!

  Hapa wizarani ni hofu tupu imetanda wakisubiri hatima hiyo ya saa kumi leo!

  UDATES:

  Mpaka naondoka eneo la tukio saa 12:30 watuhumiwa wote walikuwa hawajatoa maelezo waliyotakiwa kuyatoa, na walikuwa na kikao na ofisa mwajiri wa tanesco mkoa Ilala,

  Hatima yao tutaijua asubuhi ya kesho!

  UDATES:
  Taarifa zinajuza kuwa wafanyakazi na uongozi wao wote wamerudishwa kazini, inatajwa kuwa hayo yametokea baada ya kutokuwa na ushahidi wa wazi kuwa walipokea rushwa na walimfungia umeme feki,

  Taarifa zinazidi kusema wataalamu wa Manuvazi ndani ya tanesco walifanikiwa jana kuhuisha nyaraka zote feki za kuingizia umeme za mama Nchimbi na kuwa halali kabisa,

  Ndipo mwisho wa siku imeonekana ni majungu tu hakuna cha rushwa wala umeme wa magumashi!

  Hehee hiyo ndio Dar na wadarslam wenyewe!
   
 2. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  nimecheka sana teh,teh,teh......Kumbe wao hupenda kula tu,Wakiliwa wanakua wakali.....teh!teh!teh! Yaani hata mawazir wabadhilifu wangekua wanachukuliwa hatua hivi dah! Simpati picha nchimbi na kile kithembe chake
   
 3. mjomba wa kale

  mjomba wa kale JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 267
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ama kweli tz tuitakayo inaanza na sisi wenyewe, hongera waziri Nchimbi kwa kulivalia njuga suala hilo lakini nashauri waangalie na sehemu nyingine sio tbt pekee shirika halina picha nzuri mitaani mpaka aibu.
   
 4. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #4
  May 31, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,210
  Likes Received: 3,774
  Trophy Points: 280
  Hehee safi sana!
   
 5. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Nchimbi usituyeyushe,yani wewe kidogo tu umekimbilia tanesco,sasa huku daily tunakamuliwa umeme,maji,mgambo,watoto wa wema,serikali za mtaa yani daily mkuki kwa nguruwe eh??
   
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Ndo nchi yetu inavyokwenda kwenda....kimpango mpango, tutafanyaje
   
 7. Kakulwa P

  Kakulwa P JF-Expert Member

  #7
  May 31, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asingekuwa Waziri mambo yangeenda kama kawa, kama vishoka walikuja kwanza kufanya kazi hiyo ilikuwaje kikosi cha TANESCO kikafuata baada ya vishoka kuondoka? Jibu ni kuwa wote wanashirikiana. Fukuzeni hao wote
   
 8. FIDIVIN

  FIDIVIN Senior Member

  #8
  May 31, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sasa wewe ulitaka nini? au ndo fashion siku hizi bora umekandia tu
   
 9. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #9
  May 31, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,319
  Likes Received: 2,605
  Trophy Points: 280
  .....na kuukata umeme ambapo waliuomba wapewe pesa ili waurudishe.... hiki kipande kimeniwia vigumu kukielewa na naona ndio kinabeba taarifa nzima, ufafanuzi plzzz!
   
 10. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #10
  May 31, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Sasa hapo unampongeza Nchimbi au wafanyakazi wa TANESCO waliodai rushwa kwa mamake wa waziri? Huwa naamini kwamba kama matatizo ya rushwa na ujambazi yanayoikabili hii nchi yangekuwa huwa yanawakuta mawaziri na viongozi wengine wa serikali, vitendo hivi vingeshakomeshwa siku nyingi. Lakini kwa kuwa ambaye tunaumia kwa vitendo hivi siku zote ni sisi wa hali ya chini, hawa wakubwa huwa hawajali kabisa. Nawapongeza Tanesco kwa kuweka usawa kwa kudai rushwa hata kwa wakubwa kuliko kutuonea sisi wadogo peke yetu.
   
 11. w

  warea JF-Expert Member

  #11
  May 31, 2012
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuki kwa nguruwe mtamu, kwa binadamu ........!

  Tuone kama kwake kutatengemaa!
  Fujo za Zanzibar!
  Mauaji ya waandamaji!
  Majambazi na wezi wote!
  Vyeti feki polisi!
  n.k
   
 12. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #12
  May 31, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Ila nijuavyo sheria inasema kuwa mtoa rushwa na mpokea rushwa wote wana makosa.So tusubiri kama hao ndugu zake waziri watachukuliwa hatua .Tanzania ina mazingaumbwe sana.
   
 13. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #13
  May 31, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  kwa vile aliyelalamika ni waziri ndo maana wamejifanya kuchukua hatua.
  Angekuwa rais ya kawaida tuu kama sie asingesimamishwa wala kufukuzwa mtu.
   
 14. tete'a'tete

  tete'a'tete JF-Expert Member

  #14
  May 31, 2012
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 474
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna ndugu yangu nimempigia simu yuko tanesco tabata anasema acheni hizo story ni uzushi mbona wako kazini kama kawa...
   
 15. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #15
  May 31, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,210
  Likes Received: 3,774
  Trophy Points: 280
  Hehee hujaelewa nini hapo mkuu? Nimemaanisha kuwa kikosi cha ulinzi wa mali/miundo mbinu ya Tanesco RPU walifika kwa mama wa Nchiumbi wakakata umeme kwa madai kuwa umeme huo si halali, lakini hapohapo hao RPU wakaomba wapewe pesa ili waurudishe tena huo umeme!

  Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
   
 16. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #16
  May 31, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mkuu hapo kwenye red patamu sana,lakini hapo penye nyeusi kitendawili
   
 17. kelvito

  kelvito JF-Expert Member

  #17
  May 31, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu ukitaka tukuamini jitokeze mzimamzima kama mtoa mada hapo juu!
   
 18. F

  FJM JF-Expert Member

  #18
  May 31, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mambo miwili:

  Mosi, wafanyakazi wa TANESCO wameomba hela na ndugu wa Nchimbi wakachanga na kuwapa hao watu wa TANESCO. Hiyo ni rushwa. Hivyo nilitegemea wote aliyoomba na kutoa rushwa wawe Central sasa hivi. Kupitia haya maelezo ni kwamba ndugu wa Nchimbi wamekiri kutoa hela ambapo hapo awali Nchimbi alikataa kwa sababu alijua ni kinyume na utaratibu. Sasa kwa nini washughulikiwe watu wa upande mmoja wa shlilingi na sio washiriki wote?

  Pili, Nchimbi ni waziri wa mambo ya ndani. TANESCO iko chini ya wizara ya Nishati ya Madini. Kwa nini asiwasiliane na wizara husika badala ya ku-deal na TANESCO moja kwa moja?
   
 19. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #19
  May 31, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,202
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  Na kule Zanzibabar walikochoma makanisa alitoa saa ngapi kwa maofisa wa polisi waliozembea kufukuzwa kazi? Yaani waziri maslahi ya familia ni zaidi ya maslahi ya taifa? Hapa sipati picha.
  .
   
 20. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #20
  May 31, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kwa hiyo Nchimbi yanayotokea nyumbani kwao anayasimamia barabara kwa kutumia cheo cha uwaziri, ukienda kwenye desk lake ofisini kumejaa malalamiko kibao ameyaweka pending!
  Ubinafsi unatumaliza!!!!!
   
Loading...