Waziri Nchimbi akimbia na sanduku la kura wakati madiwani wakigombana

Hishimuni maamuzi ya wengi kwani ndio demokrasia hiyo. Ingawa story yenyewe inaonekana imeandikwa kiushabiki, Kama habari hii ni kweli basi CCm, itakuwa imefanya makosa sana na inabidi iadhibiwe.
 
Ikiwa haya tunayoletea hapa jamvini ni kweli, nina kitu kimoja ambacho kinanisumbua sana akilini: Hivi ni nini hasa kinachowafanya CCM washindwe kuelewa kuwa kwa sasa kuna wimbi la mageuzi Duniani ambalo Tanzania kama moja ya nchi za Dunia hii, haiwezi kukwepa hayo? Nini kinawafanya washindwe kuelewa kuwa watanzania wa leo wamebadilika Sana? naomba mnisaidie.
 
MADIWANI saba wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma, wametishia kujiuzulu nafasi zao kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa mambo ndani ya chama chao. Madiwani hao walitoa tishio hilo jana baada ya kumaliza kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya CCM, wakituhumiwa kushirikiana na madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kupiga kura ya ‘Hapana’ kwa mgombea pekee wa kiti cha umeya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ruvuma, Charles Mhagama (CCM).

“Tupo tayari kwa lolote ili wananchi wapime ubabe uliopo ndani ya CCM kwani wao ndio waliotuchagua, hivyo tunapaswa kushirikiana nao katika kulisukuma gurudumu la maendeleo na sio kuwadhurumu rasilimali,” alisema mmoja wa madiwani hao.

Madiwani waliohojiwa ni Cristofa Matembo (Sead Farm), Gerard Ndimbo (Ruhiko), Jenifrida Haule (Viti Maalumu), Kulabesi Mgwasa, (Msamala), Faustine Mhagama (Mshangano) na Wilon Kapinga (Ndilimalitembo).

Jumla ya madiwani waliopiga kura za kumchagua Meya ni 26, Charles Mhagama (CCM) aliyekuwa mgombea pekee aliibuka na kura 14 za ‘Ndiyo’ na 12 za ‘Hapana’ wakiwemo saba wa CHADEMA.

My take: CCM wanao ubavu wa kuwatimua kama ilivyofanya Chadema?
 
MADIWANI saba wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma, wametishia kujiuzulu nafasi zao kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa mambo ndani ya chama chao. Madiwani hao walitoa tishio hilo jana baada ya kumaliza kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya CCM, wakituhumiwa kushirikiana na madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kupiga kura ya ‘Hapana’ kwa mgombea pekee wa kiti cha umeya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ruvuma, Charles Mhagama (CCM). Uchaguzi huo ulivunjika baada ya kuibuka kwa vurugu ukumbini, CHADEMA ilisusia kusimamisha mgombea kwa kile walichoeleza kutoridhishwa na utaratibu waliodai uliweka mazingira ya kuibeba CCM.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili madiwani hao walisema jana waliitwa kwenye kikao cha Kamati ya Maadili na kuhojiwa kwanini wameisaliti CCM na kuungana na wenzao wa CHADEMA, kupiga kura za ‘Hapana’ kwa Mhagama. Katika utetezi wao, madiwani hao walikiri kuwa kweli walimpigia kura za ‘Hapana’ mgombea huyo ili uchaguzi uitishwe upya kwa sababu hana sifa ya kushika wadhifa huo.

“Ndani ya CCM, viongozi walilazimisha na Mhagama alifanikiwa kupenya kwenye mchakato wa ndani, nasi tukasema wamezoea kutuburuza kwa kutulazimisha kupitisha viongozi wanaowataka wao kwa masilahi ya wachache, sasa awamu hii tukaapa kwamba tunawaonyesha nguvu yetu kwa kupiga kura za ‘Hapana’ ili waaibike na tumefanya hivyo,” alisema mmoja wa madiwani hao ambao hawakutaka majina yao yatajwe.
Walisema si dhambi wala kosa kwao kupiga ya ‘Hapana’ kwa mwanachama mwenzao kwenye uchaguzi wowote ule, lakini ingekuwa vibaya kama wangepiga kura ya ‘Ndiyo’ kwa mgombea wa CHADEMA, kama angesimamishwa. “Tupo tayari kwa lolote ili wananchi wapime ubabe uliopo ndani ya CCM kwani wao ndio waliotuchagua, hivyo tunapaswa kushirikiana nao katika kulisukuma gurudumu la maendeleo na sio kuwadhurumu rasilimali,” alisema mmoja wa madiwani hao.

Alipohojiwa na gazeti hili, Katibu wa CCM wa Wilaya ya Songea, Alfonce Siwale, alikiri kuwaita madiwani saba kwenye kikao cha Kamati ya Maadili jana kwa tuhuma za kukisaliti chama. “Kweli tumewaita, tumewahoji kwa mujibu wa kanuni za chama, sasa kama wanatishia kujiuzulu watakuwa wametumia busara zao kwani siku zote mtu mzima, halazimishwi jambo,” alisema Siwale. Aliwataja madiwani waliohojiwa na kata zao kwenye mabano kuwa ni Cristofa Matembo (Sead Farm), Gerard Ndimbo (Ruhiko), Jenifrida Haule (Viti Maalumu), Kulabesi Mgwasa, (Msamala), Faustine Mhagama (Mshangano) na Wilon Kapinga (Ndilimalitembo).

Uchaguzi huo ulivunjika juzi baada ya kuibuka vurugu za kurushiana makonde na matusi ya nguoni miongoni mwa madiwani, wakipinga matokeo ya kura zilizotangazwa ambapo mgombea pekee wa kiti hicho, Mhagama, aliibuka na kura 14 za ‘Ndiyo’ na 12 za ‘Hapana’ Katika vurugu hizo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi, alikimbia na sanduku la kura nje ya ukumbi baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa meya yanayohofiwa kuchakachuliwa.

Jitihada za Waziri Nchimbi ziliishia ukingoni baada madiwani wa CHADEMA kumnyang’anya na kufanikiwa kulirudisha ndani ya ukumbi. Chanzo kikubwa cha vurugu hizo, kinatokana na tuhuma kuwa Naibu Meya wa Halmashauri hiyo, Mariam Dizumba, aliiba kura zilizopigwa na madiwani, hasa baada ya matokeo kuonyesha kuwa Mhagama alipata kura 14 za ndio na 12 za hapana. Jumla ya madiwani waliopiga kura ni 26, wakiwemo saba wa CHADEMA.
 
Hapo ndipo panapowawia vigumu CCM.
Kufanya maamuzi magumu ni jambo ambalo linawashinda sana.
Kama hao madiwani wamesaliti chama then kwa nini wasiwatimue?
 
MADIWANI saba wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma, wametishia kujiuzulu nafasi zao kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa mambo ndani ya chama chao.

Madiwani hao walitoa tishio hilo jana baada ya kumaliza kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya CCM, wakituhumiwa kushirikiana na madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kupiga kura ya ‘Hapana’ kwa mgombea pekee wa kiti cha umeya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ruvuma, Charles Mhagama (CCM).

Uchaguzi huo ulivunjika baada ya kuibuka kwa vurugu ukumbini, CHADEMA ilisusia kusimamisha mgombea kwa kile walichoeleza kutoridhishwa na utaratibu waliodai uliweka mazingira ya kuibeba CCM.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili madiwani hao walisema jana waliitwa kwenye kikao cha Kamati ya Maadili na kuhojiwa kwanini wameisaliti CCM na kuungana na wenzao wa CHADEMA, kupiga kura za ‘Hapana’ kwa Mhagama.

Katika utetezi wao, madiwani hao walikiri kuwa kweli walimpigia kura za ‘Hapana’ mgombea huyo ili uchaguzi uitishwe upya kwa sababu hana sifa ya kushika wadhifa huo.

“Ndani ya CCM, viongozi walilazimisha na Mhagama alifanikiwa kupenya kwenye mchakato wa ndani, nasi tukasema wamezoea kutuburuza kwa kutulazimisha kupitisha viongozi wanaowataka wao kwa masilahi ya wachache, sasa awamu hii tukaapa kwamba tunawaonyesha nguvu yetu kwa kupiga kura za ‘Hapana’ ili waaibike na tumefanya hivyo,” alisema mmoja wa madiwani hao ambao hawakutaka majina yao yatajwe.

Walisema si dhambi wala kosa kwao kupiga ya ‘Hapana’ kwa mwanachama mwenzao kwenye uchaguzi wowote ule, lakini ingekuwa vibaya kama wangepiga kura ya ‘Ndiyo’ kwa mgombea wa CHADEMA, kama angesimamishwa.

“Tupo tayari kwa lolote ili wananchi wapime ubabe uliopo ndani ya CCM kwani wao ndio waliotuchagua, hivyo tunapaswa kushirikiana nao katika kulisukuma gurudumu la maendeleo na sio kuwadhurumu rasilimali,” alisema mmoja wa madiwani hao.

Alipohojiwa na gazeti hili, Katibu wa CCM wa Wilaya ya Songea, Alfonce Siwale, alikiri kuwaita madiwani saba kwenye kikao cha Kamati ya Maadili jana kwa tuhuma za kukisaliti chama.

“Kweli tumewaita, tumewahoji kwa mujibu wa kanuni za chama, sasa kama wanatishia kujiuzulu watakuwa wametumia busara zao kwani siku zote mtu mzima, halazimishwi jambo,” alisema Siwale.

Aliwataja madiwani waliohojiwa na kata zao kwenye mabano kuwa ni Cristofa Matembo (Sead Farm), Gerard Ndimbo (Ruhiko), Jenifrida Haule (Viti Maalumu), Kulabesi Mgwasa, (Msamala), Faustine Mhagama (Mshangano) na Wilon Kapinga (Ndilimalitembo).

Uchaguzi huo ulivunjika juzi baada ya kuibuka vurugu za kurushiana makonde na matusi ya nguoni miongoni mwa madiwani, wakipinga matokeo ya kura zilizotangazwa ambapo mgombea pekee wa kiti hicho, Mhagama, aliibuka na kura 14 za ‘Ndiyo’ na 12 za ‘Hapana’
Katika vurugu hizo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi, alikimbia na sanduku la kura nje ya ukumbi baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa meya yanayohofiwa kuchakachuliwa.

Jitihada za Waziri Nchimbi ziliishia ukingoni baada madiwani wa CHADEMA kumnyang’anya na kufanikiwa kulirudisha ndani ya ukumbi.

Chanzo kikubwa cha vurugu hizo, kinatokana na tuhuma kuwa Naibu Meya wa Halmashauri hiyo, Mariam Dizumba, aliiba kura zilizopigwa na madiwani, hasa baada ya matokeo kuonyesha kuwa Mhagama alipata kura 14 za ndio na 12 za hapana.

Jumla ya madiwani waliopiga kura ni 26, wakiwemo saba wa CHADEMA.
 
tunataka watu wenye msimamo kwa manufaa ya majority,sio kama wale wa geita wamerubuniwa na walafi wa nchi hii wakamtimua mwenyekiti.shit! Hao wa songea hawako sawa na wa arusha,wamemkataa kibaraka wa wezi lakini wa a town walikuwa wanatetea matumbo yao!
 


Katika hali isiyo ya kawaida, Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma, wamerushiana makonde na kusababisha uchaguzi wa meya kuvunjika.

Hatua hiyo ilifikiwa baada ya Naibu meya wa halmashauri hiyo, Mariam Dizumba, kudaiwa kuiba kura zilizopigwa na madiwani hao kwenye uchaguzi wa kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Meya wa halmashauri hiyo, Ally Manya, aliyefariki dunia miezi michache iliyopita Kutokana na mapigano hayo baadhi ya madiwani walijikuta wakijeruhiwa na wengine kupoteza simu na vitu vya thamani. Katika uchaguzi huo, ulioanza kwa malumbano makali yaliyodumu kwa zaidi ya dakika 20 kati ya madiwani wa CHADEMA na wa CCM, ambao walikuwa wanajadili jinsi uchaguzi huo utakavyokuwa huru na haki kutokana na upinzani kutosimamisha mgombea.

Kutokana na hali hiyo, Msimamizi wa uchaguzi ambaye pia ni Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Nachoa Zakaria, alitoa ufafanuzi wa kanuni za uchaguzi wa nafasi hiyo, huku akiwataka kupiga kura za ndiyo au hapana na kwamba, wapiga kura halali waliojiorodhesha ni 26, akiwamo na Mbunge wa Songea Mjini, Dk Emmanuel Nchimbi.

Zoezi la hesabu lilipomalizika, Naibu meya Dizumba alilisimama na kuanza kutangaza matokeo, akitaja mgombea pekee wa CCM, Charles Mhagama, alipigiwa kura za ndiyo 14 na hapana 12. Madiwani wa CCM ni wengi kuliko wa CHADEMA,cha ajabu madiwani hao katika kupiga kura za kuchagua Mstahiki Meya Mheshimiwa Charles Mhagama,ni kwamba waliyo sema ndiyo ni 12 na waliyo sema hapana ni 14 hiyo ina maana hata baadhi ya Madiwani wa CCM walikuwa hawana imani na Mheshimiwa Mhagama kuwa Meya wa Manispaa ya Songea.


Dizumba alisema kutokana na matokeo hayo, Mhagama ndiye meya mpya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea, “Naomba msimamizi wa uchaguzi umwite Diwani Mhagama avae joho la Umeya na kukalia kiti chake,” alisema Dizumba.

Baada ya Msimamizi kumwita Mhagama na kumtaka kuvaa joho la Umeya, baadhi ya madiwani walimtaka msimamizi kuhesabu upya kura hizo ili madiwani wote washuhudie, “Naomba msimamizi usitishe zoezi la kumtaka Diwani Mhagama akalie kiti cha Umeya, kwa sababu kuna mashaka makubwa na zoezi la utangazaji matokeo, hivyo zihesabiwe kura upya na madiwani wote wazione,” alisema Diwani wa Kata ya Mfaranyaki, Seneta Yatembo.

Wakati wakiendelea kuzozana, Diwani wa Viti Maalum (CHADEMA), Rhoda Komba, akawaita madiwani wenzake kushuhudia Dizumba alivyokuwa anaiba kura zilizopigwa za hapana kutoka kwenye sanduku la kura, huku akichukua kura za ndiyo kutoka kwenye mkoba wake kuziweka ndani ya sanduku.

Hali hiyo ilisababisha vurugu kubwa na kumfanya Dk. Nchimbi kukimbia na sanduku la kura kuelekea nje ya ukumbi, kabla ya kunyang’anywa na kutakiwa kulirudisha ndani na madiwani wakiongozwa na CHADEMA.

Baada ya tafrani hiyo, madiwani wa CHADEMA waliitisha kikao na waandishi wa habari na kutoa tamko la kutomtambua Mhagama kuwa meya na kwamba, wameomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuitisha uchaguzi mwingine.

CHADEMA ina madiwani 7 wakati CCM inao 20.
 
Kama kweli Nchimbi ni dokta hakaika kwa hili swala ameaibisaha wanataaluma wote wa TZ!! Ni vyema hata ile nafasi aliyoteuliwa nayo na huyu mwenye Nchi aachie ngazi ili kuitoaibisha wantaaluma wa TZ Kama vile Dk Slaa, Prof Baregu nA Prof Safari!!
 
Kama kweli Nchimbi ni dokta hakaika kwa hili swala ameaibisaha wanataaluma wote wa TZ!! Ni vyema hata ile nafasi aliyoteuliwa nayo na huyu mwenye Nchi aachie ngazi ili kuitoaibisha wantaaluma wa TZ Kama vile Dk Slaa, Prof Baregu nA Prof Safari!!

baada Msemakweli kumuanika ni mmoja wa waliochakachua doctorate zao, karudi Mzumbe anapiga shule, ni kati ya vijana wa ccm wanaotarajiwa kuja kuwania nafasi ya ukuu wa nchi hapo baadae, hizi siasa uchwara anazofanya zitamtia doa kufikia lengo
 
Kama kweli Nchimbi ni dokta hakaika kwa hili swala ameaibisaha wanataaluma wote wa TZ!! Ni vyema hata ile nafasi aliyoteuliwa nayo na huyu mwenye Nchi aachie ngazi ili kuitoaibisha wantaaluma wa TZ Kama vile Dk Slaa, Prof Baregu nA Prof Safari!!

Mzee slaa... kwa elimu yake ya viji certificate katika kusomea upadre ... ndio mnamuona dr. wa ukweli...?
 
Back
Top Bottom