Waziri Nchimbi akimbia na sanduku la kura wakati madiwani wakigombana

Esoterica

Member
Jun 18, 2011
48
11
Waziri Nchimbi akimbia na sanduku la kura Songea
blank.gif
Madiwani warushiana makonde
VURUGU kubwa zimezuka jana mjini hapa baada ya baadhi ya madiwani kurushiana makonde na kumlazimu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. John Nchimbi, kukimbia na sanduku la kura nje ya ukumbi baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa meya yanayohofiwa kuchakachuliwa...

Source: Tanzania Daima
 
Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,877
6,833
KATIKA hali isiyo ya kawaida, Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma, wamerushiana makonde na kusababisha uchaguzi wa meya kuvunjika. Hatua hiyo ilitokana na baada ya Naibu meya wa halmashauri hiyo, Mariam Dizumba, kudaiwa kuiba kura zilizopigwa na madiwani hao kwenye uchaguzi wa kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Meya wa halmashauri hiyo, Ally Manya, aliyefariki dunia miezi michache iliyopita. Kutokana na mapigano hayo baadhi ya madiwani walijikuta wakijeruhiwa na wengine kupoteza simu na vitu vya thamani.Katika uchaguzi huo, ulioanza kwa malumbano makali yaliyodumu kwa zaidi ya dakika 20 kati ya madiwani wa Chadema na wenzao wa CCM, ambao walikuwa wanajadili jinsi uchaguzi huo utakavyokuwa huru na haki kutokana na upinzani kutosimamisha mgombea.

Kutokana na hali hiyo, Msimamizi wa uchaguzi ambaye pia ni Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Nachoa Zakaria, alitoa ufafanuzi wa kanuni za uchaguzi wa nafasi hiyo, huku akiwataka kupiga kura za ndiyo au hapana na kwamba, wapiga kura halali waliojiorodhesha ni 26, akiwamo na Mbunge wa Songea Mjini, Dk Emmanuel Nchimbi. Baada ya hali hiyo kutulia, Zakaria aliita orodha ya wajumbe na kuwataka kuchukua karatasi za kupigia kura, madiwani wote walipiga kura na kuitwa kuzihesabu. Zoezi la hesabu lilipomalizika, Naibu meya Dizumba alilisimama na kuanza kutangaza matokeo, akitaja mgombea pekee wa CCM, Charles Mhagama, alipigiwa kura za ndiyo 14 na hapana 12.

Dizumba alisema kutokana na matokeo hayo, Mhagama ndiye meya mpya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea.“Naomba msimamizi wa uchaguzi umwite Diwani Mhagama avae joho la Umeya na kukalia kiti chake,” alisema Dizumba. Baada ya Msimamizi kumwita Mhagama na kumtaka kuvaa joho la Umeya, baadhi ya madiwani walimtaka msimamizi kuhesabu upya kura hizo ili madiwani wote washuhudie.

“Naomba msimamizi usitishe zoezi la kumtaka Diwani Mhagama akalie kiti cha Umeya, kwa sababu kuna mashaka makubwa na zoezi la utangazaji matokeo, hivyo zihesabiwe kura upya na madiwani wote wazione,” alisema Diwani wa Kata ya Mfaranyaki, Seneta Yatembo. Wakati wakiendelea kuzozana, Diwani wa Viti Maalum (Chadema), Rhoda Komba, akawaita madiwani wenzake kushuhudia Dizumba alivyokuwa anaiba kura zilizopigwa za hapana kutoka kwenye sanduku la kura, huku akichukua kura za ndiyo kutoka kwenye mkoba wake kuziweka ndani ya sanduku.

Hali hiyo ilisababisha vurugu kubwa na kumfanya Dk Nchimbi kukimbia na sanduku la kura kuelekea nje ya ukumbi, kabla ya kunyang’anywa na kutakiwa kulirudisha ndani na madiwani wakiongozwa na wenzao wa Chadema. Baada ya tafrani hiyo, madiwani wa Chadema waliitisha kikao na waandishi wa habari na kutoa tamko la kutomtambua Mhagama kuwa meya na kwamba, wameomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), kuitisha uchaguzi mwingine. Chadema ina madiwani saba na CCM 20. Kwa upande wa madiwani wa CCM, walisema walichofanya wenzao wa Chadema kwa kufanya fujo na kutaka kuwapiga wengine ni kitendo kibaya, kukuza demokrasia.

Mwananchi
 
Esoterica

Member
Jun 18, 2011
48
11
Waziri Nchimbi akimbia na sanduku la kura Songea
Madiwani warushiana makonde
VURUGU kubwa zimezuka jana mjini hapa baada ya baadhi ya madiwani kurushiana makonde na kumlazimu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. John Nchimbi, kukimbia na sanduku la kura nje ya ukumbi baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa meya yanayohofiwa kuchakachuliwa...

SOURCE: Tanzania Daima
 
Wed

JF-Expert Member
Mar 7, 2011
315
266

Kwa wanaoamini na kuipenda demokrasia, Iko habari ya aibu, ya kushangaza na ya kuhudhunisha iliyoandikwa na gazeti la Mwananchi kuhuu
"Madiwani CCM na wa Chadema, Songea kuzipiga kavukavu".
Jisomee mwenyewe !
Je, kwa mtindo huu, tutafikia demokrasia kweli ?

---------------
Madiwani CCM, Chadema Songea wazipiga kavukavu

KATIKA hali isiyo ya kawaida, Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma, wamerushiana makonde na kusababisha uchaguzi wa meya kuvunjika.
Hatua hiyo ilitokana na baada ya Naibu meya wa halmashauri hiyo, Mariam Dizumba, kudaiwa kuiba kura zilizopigwa na madiwani hao kwenye uchaguzi wa kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Meya wa halmashauri hiyo, Ally Manya, aliyefariki dunia miezi michache iliyopita.

Kutokana na mapigano hayo baadhi ya madiwani walijikuta wakijeruhiwa na wengine kupoteza simu na vitu vya thamani.Katika uchaguzi huo, ulioanza kwa malumbano makali yaliyodumu kwa zaidi ya dakika 20 kati ya madiwani wa Chadema na wenzao wa CCM, ambao walikuwa wanajadili jinsi uchaguzi huo utakavyokuwa huru na haki kutokana na upinzani kutosimamisha mgombea.

Kutokana na hali hiyo, Msimamizi wa uchaguzi ambaye pia ni Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Nachoa Zakaria, alitoa ufafanuzi wa kanuni za uchaguzi wa nafasi hiyo, huku akiwataka kupiga kura za ndiyo au hapana na kwamba, wapiga kura halali waliojiorodhesha ni 26, akiwamo na Mbunge wa Songea Mjini, Dk Emmanuel Nchimbi.

Baada ya hali hiyo kutulia, Zakaria aliita orodha ya wajumbe na kuwataka kuchukua karatasi za kupigia kura, madiwani wote walipiga kura na kuitwa kuzihesabu.

Zoezi la hesabu lilipomalizika, Naibu meya Dizumba alilisimama na kuanza kutangaza matokeo, akitaja mgombea pekee wa CCM, Charles Mhagama, alipigiwa kura za ndiyo 14 na hapana 12.

Dizumba alisema kutokana na matokeo hayo, Mhagama ndiye meya mpya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea.“Naomba msimamizi wa uchaguzi umwite Diwani Mhagama avae joho la Umeya na kukalia kiti chake,” alisema Dizumba.
Baada ya Msimamizi kumwita Mhagama na kumtaka kuvaa joho la Umeya, baadhi ya madiwani walimtaka msimamizi kuhesabu upya kura hizo ili madiwani wote washuhudie.

“Naomba msimamizi usitishe zoezi la kumtaka Diwani Mhagama akalie kiti cha Umeya, kwa sababu kuna mashaka makubwa na zoezi la utangazaji matokeo, hivyo zihesabiwe kura upya na madiwani wote wazione,” alisema Diwani wa Kata ya Mfaranyaki, Seneta Yatembo.

Wakati wakiendelea kuzozana, Diwani wa Viti Maalum (Chadema), Rhoda Komba, akawaita madiwani wenzake kushuhudia Dizumba alivyokuwa anaiba kura zilizopigwa za hapana kutoka kwenye sanduku la kura, huku akichukua kura za ndiyo kutoka kwenye mkoba wake kuziweka ndani ya sanduku.

Hali hiyo ilisababisha vurugu kubwa na kumfanya Dk Nchimbi (ambaye ni WAZIRI wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo) kukimbia na sanduku la kura kuelekea nje ya ukumbi, kabla ya kunyang’anywa na kutakiwa kulirudisha ndani na madiwani wakiongozwa na wenzao wa Chadema.

Baada ya tafrani hiyo, madiwani wa Chadema waliitisha kikao na waandishi wa habari na kutoa tamko la kutomtambua Mhagama kuwa meya na kwamba, wameomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), kuitisha uchaguzi mwingine. Chadema ina madiwani saba na CCM 20.

Kwa upande wa madiwani wa CCM, walisema walichofanya wenzao wa Chadema kwa kufanya fujo na kutaka kuwapiga wengine ni kitendo kibaya, kukuza demokrasia.

Mwananchi,
Friday, 23 September 2011 19:39
Madiwani CCM, Chadema Songea wazipiga kavukavu

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,565
7,940
Kwa uelewa wangu inapotokea kwamba mgombea ni mmoja na kupigiwa kura za ndiyo na hapana, wakati wa kuhesabu kura mgombea huyo anateua wakala wake na kikao husika huteua wakala atakayeangalia kura za hapana.

Sasa katika hili sakata la songea ni utaratibu gani wa kuhesabu kura ulitumika? Alihesabu kura naibu meya peke yake ama alishirikiana na wakala wa mgombea na hakukuwa na wakala wa kura za hapana?

Hata hivyo hii ni dalili tosha kwamba viongozi wa ccm kuanzia ngazi za chini wamekosa uadilifu kabisa, wizi na uchakachuaji wa kura imekuwa ni kitu cha kawaida sana kwao na hii ni aibu na mfano mbaya kwa vizazi vijavyo.
 
King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,801
24,508
sasa nchimbi kutoka nduki na sanduku la kura kichwani maana yake ilikua nini? watu 26 wanashindwa kupiga kura bila kuibiana? na huyo mwenye kuficha kura za ndiyo kwenye pochi,ina maana wakihesabu nae alikua amesimama next to ambazo hazijahesabiwa? i mean,inakuaje mgombea anakua pembeni ya sanduku na kubadilisha kura? wanasiasa mnatuchosha sasa!
 
Wamezoea kuiba kura hao, kwahiyo si ajabu kusikia habari ya kukimbia na sanduku la kura.

Makongoro Mahanga naye alifanikiwa kuingia mjengoni kwa staili hiyo hiyo ya kuiba masanduku ya kura na kuingiza kura zake mwenyewe.
 
King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,801
24,508
yaani nachoka nikipata picha mzee mzima na sanduku la kura kichwani sijui kwapani! ukiwa na mishipa ya aibu,ccm hapakufai!

Wamezoea kuiba kura hao, kwahiyo si ajabu kusikia habari ya kukimbia na sanduku la kura.

Makongoro Mahanga naye alifanikiwa kuingia mjengoni kwa staili hiyo hiyo ya kuiba masanduku ya kura na kuingiza kura zake mwenyewe.
 
ntamaholo

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
12,720
6,468
Waziri Nchimbi akimbia na sanduku la kura Songea
blank.gif
Madiwani warushiana makonde
VURUGU kubwa zimezuka jana mjini hapa baada ya baadhi ya madiwani kurushiana makonde na kumlazimu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. John Nchimbi, kukimbia na sanduku la kura nje ya ukumbi baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa meya yanayohofiwa kuchakachuliwa...

Source: Tanzania Daima

KURUSHIANA MAKONDE, NI ISHARA YA KUELEKEA PAZURI. mNAWAKUMBUKA WAKENYA WALIVYOKUWA?
 
mchemsho

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
3,213
856
Leo madiwani, mara wabunge, je siku wafuasi wao wakiamua nao kuzichapa kavukavu si ndo amani kwishneyi?? Uroho wa madaraka wa Ccm utaifikisha nchi yetu pabaya.!
 
TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
575
Nilikuwa ukumbini na kushuhudia sakata hili,baada ya kupigwa kura,kura za Hapana zilipatikana 14 na kura za Ndio zilikuwa 12,baada ya Nchimbi kuona meya aliyekuwa akimtaka yeye apita amekataliwa akaamua kutumia umafya wa kuforce matokeo na kwa kushirikiana na naibu meya wakatangaza matokeo kinyume,ndipo moto ulipoanza kuwaka,wakaitwa madiwan wawil pale mbele wahesabu kura zile na baada ya kuhesabu tena kura zile,matokeo yalionesha Hapana ni 14 na NDIO ni 12,hapo ndipo naibu Meya Marium Dizumba alipoiba kura na kuzificha kwenye Chupi na sio kwenye pochi waandish wanapotosha,hali ilikuwa tete na kusababisha Diwan wa kata ya misufin(chadema)salumu mfamaji kugongwa na gar na kada wa chama cha mapinduz,bwana Nchimbi wazir aliamua kukimbia na sanduku la kura baada ya kuona wameshikwa pabaya.wanachokifanya ccm ni kulazimisha kumpitisha meya jambaz ambaye sio wananch tu hata madiwan wenzake wa ccm hawamtaki.Wanaharakat wote tuungane kote tz kusimamia hak na kupinga wale wote naotaka kutupeleka watanzania kubaya kwa maslah yao binafsi.
 
TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
575
Naibu meya wa songea mjini Marium Dizumba jana alisababisha uchaguzi wa umeya wa manispaa ya songea kuvurugika baada ya kuiba kura na kuzificha kwenye chupi,ili kumuwezesha ndugu Charles Mhagama kushinda nafas hiyo.

Wananchi na madiwan wengi wakiwemo na wa ccm hawamtaki bwana Mhagama awe meya wa manispaa yetu ya songea kwa kuwa hana sifa za uhadilifu hata kidogo na alipitishwa ili akasimamie maslahi ya wachache akiwemo mbunge Emanuel Nchimbi, kilichofanyika ni madiwani wa chadema kuungana na baadhi ya madiwan wa ccm na kupiga kura ya hapana,zoez hil liliwezekana na kura za hapana zilipatikana 14 na za Ndio 12. Hapa ndipo walipotaka kufanya njama za kubadil matokeo ili yawe kinyume, hali iliyosababisha naibu meya Marium Dizumba bila aibu kuiba kura na kuzificha kwenye chupi, huku wazir Nchimbi akikimbia na sanduku la kura nje ya ukumbi.

Wakati hali hii ikiendelea madiwan wa ccm na chadema wakazipiga kavu kavu ndan ya ukumbi huo wa manspaa huku kada mmoja wa chama cha mapinduzi Hamisi abdalar Ally akimgonga na gari nje ya ukumbi, diwani wa kata ya misufin chadema bwana Salumu Mfamaji na kumsababishia maumivu makali.
 
Black Devil

Member
Mar 16, 2011
58
8
Te he he he....

“Small nations are like indecently dressed women. They tempt the evil-minded.” -Mwl Julius Nyerere.

Nilikuwa ukumbini na kushuhudia sakata hili,baada ya kupigwa kura,kura za Hapana zilipatikana 14 na kura za Ndio zilikuwa 12,baada ya Nchimbi kuona meya aliyekuwa akimtaka yeye apita amekataliwa akaamua kutumia umafya wa kuforce matokeo na kwa kushirikiana na naibu meya wakatangaza matokeo kinyume,ndipo moto ulipoanza kuwaka,wakaitwa madiwan wawil pale mbele wahesabu kura zile na baada ya kuhesabu tena kura zile,matokeo yalionesha Hapana ni 14 na NDIO ni 12,hapo ndipo naibu Meya Marium Dizumba alipoiba kura na kuzificha kwenye Chupi na sio kwenye pochi waandish wanapotosha,hali ilikuwa tete na kusababisha Diwan wa kata ya misufin(chadema)salumu mfamaji kugongwa na gar na kada wa chama cha mapinduz,bwana Nchimbi wazir aliamua kukimbia na sanduku la kura baada ya kuona wameshikwa pabaya.wanachokifanya ccm ni kulazimisha kumpitisha meya jambaz ambaye sio wananch tu hata madiwan wenzake wa ccm hawamtaki.Wanaharakat wote tuungane kote tz kusimamia hak na kupinga wale wote naotaka kutupeleka watanzania kubaya kwa maslah yao binafsi.
 
Leonard Robert

JF-Expert Member
Apr 22, 2011
10,621
6,282
Na bado ngumi zitapigwa sana tena za 2015 sizipatii picha..umepole umetuponza sana,hivi huyu Nchimbi kwani hakupigwa ngumi za kutosha? Jamaa mtu mzima hovyo wanae wanasikia limekimbiza sanduku la kura,haya majambazi ya ccm dawa ni kuyagonga! Nyambafuu!!!
 
Ngonini

JF-Expert Member
Sep 1, 2010
2,023
562
Hii ngoma ya watu 20 tu mbo rahisi sana wanaweza kurudia hata mara kumi mpaka pande zote zikaridhika ndo watangaze matokeo! Kama ccm hawataki basi wanajua kuna kitu maaana kama ushindi uko wazi kwanini wang'ang'anie?
 
Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,618
2,123
CCM mpaka wanajiibia wenyewe maana madiwani wao kama sikosei wanafika 19 wakati wa upinzani ni 7 kama sikosei
Sasa apao ushindi si wazi wazi au Nchimbi alikuwa na Mteule wake apo alikuwa anataka kuforce king?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom