Waziri Nchemba: Napendekeza Wakuu wa Mashirika ya umma wafanyiwe usaili kwa ushindani badala ya teuzi kama awali

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
Napendekeza wakuu wote wa mashirika ya umma wafanyiwe usaili kwa ushindani. Napendekeza nafasi zianze kutangazwa punde nafasi ikiwa wazi ili wenye sifa wajitokeze na wafanyiwe usaili na iwe hivyo hivyo kwa bodi. Wenye sifa ndio wafanyiwe upekuzi kufanyiwa uteuzi na kupewa mkataba wenye malengo yanayopimika.

Mashirika na taasisi zingine, bodi na Menejimenti zimezidisha urafiki sana na wanaendesha ofisi kirafiki, hakuna uwajibikaji wa kutosha, hii inakiuka misingi ya mashirika kuwa na bodi za wakurugenzi. Hii inasababisha watu wakikabidhiwa shirika la umma wanageuza ni mali yao au duka.

--
Mheshimiwa Spika, napendekeza mashirika yote ya umma yenye kufanya kazi kwa misingi ya kibiashara yafanye kazi kwa ufanisi na faida. Yale yasiyofanya kazi kibiashara tutayapima kwa namna wanavyowezesha uchumi kuchangamka na jinsi wanavyoimarisha huduma wanazozitoa kwa jamii. Mashirika mengi ni mzigo kwa Serikali kwa kutegemea ruzuku kutoka serikalini ili yajiendeshe.

Kwa nchi zilizoendelea, mapato makubwa ya Serikali yanatoka kwenye mashirika yake ili kuwapunguzia mzigo maskini wa kulipa kodi ili ziendeshe mashirika hayo lakini pia kupunguzia Serikali kutegemea kukusanya fedha kutoka kwa watu maskini.

Napendekeza wakuu wote wa mashirika ya umma wafanyiwe usaili kwa ushindani. Napendekeza nafasi zianze kutangazwa punde nafasi ikiwa wazi ili wenye sifa wajitokeze na wafanyiwe usaili na iwe hivyo hivyo kwa bodi. Wenye sifa ndio wafanyiwe upekuzi kufanyiwa uteuzi na kupewa mkataba wenye malengo yanayopimika.

Mashirika na taasisi zingine, bodi na Menejimenti zimezidisha urafiki sana na wanaendesha ofisi kirafiki, hakuna uwajibikaji wa kutosha, hii inakiuka misingi ya mashirika kuwa na bodi za wakurugenzi. Hii inasababisha watu wakikabidhiwa shirika la umma wanageuza ni mali yao au duka.
 
Kama amependekeza jambo hili basi ni jambo muhimu sana kuliko maelezo.

Na Rais Samia atakuwa akikumbukwa kwa uzuri kuwa ni awamu ya uongozi wake ndipo jambo hili nyeti liliamuliwa kuwepo na usaili kwa ma CEOs badala ya teuzi nafasi zitangazwe Kwa uwazi na usaili huru na wa haki.

Hii itaongeza na kuboresha tija maradufu katika performance.
 
Kwa hili akilipigania basi vizazi na vizazi vitamkumbuka Mh Mwigulu na Rais Mama Samia...

Waende mbali zaidi hata hizi nafasi za wakurugenzi zisiwe za uteuzi bali ziwe zinatangazwa watu waombe...anapita kwenye interview anafanyiwa vetting then anapewa target yake anaanza kuhudumu..
 
Kila miaka 3 au 5 CEO wote wafanyiwe evaluation kama wafaa kuendelea na kazi kupitia tume huru kama hawakuleta productivity na faida yoyote waondolewe usaili mpya ufanyike kupata wengine pia wakurugenzi wa manispaa na wilaya tathimini pia zifanyike
 
Sio hao tu, mpaka mawaziri, wakurugenzi nk wote hao wafanyiwe usaili apewe kazi mwenye uwezo na sio mwenye kadi ya CCM. Hii kila kitu kupewa rais ndio kumepelekea taasisi nyingi hapa nchini kuwa dhaifu. Na mamlaka ya kuwawajibisha isiwe rais.
 
Hili sio jipya. Limefanyika sana wakati wa Kikwete, sasa hivi tunakwama wapi?
 
Kila miaka 3 au 5 CEO wote wafanyiwe evaluation kama wafaa kuendelea na kazi kupitia tume huru kama hawakuleta productivity na faida yoyote waondolewe usaili mpya ufanyike kupata wengine pia wakurugenzi wa manispaa na wilaya tathimini pia zifanyike
Kwenye maelezo akasema wapewe mkataba wenye malengo yanayopimika
 
Mbona CCM midahalo tu wanakimbia?

Usaili wakihonga wanaoendesha usaili tutajuaje?

Jiwe alikimbia midahalo na maswali na wanaccm wengine wakafuata.

Tunataka midahalo huru kwanza halafu ndio tuanze usaili wa wakuu wa mikoa na wilaya huko ndio kuna mabomu ya kutosha.
 
Kama amependekeza jambo hili basi ni jambo muhimu sana kuliko maelezo.

Na Rais Samia atakuwa akikumbukwa kwa uzuri kuwa ni awamu ya uongozi wake ndipo jambo hili nyeti liliamuliwa kuwepo na usaili kwa ma CEOs badala ya teuzi nafasi zitangazwe Kwa uwazi na usaili huru na wa haki.

Hii itaongeza na kuboresha tija maradufu katika performance.

Sio ile January Makamba anateua CEO wa Tanesco na bodi yake kabisaa
 
Back
Top Bottom