Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Ni hivi karibuni, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na michezo, Nape Nnauye amenukuliwa akivitaka vyombo vya habari kutoogopa kuikosoa Serikali.
Hata hivyo, tangu kutolewa kwa kauli hiyo, tumeshuhudia vyombo hivyo vikija na habari nyingi za kupika na uzushi dhidi ya Serikali na viongozi wake.
1. Gazeti la Tanzania Daima limeripoti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekimbia nchi na kwenda kujificha Afrika ya Kusini ambako amepewa likizo ya zaidi ya miezi miwili. Sina hakika kama Nape amechukua hatua dhidi ya Gazeti hilo au kwa vile habari hiyo ililenga kumdhalilisha hasimu wake.
2. Gazeti la Sani liliandika kwenye front page kuwa Paul Makonda amesafirishwa na Wauza Madawa ya Kulevya kwenda Afrika ya Kusini tena wakitajwa kuwa ni GSM. Sikumbuki kama kuna kauli yoyote imetolewa juu ya habari hiyo.
3. Na sasa gazeti la Mwananchi limeingia kwenye orodha ya Magazeti yanayolenga kumchonganisha Rais na Watanzania. Yaliyoandikwa kwenye gazeti hilo hayana uthibitisho wowote kwa vile kikao hicho kilikuwa ni cha ndani na vyombo vya habari havikuwepo. Pia hata wabunge hawakuruhusiwa kwenda na simu zao hivyo, hakuna uhalali wowote wa Gazeti la Mwananchi kuandika habari hiyo.
Hivi Gazeti la Mwananchi wakitakiwa kutoa ushahidi wa hicho walichoandika watakuwa nao? Na je wapo tayari kuhimili hatua za kisheria zitakazochukuliwa dhidi yao?
Nikusihi sana mdogo wangu Nape Nnauye. Ukiendelea kuchunga mbuzi shambani kwako basi ujue hakuna utakachovuna isipokuwa mbuzi hao. Habari hii ya Mwananchi imemjengea Rais wetu maadui wengi na chuki katika jamii. Nimemuona hata Lema naye amejitokeza kusema palipomgusa. Huu ni wakati wa kuchukua hatua. Usipochukua hatua wewe basi uwe tayari kuwajibishwa kwa kushindwa kutekeleza vema majukumu yako. Usipochukua hatua sitashangaa ukiwekwa pembeni licha ya hivi juzi umepokea sifa lukuki kutoka kwa Rais wetu. Sifa zimekulewesha
Nikisihi pia chama changu, CCM, chukueni hatua dhidi ya Gazeti la Mwananchi. Msipofanya hivyo uzushi huu utageuka kuwa kweli.