Waziri Nape umeanza vibaya kwanza Kwa msiba lakini pia kwa kauli isiyotekelezeka, Mkipewa nafasi Jikabidhini kwa MUNGU Kwanza awape hekima

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Poleni wote mliopatwa na msiba baada ya ajali iliyosababisha vifo vya wanahabari kadhaa huko Mwanza.

Pili nichukue fursa Hii kumwombea msamaha Mhe. Nape Kwa kuteleza wakati anatoa salamu za rambirambi. Nasema nimwombee msamaha kwa sababu alichokisema hakitekelezeki Kwa njia yoyote Ile. Naomba kueleza kwanini hakitekelezeki

1. Amevitaka VYOMBO vya habari kuwalipa stahiki zao marehemu ndani ya siku Saba; naomba kumuuliza Mhe. Waziri amewahi kupata msiba wa mtendaji aliyepo chini yake? Kama amewahi kupata msiba Tena wa ghafla kama huu atakubaliana na Mimi Kwamba watumishi wenzao na marehemu wanakuwa busy kuhakikisha Kwamba wanafanikiwa kumhifadhi mpendwa wao.

Hapa hakuna mtu mwenye uchungu uwaza madeni na mambo mengine bali WATU uwaza walivyompoteza mwenzao na namna gani ahifadhiwe. Shughuli uchukua wiki Hadi wiki mbili ofisi kutulia, Je waache msiba wafuatilie madeni anayodai na ambayo awajawahi kufikiria kuwadhulumu? Kwanini amekosa Imani na wamiliki wa VYOMBO vya habari mapema hivi? Atawezaje kushirikiana na WATU asiowaamini?

2. Marehemu azungumzi na wala halipwi Chocho wanalipwa wanafamilia. Mhe. Waziri unataka kutuaminisha kwamba familia za wana habari tayari zimeteua WATU wakulipwa haki za wapendwa wao?Kwamba ndani ya siku Saba familia zitakuwa zimekamilisha taratibu zote zakuteua utaratibu wa malipo na kuwasilisha kwa mwajiri? Nadhani Mhe. Waziri alipaswa kutoa neno la pole na kutoa rambirambi kuliko kuwaza Madara yake kwamba Yana nguvu kiasi gani.

3. Ameeleza Msibani kwamba leseni za wamiliki wa vyombo vya habari zipo mikononi mwake means anaweza kufunga na kufungua anavyojisikia. It's fine lakini atueleza kifungu gani kinampa mamlaka yakukiwajibisha chombo Cha habari kisipolipa haki za marehemu ndani ya siku Saba? Je alijipanga kuyasema haya au roho mchafu katingisha stability yake?

4. Ameongea kuhusu ajali akionesha kwamba kuna aina ya hujuma japo ajasema Moja Kwa Moja but it's like anaamini ajali za wanahabari si zakawaida. Ametaka jeshi la Polisi kuwasilisha ripoti kwake, Je tatizo lililotajwa na Polisi kwamba gari zilikuwa speed hakubaliani nalo? Arejee speed ya msafara wake aone kama je kwa miundombinu yetu speed zinakidhi au kunahitajika marekebisho kulinda afya za wanamsafara wa viongozi?

Kwa kifupi Nape ameteleza japo ajaanguka, nimwombee msamaha kwa utelezi uliomzinga ila pia nimwombe atulie na kumwomba Mwenyenzi Mungu amsaidie Nini aseme na aseme wapi na wakati gani. Poleni wamiliki wa vyombo vya habari kwa kuonekena wadhulumati
 
kwa hapa tunatofautiana, ni kawaida sana waajiri wa vyombo vya habari kulalamikiwa juu ya stahiki za waajiriwa.

alichofanya Nape ni kuwakumbusha waajiri wa MEDIA wajibu wao, kimsingi ni jukumu lake.

hayo ya kulalisha misiba sijui wiki ni yenu wahaya mama(jokes). Ila kwa familia nyingi kikao cha kumteua msimamizi wa mirathi ni dakika 30 tu, sijajua kwako ugumu umeupata wapi.

Mwacheni mh.waziri afanye kazi, tuache chuki na majungu, havisaidii kama taifa
 
Umewasilisha hoja murua, hakika ktk siku saba hayo hayawezekani kabisa. Inapotokea kadhia kama hiyo kuna taratibu zinatakiwa kukamilishwa kwanza:
1. Kikao cha familia cha kuchagua msimamizi wa Marathi
2. Kupata Cheti cha kifo kutoka RITA
3. Msimamizi wa Marathi kufungua kesi mahakamani
4. Kuwekwa kwa tangazo la siku tisini kama kuna mwanafamilia anapiga uteuzi wa msimamizi, na kutambua wadai na wadau wa
5. Kesi kuendeshwa na hatimaye warithi kupewa haki zao

Hakika Waziri ktk hili katelezea kusiko salama
 
Huu ni utopolo.
Waandishi wa jabari wanateseka sana, hawakipwi kwa wskati.
Nani hajui kuwa waandishi wa habari wa;
1. Star tv
2. Itv
Kuwa wanateseka kwa kutolipwa kwa wakati hadi miezi 3?
 
Ndio kwanza ameingia ofisini.....

Tumwache mh.komredi Nape Nnauye aifanye kazi njema TUNAYOISUBIRI🙏

Kila la heri kwake aaamin🙏

#Siempre JMT
 
Hafai huyo kuwa mtumishi wa serikali au umma labda kwenye chenye majungu na fitina.

Waandishi wa habari mlikosea sana hapo mwanzo kumpa sifa za kumfanya ajawe na kiburi na majigambo kutokana na sakata lake la kuvuliwa uwaziri baada ya kujimilikisha mamlaka ya kuunda tume wakati hana malaka hayo kuchunguza tukio la aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar kwenda kituo cha utangazaji CM akiwa na kikosi kazi usiku.

Huyo kabembeleza kupata nafasi hiyo kupitia kwa visiki wa chama hicho ili aende kulipa kisasi sio kuwatumikia wananchi wizarani.

Huyu hawezi kudumu kwenye nafasi hiyo labda watanzania sio nchi yao.
 
Hakika umezungumza hoja zenye mashiko. Waziri nnape angejaribu kutoa maoni au mapendekezo na sio amri au agizo. Kwasababu hao waajiri wanaweza kufanya hata zaidi ya hayo madai kwa familia za marehemu. Ikiwa ni pamoja na kuwapa mafao yao, kusaidia familia zao wakiwemo watoto kwa mujibu wa taratibu au utu.

Kitendo cha kutoa amri/agizo hilo kwa wakati kama huu wa majonzi ni kutengeneza mgogoro!
 
Issue ya kuomba report iende kwake ni namna ya kuangalia jinsi gani wanapunguza ajari za waandishi wa habari kwenye misafara ya viongozi.
 
kwa hili alilosema nape,yuko sahh kabisa,japo tangu aliposema unajua mm ni nani,halafu kumbagaza jiwe,ukweli huwa simfuatilii tena.ila kwenye ukweli na haki lazma tuseme ukweli,amenena vyema na kutaka haki kwa wafiwa,ni vizuri!!
 
1. Amevitaka VYOMBO vya habari kuwalipa stahiki zao marehemu ndani ya siku Saba.
hapa nimepata kigugumizi aliposema hata wauze mali zao.

Serikali ijitazame ktk hili kuna watu wanakaa miaka na miaka kupata haki zao, mabavu hayasaidi warekebishe utaratibu ukae sawa kwa wote.
 
Back
Top Bottom