Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,280
- 25,859
Najua kuwa siasa yaweza kuambatana na ahadi hewa,ulaghai na uongo. Lakini,yapo mambo ambayo hayapaswi kuahidiwa kwa ahadi za uongo,kilaghai na hewa. Mojawapo ya mambo hayo ni elimu. Waziri Nape kama Mbunge wa Jimbo la Mtama,mkoani Lindi aliahidi kuweka kambi katika Shule ya Msingi Litindi ili kuikarabati.
Kwa mujibu wa taarifa ya habari kupitia Star TV usiku huu,shule ya Msingi Litindi ina hali mbaya kitaaluma na kimiundombinu. Tangu kuanzishwa kwake,shule hii haijawahi kufaulisha hata mwanafunzi mmoja. Madarasa yake ni machache na duni;wanafunzi wengi wanasomea chini ya mti. Walimu wanasafiri kwa ugumu kila siku umbali wa kilometa ishirini kwenda na kurudi. Nyumba pekee ya Mwalimu Mkuu ni mbovu na ya kudhalilisha.
Hoja hapa ni kuwa Waziri Nape Nnauye,akiwa mgombea wa Ubunge aliahidi kuweka kambi shuleni hapo mara baada ya kuchaguliwa na kuboresha mazingira na miundombinu ya shule hiyo. Kwa aina ya maisha na hadhi ya Waziri Nape Nnauye siamini kuwa aliwadanganya wananchi wa Litindi. Namuomba kutimiza angalau ahadi ya maboresho ya shule hiyo kwakuwa si kioo kizuri kwake.