Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Waziri Nape kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika kuwa amesikitishwa sana na si sawa, kwani watu wanachukua na kutafsiri watakavyo kwa faida zao
Februari 13,2017 kupitia ukurasa wake huo, Waziri Nape alinukuliwa kwa kuandika kuwa "Ujinga ni mzigo mkubwa sana!! Omba busara ya Mungu kwa kila jambo kuliko utajiri na kiburi"
Waziri Nape katika Twitter yake aliambatanisha na kipande cha video cha Mchungaji Christopher Mwakasege akisema "Mkuu aliyepungukiwa na akili huwaonea watu sio kwamba hana akili bali amepungukiwa."
Waziri Nape amesema alicholiandika hakijamlenga na wala hajakiweka kwa makusudi yoyote yenye nia ya kumsema kiongozi yeyote, ni utaratibu wake kusoma ya Mwakasege.
Chanzo: Dar24