Waziri Nape Nnauye, akanusha juu ya katazo la Mavazi

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,486
Takribani siku mbili zilizopita zilienea taarifa juu ya katazo rasmi la mavazi ya nguo fupi ambalo ilisemekana limetolewa na wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Akiongea na Power Breakfast asubuhi ya leo, waziri mwenye dhamana ya Wizara hiyo, Mh Nape Nnauye amekanusha juu ya taarifa:

"Taarifa hizo si za ukweli, nasikitika sana watu wanatuma taarifa hiyo kwenye mitandao tofauti ya kijamii, Wizara imesikitika kwa kusambazwa kwa Taarifa hiyo ikianisha picha ya mavazi ambayo yamepigwa marufuku, naomba chombo kinachohusika kichukue hatua dhidi ya watu waliohusika na taarifa hiyo potofu ili watu wengine wajue sheria inafuata mkondo wake."

Mh. Nape Nnauye


Hii hapa chini,ndiyo habari ilikua ikisambazwa mitandaoni
969531_1015910715119013_2950541186505663123_n.jpg


===============================

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo inapenda kuujulisha Umma kwamba kumekuwapo na upotoshwaji unaondelea katika mitandao ya kijamii hususan facebook, Instagram na WhatsApp ambaposehemu ya upotoshaji huo imenukuliwa kama ifuatavyo;

“Wizara imetoa tamko kuwa kuanzia januari 2016 mavazi yote yasiyo stahiki ambayo hayaendani na mila na desturi zetu Wizara yangu na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haitafumbia macho mavazi hayo.

HAYARUHUSIWI KUVALIWA SEHEMU ZIFUATAZO
1. Kwenye masoko makubwa
2. Hospitali kubwa(Private or Public)
3. Maofisini na Vyuoni
4. Mijini kwenye mikusanyiko ya watu wengi
Hatua kali za kisheria zitachukuliwa endapo kwa wale ambao watavaa mavazi haya ikiambatana na faini ya sh. 100,000/=” mwisho wa kunukuu.
Tunachukua fursa hii kukanusha vikali taarifa hizo kuwa siyo za kweli na kwamba mhusika amefanya uhalifu wa kimtandao kwa kuaanda taarifa yake ya uongo na kuibandika katika uso wa Tovuti ya Wizara yenye anuani: www.habari.go.tzvkwa lengo la kuipotosha jamii.

Kufuatia uharifu huo Serikali inatoa onyo kali na haitawavumilia wale wote wanaokiuka misingi ya sheria ya mtandao ya mwaka 2015 ambayo inakataza kusambaza taarifa za uongo na haitasita kuwasifikisha katika vyombo vya sheria wale wote watakaobainika kufanya uharifu huo.
Pamoja na upotoshaji huo wa makusudi napenda pia kutumia wasaa huu kuwakumbusha watumishi wa umma na jamii yote kwa ujumla kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma inao Waraka wa Utumishi wa Umma Na. 3 wa mwaka 2007 kuhusu mavazi kwa watumishi wa Umma. Waraka huo umeainisha mavazi ambayo hayafai kuvaliwa katika ofisi za umma kwa wanawake na wanaume; aidha umeelekeza aina za mitindo ya nywele isiyofaa pamoja na aina za viatu visivyofaa.

Mifano ya mavazi yasiyokubalika kwa watumishi wa umma wanawake ni kama vile nguo zinazobana, nguo fupi ambazo zinaacha magoti wazi, nguo ambazo zinaacha sehemu ya mwili wazi kama vile kitovu na kifua, nguo ambazo zina picha, michoro, na maandishi ambayo hayaendani na shughuli za Serikali, kaptura aina yoyote ile kama vile pedo na pensi, nguo zinazoonyesha maungo ya mwili (transparent), suruali za ‘Jeans’, na nguo zingine zote zenye kukinzana na maadili ya utumishi wa umma na jamii kwa ujumla.

Aidha, kwa upande wa wanaume mavazi yasiyokubalika ni pamoja na nguo ambazo ni za kazi maalum kama vile michezo (hizi zivaliwe wakati wa shughuli hiyo tu), nguo ambazo zina michoro, maandishi na picha ambazo haziendani na shughuli za Serikali, nguo zinazobana, kaptura ya aina yoyote, suruali yoyote inayoachwa bila kupindwa, suruali za “Jeans” na Fulana “T-shirts” (Hizi zivaliwe tu wakati wa shughuli maalum inayotambulika), Kikoi au msuli, nguo zenye maandishi ya chama chochote cha siasa na yenye kuonyesha ushabiki wa kitu fulani.

Pamoja na kuwepo kwa miongozo ya mavazi yanayostahili kwa watumishi wa umma, tafsiri ya mavazi ya heshima hutegemea mila na desturi ya jamii husika.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
 
Last edited by a moderator:
Mchafu anachafuliwaje?
Huyo keshajichafua peke yake zamani.
Ni kweli kabisa mkuu...Toka kitambo...Nape alikuwa mstari wa mbele kwenye kupambana na mafisadi...ref to Operesheni vua magamba na Operesheni waziri mizigo ambapo Nape alikuwa Chief architect! Ila kwavile mmegeuka watetezi wa mafisadi, hamna budi kumchukia
 
Ni kweli kabisa mkuu...Toka kitambo...Nape alikuwa mstari wa mbele kwenye kupambana na mafisadi...ref to Operesheni vua magamba na Operesheni waziri mizigo ambapo Nape alikuwa Chief architect! Ila kwavile mmegeuka watetezi wa mafisadi, hamna budi kumchukia
Like serious? Nape alikuwa mstari wa mbele kupambana na mafisadi gani?
Wataje walau watatu tu.
 
Ni kweli kabisa mkuu...Toka kitambo...Nape alikuwa mstari wa mbele kwenye kupambana na mafisadi...ref to Operesheni vua magamba na Operesheni waziri mizigo ambapo Nape alikuwa Chief architect! Ila kwavile mmegeuka watetezi wa mafisadi, hamna budi kumchukia
Like serious? Nape alikuwa mstari wa mbele kupambana na mafisadi gani?
Wataje walau watatu tu.
 
Like serious? Nape alikuwa mstari wa mbele kupambana na mafisadi gani?
Wataje walau watatu tu.
We bwa'mdogo inaonekana ulikuea haujaota meno kipindi cha operesheni vua gamba. Au kama ulikuwa umeota meno basi hukuwa mfuatiliaji wa mambo...
 
We bwa'mdogo inaonekana ulikuea haujaota meno kipindi cha operesheni vua gamba. Au kama ulikuwa umeota meno basi hukuwa mfuatiliaji wa mambo...
Kuota kwangu meno kunahusiana vipi na list niliyokuambia unitajie?
Well.....nilikuwa sijaota meno wala sikuwa mfuatiliaji wa mambo,wewe uliyekuwa mfuatiliaji naomba unipe list ya mafisadi Nape aliopambana nao.
 
Ila kusema ukweli hilo nalo ni tatizo.Mtu anavaa kata k,chupi lake chafu,bukta chafu,wanatia kinyaa mno.
 
Back
Top Bottom