Waziri Nape: Nimevifungia vituo viwili vya radio ambavyo ni Radio 5 Arusha na Magic FM ya Dar

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Habari wanaJamiiForums,


14102599_1254215291278006_3013395438954102977_n.png

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametangaza kuvifungia kwa muda usiojulikana vituo vya Radio 5 ya Arusha na Magic FM ya Dar es Salaam kwa sababu za uchochezi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Waziri Nape amesema kuwa vituo hivyo kwa nyakati tofauti zilitangaza habari ambazo ndani yake zina uchochezi.

“Adhabu hii ya kuvifungia kwa muda vituo hivyo viwili inaanza leo (Agosti 29 2016) hadi pale kamati itakapomaliza kazi yake,” alisema Nape.

Aidha, amesema kuwa ameiagiza Kamati ya Maudhui ya vyombo vya habari kuviita vyombo hivyo na kuvihoji kwa kina kisha kumshauri hatua zaidi ya kuchukua.

image.jpeg

image.jpeg


Waziri huyo ameeleza kuwa Serikali inaendelea kutambua mchango mkubwa wa vyombo vya habari katika kuleta amani na ushirikiano nchini na sio vinginevyo.

Hivi karibuni, Nape alitahadharisha kuwa vyombo vya habari vitakavyoripoti taarifa ambazo ni za uchochezi vitakumbwa na rungu la kuhusika kwa uchochezi pia.
 
Mbona magic fm naisikiliza sahivi? Ametangaza lini kuvifungia? Lazima kitakuwa ni kile kipindi cha Asubuhi cha akina Horice Kawawa.

Maanake ni nini:
Manake ni kwamba uckichambua siasa ni UCHOCHEZI
 
Mbona radio zilizofungiwa ni zile zenye kuonesha zina mrengo wa kuruhusu maoni ya kuisapot UPINZANI??

Hizo radio nyengine zina zowatukana wapinzan haziguswii
 
Radio Magic Fm inafanya kazi yake kwa weledi mkubwa na huwa hawapepesi pale wanaposimamia taaluma yao ikiwemo kuwaelimisha watanzania.

Tuchoshwe sasa kuendekeza ujinga ambao unaonekana dhahiri kutaka kushika hatamu nchini Tanzania!
 
Safi sana Magic Fm walizidisha mipaka... Hakika ninge shangaa sana hawa Magic kuachwa hivi hivi hakika wana stahili adhabu tena wale watangazaji wao wa Asubuhi wamewaponza... Mtu anasoma massage bila hata kuangalia hii ni massage ya aina gani ..

Safi sana Serikali.
 
Back
Top Bottom