The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 617
- 1,799
Waziri wa Habari, Nape Nnauye, leo Jumatatu, amesema muswada wa Sheria ya Ulinzi Binafsi, uko katika hatua za mwisho “hii ni sheria muhimu sababu vinginevyo uwekezaji utakuwa mgumu. Sio kwa sababu kulikuwa na kurekodi rekodi watu, hapana lakini ni kwa sababu ya kutunza faragha.”
Nape ametoa kauli hiyo leo Jumatatu, tarehe 14 Machi 2022, jijini Dar es Salaam, akielezea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Samia, iliyoingia madarakani Machi mwaka jana, kufuatia kifo cha Hayati John Magufuli.
Mbunge huyo wa Mtama kupitia CCM, amesema katika kipindi hicho mahusiano ya kimataifa na sekta zilizo chini ya wizara yake yameimarika.
“Serikali inaendeleza mashirikiano baina ya nchi, kikanda na kimataifa, kati ya sekta ya mawasiliano kupitia tume za pamoja za mashirikiano pamoja na jumuiya za mashirika ambayo Tanzania ni mwanachama. Wote tutakubaliana tunaposema ameifungua nchi,” amesema Nape.
Katika hatua nyingine, Nape amesema Serikali imetumia Sh. 93.5 bilioni, kwenye ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano, ikiwemo ujenzi wa minara 12 kwenye maeneo ya mipakani na kupeleka huduma za mawasiliano kwenye Hifadhi ya Burigi Chato, mkoani geita.
Pia, fedha hizo zimetumika kupeleka huduma hizo kwenye ofisi 10 za halmashauri za wilaya, ujenzi wa minara 42 kwenye visiwa vya Zanzibar, kuongeza uwezo wa minara 127 kutoka teknolojia ya 2G kwenda 3G na 4G.
Nape amesema, Serikali imetenga Sh. 170 bilioni, kwa ajili ya ujenzi wa mkongo wa taifa, wakati Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limetoa Sh. 3.7 bilioni kwa ajili ya kufikisha miundombinu ya mawasiliano katika mradi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere, mkoani Pwani.
PIA SOMA:
- Dkt. Ndugulile: Sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi inakuja