Waziri Nape kaachini na Bloggers mtengeneze kanuni za uendeshaji mitandao

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
13,610
2,000
Nalitizama sekeseke la Max kwa mtizamo tofauti kidogo, sidhani kama kama max ni mhalifu kwa kiwango tulichokichukulia, na sidhani kama ni mbishi kivile na kuwa hayuko tayari kwa mazungumzo kama Joseph Kony.

Nashauri Tanzania Bloggers Network iingilie kati hili sakata, iunde kikosi kazi na wakae na mawaziri wenye dhamana waangalie mapungufu yako wapi na kwa namna gani yanaweza fanyiwa kazi. JF nadhani ni netwk pekee hapa Bongo yenye moderators wengi na makini, mfano ukiweka neno ambalo Mod wanaamini ni tusi au la hovyo linakuwa deleted automatically na yapo maneno ambayo kwa JF ni machukizo japo sio matusi.

Nashauri kupitia TBN na MCT na TCRA wakae chini na waziri mwenye dhamana watunge kanuni za uendeshaji wa mitandao. Ikiwezekana iundwe appeal board ambayo itasikiliza malalamiko ya watu wanaoathiriwa na matumizi ya mitandao. Ukweli JF imejitahidi sana kuweka mambo sawa watu kilasiku wanakula BAN na topic kufutwa.

Tunaweza weka msajiri wa mitandao ambaye atakuwa na uwezo wa kuamuru picha fulani ziondolewe au topic fulani iondolewe, na kama mhusika ataona sio haki basi atapeleka malalamiko yake appeal board.

Binafsi michango ya JF sioni kama inatofauti na maswali yanayoulizwa kwenye mikutano ya makonda, yote inatoa picha ya uozo mahali fulani na tusiposikiliza basi hatutajua wapi pameoza.
 

MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Oct 23, 2013
8,949
2,000
Ushauri wako unaweza kuwa mzuri Mkuu...

Hakuna kitu Nape anachoweza kufanya kwa utawala huu.

Yupo pale lakini anakuwa remoted kwa kila kitu na Mkubwa.

TCRA nayo ndio sasa imejaa siasa tupu.

Majuzi tu hapa TCRA waliwahi kuipongeza JF kwamba ni mtandao umaoendeshwa vizuri kwa kufuata Sheria na kanuni zao..

Baada ya Max kukamatwa wamegeuka kuwa huu mtandao haujasajiliwa hapa... sijui mambo ya. com na .com.tz... yaani siasa tupu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom