Waziri Nape, Bando linamhujumu Rais, CCM na nchi yetu

Suphian Juma

Senior Member
Apr 2, 2019
132
541
WAZIRI NAPE, BANDO LINAMHUJUMU RAIS, CCM NA NCHI YETU.

Kaka Waziri, awali ya yote nikusalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa hakika unastahili pongezi za dhati kwa kuwa mstari wa mbele kuisimamia maridhawa Wazara ya Habari tangu Mheshimiwa Rais na Mwenyekiti wetu wa Chama cha Mapinduzi CCM akuteue. Kuna mabadiliko chanya mengi tunazidi kuyaona ambayo kwa dhati ya mioyo ya sisi wengi tuliyakosa takribani miaka 5 iliyopita. Kudos!!

Kaka Waziri, pamoja na mafanikio haya, leo kupitia BARUA HII YA WAZI naomba nilete kwako lalamiko la mamilioni ya WaTanzania ambalo limedumu kwa zaidi ya mwaka sasa bila kupatiwa tiba sahihi; KUPANDA KWA BANDO.

Lalamiko ambalo mimi binafsi mdogo wako Suphian Juma Nkuwi kama raia wa Tanzania pamoja na watumiaji wengi wa Huduma za mawasiliano tumelisemea mara kadhaa kwenye mtandao ya kijamii ambapo kama hatua ya usikilizwaji, Serikali yetu pendwa kupitia wewe kwa nyakati tofauti ikiwemo Jana Novemba 10, 2022 imeanza kulifanyia Uchaguzi na kuchukua hatua. Wanyaturu wa Singida huwa tunasema WAJIFYA INO (Ahsante sana).

Naleta hili lalamiko kwako nikitambua kwamba kwa mujibu wa Sera ya Taifa letu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ya mwaka 2016 iliyoboreshwa kutoka Sera ya Mawasiliano ya 2003, kwamba Serikali ndiyo Msimamizi na Mthibiti Mkuu wa Habari na Mawasiliano nchini kupitia Wizara ya Habari na Mawasiliano ambayo kwa sasa wewe ndiye Kiongozi Mkuu mlengwa.

Kaka Waziri,
Dira, Malengo Makuu ya Sera hii ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ambayo imeundwa kutokana na Dira ya Maendeleo ya Taifa inasema: wananchi watatumia teknolojia ya Habari na Mawasiliano kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi na hivyo kuifanya Tanzania kuingia uchumi wa Kati ifikapo mwaka 2025.

Kaka Waziri, napata mashaka kama Malengo haya kama tutayatimiza kwani Makampuni ya Simu nchini ambayo zaidi ya 90% ni mali ya SEKTA BINAFSI yanaonekana wazi kushindwa kutoa huduma ya bando kwa bei nafuu kulingana na vipato vya walaji wa Huduma zao za vifurushi vya "Internet" kinyume na maelekezo ya Sera ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya 2016 inayowataka watoa huduma hawa kuwapa wananchi huduma nafuu wanayoimudu ili kufurahia maendeleo ya Habari na Mawasiliano duniani na kujiletea Maendeleo yao na ya Nchi yao.

Tangu mwaka huu wa 2022 uanze pamekuwa na mabadiliko ya vifurushi vya Bando kwa kila Makampuni ya Simu; Vodacom, Tigo, Airtel, TTCL, Halotel na Zantel ambapo gharama za fedha zimebaki kama zilivyo lakini MB/GB zimekuwa zikipunguzwa mara kwa mara tena bila taarifa moja kwa moja kwetu walaji.

Kwa mujibu wa Gazeti la Mwananchi la Novemba 10, 2022 Makampuni haya ya simu yameonekana kuongeza bei ya vifurushi hususani vya internet (Mabando), nanukuu:

"Mathalan, katika moja ya mitandao hiyo, kifurushi cha gigabaiti 1.2 kwa siku tatu kiliuzwa Sh2,000, lakini sasa kiasi hicho cha fedha kinawezesha kupata megabaiti 985 tu, zikipungua kwa asilimia 17.9."

Gazeti hilo limeendelea kuelezea; "Katika mtandao mwingine nchini, kifurushi cha data kilichouzwa kwa Sh1,000 kiliwezesha megabaiti 450 kwa wiki, lakini sasa kwa bei hiyo zinapatikana megabaiti 350 sawa na upungufu wa asilimia 10."

Kaka Waziri,

Sio tu suala la kupanda kwa bei tu ya Bando bali pia hata hayo Mabando ambayo tunayanunua ghali nayo kwa siku ya Karibuni yameonekana kuisha haraka tofauti na matumizi ya kawaida ya sisi walaji tuliyoyazoea kulingana na Ujazo wa Mabando hayo, na hivyo kuhisi harufu ya utapeli au kuwepo mchezo mchafu wa baadhi ya Makampuni au wafanyakazi wao wanaosimamia uundwaji, utoaji na usimamizi wa Huduma za Mabando kwa wateja.

Kwa lalamiko hili mimi binafsi ni Shahidi kwani siku hizi imekuwa ni jambo la kushangaza MBs za elfu 50 ambazo nilikuwa nazitumia mwaka jana au mwanzo wa mwaka huu kwa matumizi yale yale kwa Simu hii hii kwa sasa zinaisha haraka utafikiri ni MBs za elfu 10.

Mshangao huu Kaka Waziri pia umewapata WaTanzania wengi akiwemo Mwanamitindo wa Kimataifa kutoka Tanzania, Flaviana Matata ambapo Novemba 10, 2022 naye amelalamikia adha hii kupitia Ukurasa wake wa Twitter nanukuu:

"Bundle ya 50k inaweza isha in 5 days kwa kutumia IG, twitter na emails tu?! Na hapo mtu unatumia wifi nyumbani na ofisini! Hii kali aisee unless simu yangu ina matatizo."

Kaka Waziri,

Bila shaka utaungana nami kwamba Bando sasa sio anasa, Bando sasa ni kama Basic need (hitaji la lazima) la binadamu kama ilivyo maji na chakula kulingana na kiu kubwa ya watu wote na nchi zote duniani kuhitaji kujamiana (socialize), kubadilishana maarifa, kupeana fursa, kupashana habari na hata kutuliza nyoyo zao baada ya mihangaiko ya kila Siku.

Mtu anaweza kuwa elfu mbili akaacha kula mchana, akanunua Bando akafanya mawasiliano akajikuta anapata fedha ya mlo huo wa mchana na hata na mwingine mwezi mzima. Bando sasa ni sawa na chakula.

Kaka Waziri,

Huduma ya bando imekuwa zaidi ya huduma ya kawaida kwa almost kila mtu na makundi yenye raia wengi Nchini, na hivyo hadi niandipo barua hii adha hii ya bando inawakumba wengi kama ifuatavyo (to mention a few).

WANAFUNZI.

Tofauti na miongo ya nyuma, baada ya Nchi yetu kuukaribisha mfumo wa Teknolojia na Habari mwaka 2012 na kuuzima mfumo wa analogia (Analogue Switchoff (ASO), wanafunzi wa ngazi zote za Elimu kuanzia Shule ya Msingi hadi vyuo vikuu nchini wanategemea Bando ili kupata internet kwa malengo ya kupata taarifa, kujibu mitihani na mazoezi wanayopewa na walimu wao darasani. Swali Je, wataweza kumudu gharama hizi kero za Bando kufaulu kwa kila somo? Hatuoni kwamba wataghairi kutumia Bando, au watatumia kwa kiasi na Kukosa kuwa katika ushindani wa kielimu duniani? Na hata kufeli mitihani yao mashuleni? Na hata kuzalisha wanafunzi wasio na maarifa ya kisasa ya kukidhi matakwa ya dunia ya sasa ya kidijitali?

WAFANYABIASHARA.

Kaka Waziri kwa sasa ni dhahiri njia rahisi ya vijana wetu kujiajiri kama ambavyo Serikali yetu pendwa imekuwa ikisisitiza ni kujiajiri katika Mitandao ya Jamii. Ombwe la vijana kufanya biashara mtandaoni ni kubwa na linaongezeka kila uchwao. Na tiketi yao ya biashara ni Bando. Binafsi nimeshuhudia vijana wengi wakiuza nguo, chakula, viatu, vito vya thamani, urembo na hata mboga mboga kupitia mitandao ya kijamii, na wote hawa wanalalamika hali tete kwani kupanda Bando linakwamisha biashara zao.

Siku chache nilitembelea mtandao wa Instagram niliona Binti mmoja mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anayeitwa Jennifer Jovin almaarufu kama Niffer akitumia "Niffer Outfit Store" kama jina la ofisi yake ya kibiashara ya nguo ameandika kwa uchungu sana kuhusu namna kupanda gharama za Bando inavyomkosesha yeye na vijana wa Aina mapato. Niliumia sana. Kaka Waziri tujiulize hawa mabinti warembo akina Niffer wanategemewa na watu wangapi? Na je wakiacha hizo biashara zao watafanya nini kama sio kujihusisha na biashara za miili yao na kufa kwa magonjwa wangali wadogo, na hata kuongeza tatizo la watoto wa mtaani?

ONLINE TVs, BLOGS.

Kaka Waziri, kwa sasa hakuna mjadala kwamba njia rahisi, ya uhakika na ya haraka ya umma wa WaTanzania na hata dunia ya kupata taarifa muhimu ni kupitia vyombo vya habari vya mtandaoni hususani ONLINE TVs. Tanzania hadi kufikia May 2021 kwa mujibu wa Hotuba ya Rais Samia tuna online TVs 451 na Blogs 122.

Na kwa hakika ukitafiti roughly tu utabaini wamiliki wa vyombo hivi zaidi ya 80% ni vijana walioamua kujiajiri na kuajiri wenzao humo.

Hizi online TVs zote zinategemea Bando kuhabarisha umma, tena habari ambazo nyingi sio matangazo ya kulipwa bali habari za matukio ya kijamii, shughuli za kiserikali. Tujiulize huyu kijana ataweza ku-post video YouTube kwa mfano ya tukio la maafa ya ajali ya ndege ziwani Victoria Bukoba kama Bando shida kwake? Na akiweza ataweka video ngapi kwa siku ili angalau mwisho wa mwezi naye apate kulipwa "chochote kitu" na YouTube akidhi mahitaji yake ya kila siku?

WASANII

Wasanii wote nchini wawe waimbaji, waigizaji, wachoraji ama wachekeshaji kwa sasa palio lao Kuu la kuuza bidhaa zao kwa Umma ni mitandao ya kijamii. Mathani wanamuziki, ili wapate kulipwa na YouTube ni lazima wajiunge Bando na kutupia nyimbo zao na matamasha yao huko, Sasa watawekaje kama Bando ghali?

Na Hawahawa wasanii licha ya kutuburudisha ndio wanaoongoza kulipa kodi kwa Serikali, mfano mwishoni mwa mwaka 2021 Mwanamziki Diamond alisikika kwenye vyombo ya Habari kutumia Bilioni 1.7 kwa mwaka kulipa kodi Serikalini kupitia muziki wake, je tukimshushia ari ya kupost vitu kisa Bando hatuoni tunaikosesha Nchi mapato? Vijana wenzake aliowaajiri pale kwenye kampuni yake ya WASAFI je atawalipaje?

WANANCHI KWA UJUMLA.

Kwa takwimu za Serikali yetu ya Tanzania watumiaji wa internet hadi kufikia Aprili 2021 walikuwa wapatao 29,071,817 hawa ndio wanategemewa na wenzao wote wanaofanya biashara mtandaoni kununua bidhaa zao yaani akina Diamond, je tujiulize watawezaje kutazama hizo nyimbo YouTube au Instagram mathalani kama Bando ni kikwazo? Matokeo yake wasanii watakosa subscribers na views na hatimaye kukosa kipato.

Lakini pia hawa wananchi kutokana na Sera yetu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya mwaka 2016, Sheria ya huduma ya vyombo vya habari ya mwaka 2016 na hata Katiba yetu ibara ya 18 hadi 21 wana haki ya kutoa maoni na kuwasiliana na wenzao duniani. Hivyo Bando linawahujumu.

Na mbaya zaidi lawama za makundi haya yote zinaelekezwa kwa Rais wetu kipenzi Mama Samia Suluhu Hassani , Waziri wetu wa Habari Nape na Chama cha Mapinduzi badala ya ukweli kwamba tatizo kuu ni Watoa huduma (Makampuni ya Simu) ambayo almost ni SEKTA BINAFSI ambayo yamekazana kupandisha gharama za Bando bila kujali kelele za wananchi licha ya kwamba Serikali hadi sasa imejitahidi kuyawekea mazingira mazuri ya Biashara na Uwekezaji, na wala hakuna tozo ama kodi mpya yamechajiwa hayo Makampuni.

Na Ni kweli kabisa sisi walaji tuna fursa ya kuchagua vifurushi vya Bando tunavyovimudu kwenye menu; na ni kweli Makampuni ya Simu ndio yana Uhuru wa kutupangia ili kupata faida. Kaka Waziri tuwe wakweli Uhuru wa Makampuni haya kwa sasa umezidi mipaka, wanaona raha kuvuna zaidi bila kujali hali halisi ya vipato vyetu.

Makampuni haya yanachukulia advantage (udhaifu) wa sisi WaTanzania kufurahia na kuhamasika kutumia kwa kasi huduma ya bando kutupandishia gharama za Mabando watakavyo kwakuwa wanajua watumiaji wa Internet sasa ni wengi na wanazidi kuwa wengi na maisha yetu sasa yapo kwenye ulimwengu wa kidijitali. HUU NI UNYONYAJI NA UKATILI.

Kaka Waziri kwa kuwa wananchi karibu wote wanalalamikia adha hii, na kwakuwa Serikali yetu ya Chama cha Mapinduzi CCM ndiye Msimamizi Mkuu CHIEF REGULATOR (Msimamizi Mkuu) na COMFORTER IN CHIEF (Mfariji wao Mkuu),

Na kwakuwa Ilani ya Chama chetu cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2020 - 2025 imetilia mkazo sekta ya TEHAMA katika sura ya 4 (61) (e) nanukuu:

"Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, sekta ya mawasiliano itajikita
zaidi katika kuimarisha ubora wa mawasiliano nchini na kuhakikisha
wigo wa mawasiliano unaongezeka na kuwafikia wananchi wote. Katika
kufikia lengo hilo, Chama Cha Mapinduzi kitahakikisha Serikali yake
inatekeleza yafuatayo:-

(e) Kubuni na kutekeleza mikakati ya kuweka mazingira bora ya
ushindani na udhibiti katika sekta ya mawasiliano ili wananchi wengi
zaidi wamudu gharama za mawasiliano;"

Na kwakuwa Serikali yetu SIKIVU ya Chama cha Mapinduzi CCM ni Serikali ya Kidemokrasia iliyotokana na watu, ipo kwa ajili ya watu wake na inaendeshwa na watu wake kama alivyowahi kusema Rais wa awamu ya 16 wa Marekani, Abraham Lincoln: Democracy is a government of the people, by the people and for the people,

Hivyo kwa kuepusha Serikali yetu SIKIVU inayoongozwa na Rais makini aliyejaa upendo, Rais Samia Suluhu Hassan kupakwa matope kwamba haishughuliki na vilio vya wananchi wake, na pia kuepusha dhana potofu ambazo zimeanza kusemwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba eti Kaka Nape wewe binafsi kama Waziri husika wa Habari pamoja na Serikali yetu mnakula njama na Makampuni ya simu kujipatia faida nyuma ya pazia kupitia Mabando haya yasiyohimilika;

Hivyo napendekeza hatua zifuatazo zichukuliwe na Serikali pamoja na Makampuni ya simu na wananchi kwa ujumla ili kilio hiki cha Bando kifutike na kuwapata Uhuru na haki wananchi kufaidika na teknolojia ya Habari na Mawasiliano kupitia huduma ya bando;

1) Sera ya Taifa ya TEHAMA ya 2016 itathiminiwe upya, kwamba bado inakidhi matwakwa ya sasa ya ukuaji wa TEHAMA nchini na duniani? Watoa huduma wa Habari na Mawasiliano wanaifuata ipasavyo? Hivyo kama kuna marekebisho yafanywe ama ianzishwe Sera nyingine mpya ya TEHAMA mujarabu.

2) Kwakuwa kilio hiki cha Bando kimekuwa kikubwa na cha muda mrefu sasa, na Makampuni ya simu hayaoneshi dalili ya kujali walaji wa Huduma zao za Bando, na kwa sasa Bando ni Huduma ya Msingi ya Kila Mtanzania iwe 'directly' ama 'indirectly'; Serikali kama REGULATOR:-

a) Ichukue hatua za udharura kuweka BEI ELEKEZI kwa Mabando kulingana na unyeti wa mabando uliopo.

b) Ibadili kanuni/utaratibu uliopo wa kusubiri miaka mitano wa kufanya tathimini ya huduma za mawasiliano angalau review iwe kila mwaka kwani mageuzi ya TEHAMA ni makubwa mno kila uchwao, tukisubiri miaka mitano tutajikuta mabadiliko mengi yametokea, uonevu mwingi umefanyika kwa wananchi wetu.

3) Serikali iongoze uthibiti kwa Makampuni ya Simu ili yafuate Sheria na Sera ya TEHAMA, Katiba na miongozo ya Serikali, na makubaliano mbalimbali yanayolenga kuwapatia wananchi huduma za uhakika, uwazi, uadilifu, na nafuu za mawasiliano ili kuepusha mianya ya utapeli, unyonyaji na kutosikilizwa walaji ambao wengi wao ni wananchi wa kipato cha chini.

4) Serikali yetu pendwa iendelee kutekeleza Ilani ya Chama chake Tawala, CCM ya 2020-2025 ambayo katika Sura ya 4 (61) imeelekeza Serikali yake ihakikishe wananchi wote wanapata huduma za mawasiliano kwa gharama zinazomithilika.

5) Makampuni ya Simu tunayashukuru kwa kutuletea huduma ya bando na huduma zingine za mawasiliano, ila yachukue hatua zifuatazo za makusudi kutibu tatizo hili la kupanda Bando kwani wapo hapo kwasababu ya walaji hawahawa wanaolia kutwa kupanda kwa bando:-

a) Yaweke mfumo au utaribu thabiti wa kusikiliza malalamiko ya walaji wa bidhaa zao. Kwa utafiti wangu usio rasmi, Makampuni haya yanatumia zaidi Top to bottom governance tu, ambayo viongozi wa juu huwa na kazi ya kutoa maagizo tu kwa viongozi ama wafanyakazi wa ngazi ya chini, na wafanyakazi wa chini mathalani Customer Care/Call Center ama Branches ndio usiku na mchana hupokea malalamiko ya kupanda Bando na vifurushi vingine, ila kuna kila dalili wakisema juu, juu hawafanyii kazi. Wajisahihishe wajali Bottom to Top governance.

b) Makampuni ya Simu yabuni mkakati mpya rafiki uliojaa utu wa kupanga bei za Bando na vifurushi vingine, huu wa sasa wa kubadilikabadilika, mara washushe mara wapandishe gharama, si tu unatia kinyaa wateja bali unawasumbua na kujipotezea wateja mamilioni kwa mamilioni bila sababu. Inashangaza kuona Makampuni karibu yote ya simu hayana "customer parenting", mtu unakuwa Mteja mzuri (LOYAL CUSTOMER) wa bidhaa zao badala wakulee kwa hata kukupa discounts na OFA mbalimbali, wao ndio kwanza wakiona unanunua zaidi huduma zao ndio wanakupandishia gharama za vifurushi na kama kulikuwa na OFA nazo zinaondolewa. Too terrible.

C) Makampuni ya Simu watathimini upya uaminifu wao kwa wateja. Wawatathimini wafanyakazi wao wanaosimamia utoaji wa Huduma za mawasiliano, ni kweli waaminifu? Au ndio wao hao wanatuaminisha kifurushi kinauzwa 2000 kina MBs 800, Mteja akinunua wanacheza na TEHAMA kupunguza MBs kadhaa bila Mteja kujua? Au ndio kama wale wa majuzi walioweka mabango ya zamani kumbe bei zimebadilika na kuwarubuni wateja kwa maslahi yao? Biashara bila uaminifu na uadilifu ni ujambazi kama ujambazi mwingine.

d) Makampuni ya Simu wawe wabunifu wa miradi au program mbalimbali halali na rafiki za kujiongezea faida. Wabuni bidhaa mbadala za kutosha kuliko kuweka nguvu na macho yote kwenye kupandisha Mabando tu.

6) Wananchi kama walaji wakuu wa Huduma za Bando, vifurushi vingine na huduma zinginezo za mawasiliano tuwe na Umoja, tuelimishwe na wenyewe tupambane kujielimisha haki zetu za habari na Mawasiliano. Tuiambie Serikali kama REGULATOR, tukionewa na Makampuni haya, na bahati nzuri tuna Serikali SIKIVU, itatusikia. Tuache migawanyiko kwenye masuala ya sisi wote kama hili la Bando kwa kigezo cha kwamba eti akilalamika Suphian wa CCM au Hilda wa CHADEMA, au mkiristo au Msomi au mzee au mwanamke siungi mkono. Tuichuje hoja yake, kama ni hoja ya msingi tumuunge mkono, hii ni Nchi yetu sote.

ANGALIZO

Tusipothibiti mapema hali hii ya bando na vifurushi vingine kupanda gharama bila utaratibu wala kujali vilio vya walaji wake kuna hatari mbeleni yafuatayo kutokea.

1) Wananchi watakuwa conservative watarudi kwenye analogy automatically, kakundi kadogo tu cha watu wanaojiweza kimapato ndicho katabaki kanatumia internet. Ieleweke Jamii yetu ni (price player), wengi huangalia penye unafuu hata katika maisha ya kawaida mtu yupo radhi kwenda mtaa wa 7 kununua kiberiti cha 100 kama mtaani kwake kinauzwa 200.

Wananchi wataachana na spidi ya TEHAMA duniani, watachagua njia yao nyingine ya mawasiliano hata kama ya kutumiana barua kama enzi zile za 90s. Sasaivi I'm sure kuna lundo la watu wameanza kuingia mtandaoni kwa mwendo wa kinyonga, kama alikuwa anaingia wiki nzima, Sasa kwa wiki anaingia mara 2 ama 3 tu.. Tusisubiri mtu wa namna hii aache kabisa kutumia internet.

2) Biashara hususani za mtandaoni zitafungwa, watu hawatajiajiri, watu watarudi kuilalamikia Serikali, na kuilazimu kuipa mzigo mkubwa wa kuajiri na wale wambao hawatapata ajira watajiingiza kwenye vitendo viovu ikiwemo wizi, ujambazi, Wanawake kuuza miili yao na kadhalika.

3) Wananchi watanyimwa haki ya kupata na kutoa taarifa na kuwasiliana kinyume na Sera na Sheria ya TEHAMA, Katiba na makubaliano mbalimbali ya TEHAMA ambayo Nchi yetu imeingia duniani.

4) Tutajikuta kama Nchi tunabaki kama kisiwa hatutakuwa connected na ulimwengu. Mambo mengi ikiwemo fursa tija duniani zitatupita. Tutakuwa Nchi ya Ujima ndani ya dunia ya TEHAMA.

5) Serikali itapata tabu kuwahudumia wananchi wake kupitia e-government; Kama tujuavyo huduma nyingi za Serikali kwa sasa zinamtaka mwanachi atembelee mitandao ya kijamii.

6) Wananchi watakosa imani na chama chetu pendwa cha Mapinduzi na Serikali yake, na kuwapa fursa ya kusemwa vibaya na vyama vingine rafiki nyakati za Uchaguzi.

Kaka Waziri,

Naomba kuwakilisha. Natumaini maoni yangu yatafanyiwa kazi kwa manufaa ya Wananchi wetu, Serikali yetu, Chama chetu Tawala, CCM na Taifa letu.

Suphian Juma Nkuwi,
Singida,
Mwanachama kindakindaki wa CCM,
Novemba 12, 2022
Email: yessuphian@gmail.com
Phone: 0717027973

IMG_20221112_091002_309.jpg
 
Sijasoma gazeti lako,lakini kichwa cha gazeti lako kinaonyesha maumivu makali kwako, tunavo sema sisi mnasema hatuna jema na kulinganisha na nchi zingine kuwa tz kunabei ndogo
 
Unakosea mahala.

Sa100 ana uwezo wa kumtimua au kumwacha pena na hafanyi hivyo.

Ni dhahiri,vsa100 anawahujumu wananchi nape akitumika kimkakati.
 
View attachment 2414149
Umeamua utoke kulilia Twitter sasa uje na huku. Mambo yakienda kombo hata ninyi mnaoona serikali ni malaika huwa haikosei mtalia tu.
 
Na Kupanda Hali ya Maisha, Kila kitu bei Juu..., Utendaji haueleweki ni Nani anayewahujumu Watanzania na tupeleke lawama zetu kwa nani ?

Ukiangalia sana humo ndani wote ni wale wale tu...
 
Umeamua utoke kulilia Twitter sasa uje na huku. Mambo yakienda kombo hata ninyi mnaoona serikali ni malaika huwa haikosei mtalia tu.
Tunawalipa ili wasifanye makosa, makosa yakiwa mengi wakae kando, Hakuna aliyewalazimisha kukaa hapo...
 
Ndio mkome na nyie huyo kaka yako anatetea na kuropokwa kama mwakilishi wa makampuni ya simu, ni aibu sana majibu hovyo na usaliti juu
 
Wanakopa kiwango kikubwa zaidi ya uwezo wa kulipa Kutoka vyanzo vya makusanyo ya ndani ambayo haizidi bil 800 Kwa mwezi.

Kinachofanyika, wanaongeza deni Ili deni litumike kulipa deni la nyuma na riba zake.

Familia imekuwa kama mwalimu, akidaiwa huku, anahamia Benki ingine anakopa Ili kulipa deni la Benki ingine, wakati huo huo anaangalia wapi pengine anaweza kopa kuhamisha deni.

Mbaya kuliko yote, anayeenda kutukopea siye atakayelipa.

Anakopa na kwenda kujenga UKWENI.

Unaweza ona hatojali hata kama Nchi itapigwa mnada.

Ni dhahiri, HATOGOMBEA.

Anachukua chake mapema.

Ameeeen.
 
NAPE na mama yao wote lao ni moja.....kwa upande wangu mm mbunge wa JIMBO langu asitegemee kurudi bungeni kwa kweli na kile kichwa chake kama bakuri
 
Nape amefeli vibaya kusimamia maslahi ya wananchi kwenye mashirika ya simu. Kauli anazoibuka nazo ni za kusimama na makampuni ya simu na siasa zaidi.

Hata kama ccm inanufaika na kampuni za simu lakini wanachi tunahitaji huduma nzuri kwa gharama nafuu.
 
....nilitembelea mtandao wa Instagram niliona Binti mmoja mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anayeitwa Jennifer Jovin almaarufu kama Niffer akitumia "Niffer Outfit Store" kama jina la ofisi yake ya kibiashara ya nguo ameandika kwa uchungu sana kuhusu namna kupanda gharama za Bando inavyomkosesha yeye na vijana wa Aina mapato. Niliumia sana. Kaka Waziri tujiulize hawa mabinti warembo akina Niffer wanategemewa na watu wangapi? Na je wakiacha hizo biashara zao watafanya nini kama sio kujihusisha na biashara za miili yao na kufa kwa magonjwa wangali wadogo, na hata kuongeza tatizo la watoto wa mtaani?
Ukweli mchungu !
Ila sikio la kufa halisikii dawa🙄
Nape Nnauye
 
First Mh Nape Is useless for this(for this), I am afraid I have to say this. Anaelewa kinachozungumzwa lakini he is dodging it. Of course, we know that bundles are services regulated by providers and the authorities have little to do with it. What I would like to hear from him is :
1. Akiwa kama kiongozi wa wizara kuwashirikisha wadau na watoa huduma juu ya malalamiko ya watumiaji na kwanini kiasi kipungue tofauti na hapo nyuma ? .
2. Akiwa kama kiongozi wamechukua hatua gani kuhakikisha kuna ushindani unaoletwa na TTCL katika kutoa huduma dhidi ya taasisi nyingine binafsi, mlengo mkubwa wa taasisi za serikali ni katika kuihudumia jamii na dhamira hii isifichwe na shauku ya kuvimba kutoa gawio kubwa kwa serikali.
3. Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) imekuwa chagizo kuwa kwa nchi zilipiga hatua kwenda katika uchumi wa awali na kati, yeye atueleze akiwa kama waziri anadhani kwa upatikanaji huu wa mtandao ambao ndio nyenzo kuu je TEHAMA itakua na mchango wowote katika uchumi wetu?, hapa niweke sawa, nadhani hii inaoneka sawa pia sababu taasisi za serikali wako na fiber za ttcl kwaajili ya shuhuli za serikali na hakuna wasi kabisa lakini je wananchi ambao ndio wachumi wakuu wanapata mtandao kwa uhakika ? . Mitandao ya kijamii kama Instagram imekuwa mama katika mauzo na matangazo,wapo wanatangaza insta tu na wanauza mjini ni kwasababu huko ndiko walipo wateja.

Pia kama nakuwa muwazi basi namuomba Mh Nape kwanza aache kuwa defensive kwani hili swala sio lakwake personal, ni swala la kuwashirikisha na kuwashawishi watoa huduma (ni sawa na baba kumshauri mwanae, kuna uwezekano mkubwa akapokea).

Pia watumiaji hawajali juu ya serikali kuwa na mamlaka kisheria ya kuhoji ma bando, ila kama angelifanikiwa kuwashawishi basi angeli pongezwa sana.

Na mwisho TTCL, hii ndio nafasi ya kusimama na wengi na kujiimarisha, the good thing about selling the same product in the same place with the same quality is that once one get low others have two choices GETTING LOW TOO TO COMPETE OR REMAIN HING FOR NOTHING.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom