Waziri Nape achana na Blaa blaa za siasa; Jenga shule moja ya michezo tukukumbuke miaka 100

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,179
7,330
Inajulikana kuwa wapo watu wengi waliowahi kuwa mawaziri serikalini kwa miaka mingi lakini lakini leo hakuna kinachoonekana cha kuwakumbuka. Wapo wachache waliofanya mambo watakayokumbukwa daima.

Leo naanza na Nape. Najua una mipango yako lakini unaonaje ukaongeza huu kama haupo. Anzisha mpango wa serikali kulea kwa namna maalumu vijana wenye vipaji vya michezo na utamaduni. Lengo ni kuwezesha miaka angalau mitano ijayo vijana wasiopungua 20 wanapata fursa za ajira za michezo nje ya nchi kwa mwaka. Lakini pia vijana wasiopungua 50 kila mwaka wapate nafasi ya kuitangaza Tanzania huko nje

Inasikitisha sana pamoja na vivutio vya utalii tulivyo navyo, Tanzania inafahamika kidogo sana huko nje ukilinganisha na nchi kama Kenya. Yaani kwa wastani ni kuwa ratio ya watu wanaoijua Kenya kwa wanaoijua Tz huko nje ni 100:1. Wengi wanaifahamu Kenya kutokana na uwakilishi wao kwenye michezo pamoja na sababu nyingine

Kwa hiyo basi namshauri Nape aanzishe mradi wa shule kubwa ya serikali ya michezo kwa ajili ya kutambua, kulea na kukuza vipaji vya michezo na utamaduni hapa nchini. Shule hiyo ambayo itakuwa mojawapo ya shule za serikali isiwe tena chini ya wizara ya elimu, bali chini ya wizara inayohusika na michezo na utamaduni. Iwe na kidato cha kwanza hadi cha sita, na wanafunzi angalau 100 kila kidato.

Ipokee wanafunzi wanafunzi toka nchi nzima walioonekana kuwa na vipaji vya michezo. Ili kufanikisha upatikanaji wa wanafunzi wanaostahili, serikali iwe na shule wakala (shule ya serikali) kila mkoa ambazo ingawa zitakuwa shule za kawaida chini ya wizara ya elimu ziwe na programu ya kusaka vipaji mikoani humo na watakaoonekana wanafaa waingizwe kwa masharti nafuu. Then wanafunzi hao "wauzwe" kwa shule ya michezo ya taifa, na kila mwanafunzi anayekidhi viwango na kuchukuliwa na shule ya taifa ya michezo, shule wakala ipewe kiasi fulani cha hela. Hii itahamasisha shule wakala kusaka vipaji vya kweli kutoka mikoani (Nimeelezea kwa ufupi sana jinsi plan inavyoweza kuwa).

Wanafunzi wenye vipaji vya utamaduni kama kuimba nk, watumike kufanya ziara za kutangaza nchi sehemu mbalimbali duniani. Hili linaweza kurahisishwa kwa wizara kuwa saidia kupata scholarships za kusoma nje, ambapo wakiwa huko program maalumu zinaweza kuanzishwa wakawa wanafanya matamasha nk.

Shule hiyo ya michezo iwe na viwanja vya kutosha vyenye viwango vinavyofaa, pia vifaa vingine vya kujifunza michezo na utamaduni kama gym, theatre za muziki, nk. Wanafunzi wapewe lishe bora pamoja na vifaa va michezo kama viatu na mipira. Kuwe na walimu proffesional wa kutosha kwa michezo itakayokuwa inakuzwa.
Mpango kama huu unaweza kuigharimu serikali takribani shilingi bilioni 10 hadi 20 kwa mwaka, lakini nina uhakika faida yake kwa miaka michache ijayo katika kukuza utalii na vijana wetu kucheza nje ya nchi ni fedha nyingi sana zaidi ya hapo. Hapo hatujaongelea kuimarika kwa timu za taifa na sekta ya burudani kwa ujumla nchini.
 
I wish angekuwa kama ulivyoandika,lakini anafikiria namna gani atazuia watu kuhoji namna serikali inavyofanya mambo yake au kujipa ujiko pale Samata mwingine atakapojitokeza
 
Back
Top Bottom