Waziri na Wizara ya Mambo ya Nje wanashindwa majukumu yao: tit fot tat na Kenya

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
92,334
2,000
Ccm hoyeeeee
Yanayoendelea katika mahusiano kati ya Kenya na Tanzania kwa sasa hivi hanasikitisha. Kenya ni jirani yetu na jirani ni ndugu.

Hivyo basi, matukio matatu ya haraka haraka yaliyotokea yanatushangaza. Kwanza ndege ya ujumbe wa Kenya ili rudi au kurudishwa Nairobi hivi majuzi.

Ndege hii ilikuwa na ujumbe wa viongozi waliokuwa wanakuja kuaga na kuhani msiba wa Mzee Mkapa.

Pili, Kenya iliondoa ukaribisho kwa Watanzania, kati ya nchi nyingi, kwenda Kenya ati kutokana na janga la Korona.

Tatu, leo Tanzania kwa kulipiza kisasi imeondoa ruksa ya ndege za Kenya, KQ kutua Tanzania toka tarehe 1 Agosti, yaani kesho.

Sasa hapa napata wasi wasi juu ya ukaribu na mfululizo wa matukio haya.

Je, hakuna hotline kati ya wizara za nje kati ya Kenya na Tanzania?

Kweli watu wanafanya kazi zao kwa weledi hadi mambo yatokee hadharani na kuzivunjia heshima nchi zote mbili?

Mimi nayachukulia masuala haya kama failure in Diplomacy, na watu inabidi wawajibishwe.
 

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
6,816
2,000
Hongereni sana kwa kuendelea na wimbo wa zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa chama
Against all odds tutayamaliza matatizo na Kenya kistaarabu.
Tusiwe kama fisi anayesubiri kudandaoka kwa mkono wa binadamu akifikiria ni nyama itakayo dondoka wakati wowote.
 

Chesty

JF-Expert Member
Aug 30, 2009
5,617
2,000
Kiufupi mgogoro wa kiuchumi kati ya Kenya na Tanzania ni wa muda mrefu sana japo wamekuwa wakijitahidi kuufukia ila unaibuka tena, kibaya zaidi Wakenya wanahofu sana juu ya Tanzania kuwavuta nyuma ki uchumi na Tanzania kuwa mbele ya Kenya na hapa ndipo ukweli umelala. Yote tisa la kumi wahakikishe hii migogoro inafutika, kwani sote kuna kiasi tunategemeana.
Itachukua muda mrefu sana Tanzania kuikuta Kenya kiuchumi. Kitendo cha kuwa mabepari tangu mwanzo kimewafaidisha zaidi kuliko sisi wakomunisti.
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
92,334
2,000
Against all odds tutayamaliza matatizo na Kenya kistaarabu.
Tusiwe kama fisi anayesubiri kudandaoka kwa mkono wa binadamu akifikiria ni nyama itakayo dondoka wakati wowote.
Tulishauri sana juu ya hiyo issue inavyochukuliwa lkn mkatuona kuwa ni kuwaoneeni wivu kisa ni wapinzani.

Hilo suala msipo lichukulia kwa akili kubwa au kwa mihemuko mtajikuta mnaliingiza taifa kwenye mgogoro mkubwa.
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
6,934
2,000
Tanzania exports, imports and trade balance By Country. In 2018, Tanzania major trading partner countries for exports were Rwanda, Kenya, Congo, Dem. Rep., Zambia and Uganda and for imports they were China, India, United Arab Emirates, Saudi Arabia and South Africa.
Main Partner Countries
Main Customers
(% of Exports)
2018
Rwanda18.7%
Kenya9.2%
Zambia7.3%
Uganda5.3%
United States4.1%
See More Countries55.4%
https://www.nordeatrade.com/en/explore-new-market/tanzania/trade-profile
'Jidu', nashukuru sana kwa ushahidi huu uliouweka hapa, pamoja na kwamba sikuwahi kuuona mahali popote.

Mkuu, Nakataa. Nitajaribu kutafura ushahidi mbadala ya huu wenye uwezekano angalau kidogo.

Tatizo la nchi yetu, kati ya mengi, ni hili la kutokuwa na takwimu maalum (au hata kama zipo, zinafichwa, hazitolewi) kana kwamba ni siri.

Mfano ni huu uliotumia hapa. Si ingekuwa bora kama hizi takwimu zimetoka Benki Kuu yetu au ile idara yetu yenye siri kubwa na upotoshaji kwa kila kitu. Kurugenzi ya Takwimu!

Ninachokiona kwenye tarakimu ulizoweka hapa, hasa kuhusu, Rwanda, biashara yetu na wao ni 'Re-export' tu ya vitu kama mafuta, na hali ni hivyo hivyo na Zambia na hata Uganda.
 

mtumishiwaleo

Member
May 4, 2020
80
125
Mtema mate
Ndio maana Mkapa aliwaita Marofa na wapumbavu, ukitaka Kabudi aende akawapigie magoti, kwanza wewe bado kinda ungelikuwa umejenga angarau banda ukapakana na jirani mkorofi usingekuwa unayasema haya, diplomacyia inafanyika Kwa mtu anayejielewa sio Kwa vichaa. Wewe imenizuia kuja kwako nawewe usije kwangu basi.
 

mjingamimi

JF-Expert Member
Aug 3, 2015
22,269
2,000
Unapopanda MAWE usitegemee kuvuna MAHINDI.
Huu ndio ushahidi ulionao mkuu 'mjinga wewe'?

Mbona unazidi kujidhalilisha, pamoja na kwamba jina lako linaeleza uhalisia wako?

Pole sana. Hata sijui umesoma hadi darasa la ngapi, lakini najua hata la saba mwenye kujitambua hawezi kuwa mjinga kiasi hiki.
Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
 

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
6,816
2,000
Itachukua muda mrefu sana Tanzania kuikuta Kenya kiuchumi. Kitendo cha kuwa mabepari tangu mwanzo kimewafaidisha zaidi kuliko sisi wakomunisti.
Hatujawahi kuwa communists bali socialists.
Soma uelewe kuna tofauti kubwa kati ya mifumo hiyo miwili.
Kimaendeleo Tanzania inaenda kwa spidi kubwa, na background ya socialism imesaidia sana kupunguza tofauti ya kipato kati ya walio nacho na masikini hohehahe.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom