Waziri na katibu tamisemi wawajibishwe kwa system kucheleweshwa malipo halmashauri? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri na katibu tamisemi wawajibishwe kwa system kucheleweshwa malipo halmashauri?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nchiyangubwana, Aug 2, 2012.

 1. n

  nchiyangubwana Member

  #1
  Aug 2, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuanzia mwaka huu wa fedha 2012/2013 mfumo (system) fedha mapato na malipo ya fedha katika halmashauri unatakiwa uunganishwe na TAMISEMI ili TAMISEMI waweze kuona transactions zinazoendelea halmashauri na kuweza ku control malipo yaliyo nje ya bajeti na kuangalia hali halisi ya mwenendo wa bajeti n.k.


  Jambo hilo ni zuri sana. Lakini suala linalonikera ni muda/timing ya mpango huo mzuri. Nasema timing imekosewa kwani mfumo huo mpaka leo hii haujazaanza kufanya malipo na shughuli za malipo katika halmashauri zimesima kwa muda wa mwezi mmoja sasa. Sasa sijui halmashauri zinajiendeshaje. Halafu itakapofika mwisho wa mwaka halmashauri zitalaumiwa kwa kutotekeleza mpango wake kwa wakati wakati kumbe zilicheleweshwa kwa zaidi ya siku 30 kuanza kuutekeleza na pia ukichanganya na kuchelewa kwa maingizo ya fedha ndo kabisa inakuwa shughuli!


  Swali langu kuu ni kuwa je, kwanini mpango huo usingefanyiwa majaribio mahali katika wilaya chache katika kila mkoa nchini na mwaka huu ndio ungeanza? Hii ingesaidia kuona mapungufu ya mfumo huo na kuchukua hatua za marekebisho marekebisho mapema na pia wilaya zingeanza kufanya maandalizi mapema then tarehe moja july malipo yangeanza haraka.


  Lakini cha kitendo hiki halmashauri ambazo ndio ziko karibu na wananchi zimesimamisha shughuli na zenyewe zinajiendesha kwa kukopakopa hapa na pale mpaka inakuwa kero na inavunja heshima ya serikali na pia imefikia hatua hata kukopeshwa imeshindikana na hii inaweza ikaletea hata fedha za makusanyo ya kila siku kuanza kutumiwa hata kabla hayajaingia kwenye system na kusababisha hoja za ukaguzi. Lakini hoja hizo zikija je, itakuwa haki kwa halmashauri kulaumiwa kwa kujaribu kuokoa situation?


  Mi nnavyojua watendaji walio TAMISEMI wameenda shule vizuri na wanajua suala la planning vizuri. Je, hawakuliona hilo? Embu piga hesabu kwa halmashauri zote hasara iliyopatikana kwa kuchelewesha shughuli za maendeleo. Hasara hiyo hakika ni kubwa sana kwa kiwango cha mabilioni ingawa ukiangali kwa haraka ni kama haionekani lakini ipo na ni kubwa sana! Sasa je, ni kwanini viongozi wakuu wa wizara hiyo wasiwajibike kwa hasara hiyo??

  Poor planning! pooor coordination!! Maamuzi ya kukurupuka ndio yanayoimaliza nchi yetu ukichanganya na mengine. Bunge livalieni njuga suala hili!
   
 2. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #2
  Aug 2, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Naamini ugonjwa wa ufisadi ndio sababu kubwa ya kuingiza Halmashauri kwenye mkenge huu.Kwa nini mratibu wa mifumo ya TEHAMA hapo TAMISEMI hakufanya uchambuzi wa kutosha .Kuna zaidi ya Halmashauri zaidi ya 130 hivi sasa na kuziunga zote mara moja na kubandone previous systems at once ni ujinga.
  Mfano wilaya kama Mafia au Mbinga zi connect kwenye server moja kwa wilaya zote nchini sijui uwezo wake ni mkbuwa kiasi gani. Vema mpango huo ungeanza taratibu kwa wilaya chache au majiji tu na baade kuendelea kuisoma performance yake.Tumejaribu kuonyesha ujinga wetu hadharani.
   
Loading...