waziri na Katibu Mkuu wa Wizara nani mwenye mamlaka na madaraka katika uamuzi na uten

terabojo

JF-Expert Member
Aug 3, 2010
215
45
Wana JF nisaidieni n iweze kuelewa nani kati ya hao anao uwezo wa lutuletee neema kiutendaji na kufanikisha malengo ya wizara husika?? Binafsi ninadhani Katibu Mkuu ndio hasa "engine" ya wizara na kwa umoja wao serikali. Waziri anakuja na kuondoka - wizara ya mabo ya ndani ni kigezo. Je, wewe mwana JF unasemaje?
 
Katibu ni muhimu sana,anaweza kufanya mambo yakaenda haraka pale wizarani.mara nyingi yeye ndiye professional anayejua utendaji kuliko waziri but hatuwezi kusahau umuhimu wa waziri kwani yeye anaweza kuamuru kitu kifanyike,kipi kiwe priority n .k
 
Kwa ufupi tu, waziri ana madaraka ya juu kuliko Katibu mkuu wa wizara, mambo yanaenda hivi, katibu mkuu ana riporti utendaji kazi kwa waziri na waziri anaripoti kwa Rais, Lakini katika majukumu ya kiutendaji yaliyokwisha amuliwa ama kupendekezwa na waziri katibu mkuu huwa ana madaraka ya kuamua jambo kisha kupeleka ripoti kwa bosi wake ambaye ni waziri
 
unasema katibu mkuu anaripoti kwa waziri, waziri kwa rais

waziri mkuu yuko wapi hapo(mkubwa wa mawaziri), pamoja na katibu mkuu kiongozi (mkubwa wa makatibu wakuu)?

kumbuka katibu mkuu wa Masha alivyokuwa anaripoti kwa katibu mkuu kiongozi, Masha akalalamika kwa waziri mkuu
 
Jamaa alimuona Kilaza nini akaamua awe anamruka...
 
Naam wengine wamesema nami naongeza. Katibu Mkuu ni mtendaji Mkuu wizarani. Mawaziri wengine hawapati makatibu walio watendaji yaani wachapa kazi maana wapo makatibu wakuu VILAZA pia hawa wanatakiwa wajue vipau mbele vya wizara zao wapi na namna gani watapata resources kwa ajili ya kuimplement vipau mbele hivyo etc etc na anatakiwa ampe Waziri wake malengo hayo. Waziri makini atachukua ya katibu Mkuu wake atayafanyia kazi pamoja na ya ziada toka kichwani mwake. Ukipata waziri Kilaza na katibu Mkuu kilaza pia basi kwa kifupi Wizara yote IMEKUFA.
 
Nadhani waziri kazi yake ni WHAT should be done =Sera
Katibu mkuu yeye kazi yake ni HOW and WHO= Utekelezaji

Kisheria resources za wizarai ziko chini ya katibu MkuuKatibu Mkuu ndo mwenye wajibu wa ya Ku hire na ku fire .

Kwam tazamo wangu Ki

  • Ki structure ya Utendaji katibu mkuu yuko juu

  • Ki structure ya Kisiasa Waziri yuko juu
Tatizo naloliona mimi wote hawa ni Presdential appointment. Ingekuwa vizuri hata kama wanakuwa appointed na ofisi ya rais makatibu mkuu wa wizara wakawa apointed after job applicationand interview. Itawafanya makatibu wa wizara kuwa more professional
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom