waziri mwinyi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

waziri mwinyi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Makene, Jul 13, 2011.

 1. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  nafurahishwa na waziri Mwinyi jinsi alivyo makini, mwenye uelewa, stahaa na mwenye kujiandaa.
  Anapojibu maswali anaonyesha uelewa, ukomavu na usikivu.
  Anaweza kujenga hoja bila kutegemea msaada wa kejeli za spika magamba au chorus za ushangiliaji bofu bofu.
  Huyu ndiye waziri ningempa kura yangu awe waziri.
  Nasimama kukosolewa.
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Ukipenda chongo unaona ni makengeza.
   
 3. j

  jakamoyo JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  ni mtazamo wako, unaweza kuwa sahihi au kinyume. Napita tu.
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mbagala, Gongo la Mboto... hivyo ndivyo vipimo stahiki. Niliona alivyoanza kwa kumshukuru mungu kumjalia uzima, more than 50 weren't so lucky kusikiliza hotuba yake na hoja zake makini. Maneno mazuri, ustadi wa kujenga hoja hautarisha uhai wahanga wa mabomu.
   
 5. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135

  "I disagree profoundly with what you are saying but i shall defend unto death your right to say it"-
  Voltaire. Kaka kitu kimoja hakipingiki kuwa jamaa ni msomi na anajitahidi kujenga hoja kwa kiasi fulani but sio leo. Kwa kweli leo kilichofanyika ni ule UTATU USIO MTAKATIFU (UNHOLY TRINITY), baina ya wabunge wa CCM, Naibu Speaker (Mwenyekiti) na Serikali (Waziri).

  Na hii ni stratergy mpya inayotumika ili kupunguza makali ya kambi ya upinzani baada ya kuona wamekabwa koo. Ukiangalia waliokuwa wamejitokeza jioni hii kuhoji baadhi ya mambo kwenye fungu ambalo mshahara wa waziri upo utawaona ZITTO, TUNDU, MDEE pamoja na wengine. But aliyekuwa na hoja (inayojulikana) yenye mashiko ya kutoa shilingi ni ZITTO hasa baada ya mchango wake kujiegemeza kwenye suala la MEREMETA.

  Waziri Mwinyi awali hakujibu suala hilo, sasa Zitto aliamua kusubiri kwenye Mshahara wa Waziri. Kama vile wameambiza, (na kweli waliambiwa) wakajitokeza wachangiaji wengi (wasio na hoja za msingi sana) baada ya fungu husika kufikiwa ili Zitto, Tundu, Mdee wasipate nafasi ya kuchangia na muda uishe. Baada ya hapo ni kupitisha mafungu kama yalivyo. Duh! kwa kanuni hizi Mbona tutalizwa sana. Na in the mean time between time anajitokeza Anne Kilango Kuishauri Serikali isizungumzie Siri za Majeshi ndani ya Bunge. Give me a break! Kweli zipo siri za majeshi ambazohazipaswi kujadiliwa kwenye Public lakini hili la Meremeta sio mojawapo.

  Nahofia UTATU huu unaweza kutumika katika bajeti ya wizara ya NISHATI na MADINI ili kumnusuru Ngeleja kwani kwa mgao huu na kupwaya kwake, haki ikitendeka hatoki. Natoa rai kwa Kambi ya Upinzani nayo Ijipange kimkakati zaidi ili kukwepa hujuma hizi kwani CCM wana karata ya turufu kwa kuwa ni wengi bungeni na wanahodhi kiti cha SPEAKER. Na hapa ndio umuhimu wa Katiba mpya unaonekana- Tunahitaji Speaker asiwe mwanachama wa Chama Chochote ili awe Impartial
   
 6. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #6
  Jul 13, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,583
  Likes Received: 1,675
  Trophy Points: 280
  Alafu anasema kulipuka mabomu ni kawaida, hata juzi cyprus kimenuka, ila anasahau kuwa cyprus waziri wa ulinzi hapohapo alijiuzulu hakutaka kusubirihata uchunguzi.
   
 7. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #7
  Jul 13, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Bila shaka napata picha nzuri yenye uhalisi wa mambo ambayo sikufikiria kabla au kiukweli sikuyajua.
  Nilifikiri pia huyu mwinyi anajitahidi kujiweka sawa bila mawaa kwa mtaji wa 'urahisi' ujao wa z.
  Napenda maoni yenu.
   
 8. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,583
  Likes Received: 1,675
  Trophy Points: 280
  Alafu anasema kulipuka mabomu ni kawaida, hata juzi cyprus kimenuka, ila anasahau kuwa cyprus waziri wa ulinzi hapohapo alijiuzuru hakutaka kusubirihata uchunguzi.
   
Loading...