WAKUU HUU NI UKWELI NA CHANZO NI MIMI MWENYEWE, UKIPENDA PIA WAULIZE JAMES MBATIA, MOSENA NYAMBABE NA WENGINE WALIOKUWA VIONGOZI DARUSO NA ARISO 1989-1992
Mwaka 1991 katika hali ya kushangaza tulipata habari kuwa Rais wa daruso wakati huo Matiko matare amekamatwa na serikali na kuwa alikuwa apelekwe kwenye kambi moja ya JKT, kwa kuwa alijiunga na chuo kikuu bila kupitia JKT kwa mujibu wa sheria. kilichomponza matiko matare ni kuwa yeye alikuwa amejiuinga kwa masomo ya diploma ya ualimu chuo cha ualimu korogwe , kulikuwa na program ya miaka mitatu, miaka 2 ya kwanza unasoma masomo ya sekondari na mmoja uliobaki unasomea ualimu. Matiko aliamua kuacha baada ya miaka miwili ya kwanza na kuamua kujiunga na UDSM
kilichotokea asubuhi siku iliyofuata, Tuliunda kamati na kuamua kwenda kwa aliyekuwa waziri wa elimu sasa marehemu Jakson Makweta. nakumbuka alikuwa anakaa maeneo ambayo kwa sasa nimekuja kujua ndo osterbay, nyuma ya kanisa kuu la St Peter. tulikaribishwa vema uJumbe wetu na tukamweleza waziri kuwa tumekuja kumpongea waziri kwa kumkamata Matiko Matare ili aende jeshini kwa mujibu wa sheria. nakumbuka pia mheshimiwa Mbatia alikuwa sehemu ya ujumbe ule.
waziri alifurahi sana na akatukaribisha chai, na kushukuru kwa jinsi upeo wetu ulivyokuwa juu(mkumbuke kuwa Matiko alikuwa ni mwiba kwa serikali hasa kwa waziri mkuu wa wakati huo matiko Joseph Warioba0. hili nitakuja kuandika makala baadaye yaani mchango wa Matiko Matare katika siasa za mabadiliko katika nchi hii. furaha ya waziri Makweta kwa kuunga mkono kwetu kwa matiko kupelekwa JKT kwa nguvu haikudumu sana, kwani muda mfupi na hasa baada ya kunywa chai ya waziri ilikuja mada ya pili, ni lini Matiko ma angeplekwa JKT? bila shaka waziri akajibu haraka haraka kuwa hata leo leo mkitaka, ndipo lilipofuata swali au ushauri wa marehemu idrisaa kuwa , mheshimiwa waziri umejibu vema na sawa, ila itakuwa vema Matiko Matare akamsubiri Husein Ali Hassan Mwinyi mwananfunzi aliyekuwa anasoma Chuo kikuu cha Uturuki ili wote waende JKT kwa kuwa huyu naye alikuwa amechenga kwenda jeshini kwa mijibu wa sheria. Husein ndo huyu waziri wa ulinzi n JKT na mtoto wa rais Mwinyi ambaye aliamua kwa makusudi kumkwepesha mwanaye kwenda JKT kwa mujibu wa sheria na leo anateuliwa kuwa waziri kusismamia kile alichokwepa na kukikana.
kuna madudu mengi, lakini ndo maana tunasema kila siku kuwa wanaohubiri uzalendo ni wale walioshindwa kuutumikia, anaweza kusimamia JKT aliyoikana mwenyewe na kutorokea uturuki?! tunajua zaidi kuwa hakuwa na passes za kutosha kusoma UDSM kwa kuwa hakufanya vizuri katika masomo yake ya PCB hili atalijibu mwenyewe.