Waziri Mwingine apata ajali.

M

MegaPyne

Guest
Mhe. Daniel Nsanzungwako naibu waziri wa Wizara ya Habari, Michezo na Utamaduni amepata ajali alipokuwa anaelekea arusha kwenye mkutano.

Mhe. Daniel alipata ajali hiyo Kondoa mkoani Dodoma baada ya kugonga kundi la ngombe likikatisha barabara.

Mhe. Daniel na devera wake hawakuumia, ila Gari lake limeharibika vibaya.

Mhe. Daniel alikuwa akielekea jijini arusha kuhuthuria mkutano wakisekta wa Afrika Mashariki kuhusu maswala mbalimbali ikiwemo uandaaji wa kamisheni ya kiswahili na maswala ya utamaduni

Mhe. Daniel amefanikiwa kuendelea na safari yake baada ya kupata Gari ingine.

Habari zaidi, tusubiri magazeti ya kesho. Thats all i have for the day!
 
Sasa inabidi hawa mawaziri wapunguze safari zisizokuwa za lazma- kazi zingine wazifanye wakuu wa mikoa na wilaya!

Kwani Arusha hawezi kwenda kwa ndege? Air tiket is cheaper kulinganisha na kuwa na toka na gari Dodoma au Dar!
 
Mhe. Daniel Nsanzungwako naibu waziri wa Wizara ya Habari, Michezo na Utamaduni amepata ajali alipokuwa anaelekea arusha kwenye mkutano.

Mhe. Daniel alipata ajali hiyo Kondoa mkoani Dodoma baada ya kugonga kundi la ngombe likikatisha barabara.

Mhe. Daniel na devera wake hawakuumia, ila Gari lake limeharibika vibaya.

Mhe. Daniel alikuwa akielekea jijini arusha kuhuthuria mkutano wakisekta wa Afrika Mashariki kuhusu maswala mbalimbali ikiwemo uandaaji wa kamisheni ya kiswahili na maswala ya utamaduni

Mhe. Daniel amefanikiwa kuendelea na safari yake baada ya kupata Gari ingine.

Habari zaidi, tusubiri magazeti ya kesho. Thats all i have for the day!

Kitila na Mzalendo, vipi wakuu?
Quick recovery wakati hawakuumia? Au quick recovery ya shock ya ajali? Au ndiyo kumchulia huko!!!
 
Ng'ombe wangapi wamepoteza maisha katika uzembe wa huyu dereva wa Nswazugwanko??? Huyo waziri pamoja na dereva wake wanatakiwa kutoa fidia kwa huyo mfugaji. Ng'ombe hawawezi kukatisha barabara ghafla, hasa ukizingatia lilikuwa ni kundi la ng'ombe. Dereva alipaswa kuwaona hawa ng'ombe akiwa mbali.

NB: Kama kuna ng'ombe wamepoteza maisha au wameumia. Manake mtoa taarifa hajaweka bayana kuhusu ng'ombe wameumia au wamepoteza maisha.
 
Tanzania tunaweza kutumia ICT kupunguza hizi safari na gharama kibao. Teleconferencing inaweza kuwa ndio solution.

Kila siku viongozi kusafiri lazima kutatokea ajali tu na pia ni gharama mno kwa serikali na familia kutokuwaona wapendwa wao
 
Nasikia na hii pia ilitakiwa auwawe Zitto, sio ng'ombe.....siasa za tunguli.
 
Nasikia na hii pia ilitakiwa auwawe Zitto, sio ng'ombe.....siasa za tunguli.

yawezekana...ha haha haha ha sina mbavu mie..labda tuambiwe na zitto alipita muda gani after ajali...maana bongo hakuishi matukio..full usanii
 
Kitila na Mzalendo, vipi wakuu?
Quick recovery wakati hawakuumia? Au quick recovery ya shock ya ajali? Au ndiyo kumchulia huko!!!

ehee, yaani uzee tena unatunyemelea wengine, basi mwenzako niliposoma tu wamepata ajali, nikajua na habari hii mpaka imewekwa hapa basi ni issue! Sasa kama hawakuumia kulikuwa na haja kweli kuiweka hapa? Watanzania wangapi leo wamepata ajali achilia mbali mshtuko? Jamani tusifanye JF ikawa kama magazeti ya jioni ya Alasiri na Dar Leo, ebo!
 
yawezekana...ha haha haha ha sina mbavu mie..labda tuambiwe na zitto alipita muda gani after ajali...maana bongo hakuishi matukio..full usanii

Mtaalamu, wewe subiri tu utasikia Zitto au Nchimbi wanahusika katika hii ajali ya ng'ombe. Wala husicheke utakaposikia Zitto alikuwa malishoni na hao ng'ombe muda wanapata ajali, au Nchimbi kagombana na Nsanzungwako!!!
 
Kitila na Mzalendo, vipi wakuu?
Quick recovery wakati hawakuumia? Au quick recovery ya shock ya ajali? Au ndiyo kumchulia huko!!!

Sema wewe kaka, watu wanasoma headlines tu au mistari miwili ya kwanza then hao wanakurupuka kutoa maoni...........ukisema, watadai kwamba wao magwiji jamvini na kukuita names tena nasty ones!!!. Haya tutafika tu.
 
oyaa hahahaha acheni vituko wakubwa, yaani iwezekane kuwa kila ajali ya kigogo iwe zitto ahusika??
mie nipo zaidi ya hapo, Inabidi waziri au dereva wake au wote kwa pamoja wajibu tuhuma za kuendesha mwendo kasi. Hii haina tofauti na kwenda msibani kumzika mpendwa aliyetwaliwa kwa ukimwi lakini at same time unaopoa tot hapo hapo msibani (mambo ya kanga). Tumempoteza salome kwa mwendo kasi halafu leo waziri anashindwa kumuongoza dereva (mmoja) kuendesha kwa nidhamu halafu uniambie nimwamini huyo waziri anaiongoza wizara kwa ufanisi.... thubutuuu!!! sintoamini kamwe hiyo. Huu ni uzembe ambapo kama waziri hatoweza kuthaminisha maisha yake awapo na dereva wake, je atatuthamini sie?? Mheshimiwa waziri kuwa makini maana sie tushachoka kulia. Dereva afutwe kazi na waziriapewe onyo kutoka usalama barabarani

unajua waziri akipotea mmoja, atawekwa mwingine ila huyo mpya hatujui njaa yake....
 
ajali hiyo inambnisha serikali itaingia hasara kwa kununua shangingi lingine la million 100,inabidi tusikitike kwanza
 
ajali hiyo inambnisha serikali itaingia hasara kwa kununua shangingi lingine la million 100,inabidi tusikitike kwanza

...ina maana hawana hata insurance kwa gari ya milioni 100nakataa kuamini just for the sake ya kukataa tuu hata kama ni kweli,maana naona milioni nyingine zikilipwa pale kwa muhindi...kazi ipo!
 
Back
Top Bottom