Waziri mwingine anusurika katika ajali ya gari mkoani

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,004
Posted Date::10/9/2007
Waziri mwingine anusurika katika ajali ya gari mkoani
Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi

AJALI za magari zimezidi kuwaandama viongozi wa serikali, baada ya Naibu Waziri wa Afrika Mashariki, Dk Diodarus Kamala, kunusurika baada ya gari aina ya Mitsubishi Prado aliyokuwa akisafiria kuchomoka gurudumu ya mbele.

Tukio hilo limetokea jana mkoani Kagera wakati Dk Kamala akitokea Kata ya Kasambya Kanazi kuelekea Kakunyu na gari hiyo mali ya serikali mkoa wa Kagera.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu kutokea eneo la tukio, Dk Kamala alisema hakupata madhara.

"Tupo Kakunyu, kutokea Kasambya Kanazi, gari lilichomoka gurudumu la mbele lakini nashukuru niko salama," alisema Dk Kamala.

Dk Kamala alisema katika msafara huo alikuwa na watu wengine watatu wakiwemo Benjamin Rwegasira na Raymond Wanai ambao ni waandishi wa habari na dereva ambaye hakumtaja jina na kwamba hakuna aliyejeruhiwa.

Dk Kamala alikwenda Kagera juzi akitokea Mkoa wa Mara, ambako alikuwa katika ziara ya kiserikali kueleza utekelezaji wa falsafa ya maisha bora kwa kila Mtanzania.

Hivi karibuni kumekuwa na ajali zinazokumba viongozi wa serikali, miongoni mwao ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Profesa Juma Kapuya aliyepata ajali mkoani Tabora na Mbunge wa Mchinga, Mudhihir Mudhihir, aliyepata ajali mkoani Lindi iliyosababisha mkono wake kukatwa.
 
Mitsubishi Prado!!?? *Mitsubish Pajero*
 
Back
Top Bottom