Bekabundime
JF-Expert Member
- Aug 6, 2014
- 2,016
- 1,732
Kuna vitu najiuliza sana kama kweli serikali ipo kwa ajili ya wanyonge na masikini, nimemuona WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa nchini Tanzania Mhe. Charles Mwijage ITV, kwenye taarifa ya habari eti anasema hatutaruhusu uwekezaji wa biashara ya mitumba tena, kuanzia sasa hivi.
Ameongeza kwa kusema kuwa 2019 ndio mwisho wa kuonekana mitumba Tanzania
Dah nimejiuliza sana hivi huyu ni Mtanzania kweli? hivi anajua familia za walalahoi wakulima zinaponea wapi? hivi amefika mikoani akaona watoto wa masikini wanaishije na kinachowasitiri ni nini? hivi anajua nguo mpya ya dukani hata yuniform inawashinda masikini kuinunua na wananunua mashati meupe ya mitumba na kuyapunguza ili mtoto avae?
Tukiacha vijijini hapa mjini anajua vijana wangapi wamejiajiri katika Mitumba?
Anataka kutuambia atakapo izuia hii biashara ana mbadala gani, hivi hii Serikali imekuja kwa ajili ya maskini kweli mbona kama kila siku huyu masikini ndio anaezidi kukomolewa?
Jamani wadau nyie mnalionaje hili?