Waziri Mwigulu: Watu milioni 30 wanaofanya miamala ya Sh1 hadi Sh999 kwa siku hawakukatwa tozo ya kutuma na kutoa fedha

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
672
1,000
1630489898001.png
Serikali ya Tanzania imesema watu milioni 30 wanaofanya miamala ya Sh1 hadi Sh999 kwa siku hawakukatwa tozo ya kutuma na kutoa fedha.

Hayo yamesemwa leo Septemba mosi, 2021 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba katika mkutano wake na wanahabari akibainisha kuwa lengo ni kuangalia ustawi wa jamii.

“Tumeachia miamala zaidi ya milioni 29 kwa watu ambao wanatumiana kuanzia shilingi moja mpaka Sh999, watu wanaotumiana viwango vile tuliiachilia yote ile kwa sababu dira ya rais sio kukusanya hela tu anaangalia na ustawi wa jamii, amesema Nchemba.
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
9,655
2,000
Hivi mtu anayetuma Tshs 1 mpaka Tshs999/= Hio pesa anaituma vipi kama hajaweka ?

ili atume hio pesa inabidi aweke na wengi wanaweka elfu 10, 20 au mpaka laki
Hii nchi ina viongozi wenye akili za ajabu, ila huyu Lameck! Nadhani amewazidi wengi kati yao.
 

KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
5,575
2,000
Hii nchi ina viongozi wenye akili za ajabu, ila huyu Lameck! Nadhani amewazidi wengi kati yao.
Sialumu viongozi / wanasiasa sababu najua huo ndio utamaduni wao kudanganya na kupiga propaganda..., ninalaumu watanzania wenzangu kwa kumeza na kuzila hizi propanganda
 

kwitao

Member
Apr 30, 2021
56
125
Waziri, ulitakiwa uwaambie watanzania kwa nini anaetuma pesa anakatwa tozo na anatumiwa wakati wa kutoa anakatwa pia, kama siyo wizi ni nini? Msituibie kwa kisingizio chakuleta maendeleo.

Mwenzenu alituongoza kwa maigizo eti pesa zipo za kutosha, baada ya kifo cha chake miezi miwili tu pesa hakuna! Mnaanza kuwaibia watanzania bila aibu.

Natamani uchaguzi uwe leo na tume iwe huru tuwanyooshe kwenye sanduku la kura.
 

Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
37,526
2,000
Hivi mtu anayetuma Tshs 1 mpaka Tshs999/= Hio pesa anaituma vipi kama hajaweka ?

ili atume hio pesa inabidi aweke na wengi wanaweka elfu 10, 20 au mpaka laki
Sasa wapi ukiweka hela wanakata?,kuweka pesa ni bure mitandao yote
 

Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
37,526
2,000
Daima nitabakia tu na mshangao kwa aliyemteua huyu Waziri! Sijui aliwaza nini!!!
Tatizo mnapinga tu fir the sake of kupinga,hapa anamaanisha unaweza kumtumia bibi yako kijijini hela ya chumvi au mafuta na isikatwe,,au vijijini kwa watu wa chini wanaweza kutumiana hela hiyo kidogo na isikatwe
 

MWANDENDEULE

JF-Expert Member
May 24, 2015
3,089
2,000
CCM ni ile ile. CCM wote ni Ndu-guy wanadanganya mchana kweupe kabisa tena wakiwa wametoa macho mithiri ya yule jamaa wa kujaza Mtera kwa mdomo 🌬️ akiwa anaongea
 

KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
5,575
2,000
Sasa wapi ukiweka hela wanakata?,kuweka pesa ni bure mitandao yote
Ni bure sababu mtandao haukukati pale pale lakini hapo kumbuka wakala analipwa n.k. (kwahio hapo provider anakuwa kama ametoa mkopo ambao in the future utalipwa).

Kumbuka hizi tozo Serikali wameweka kwamba mpaka yule anayeweka pesa anakatwa (even if isipokatwa wakati unaweka ni kwamba mwisho wa siku itakuwa recovered);

Inakuwa taxed kwahio hata huyo mwenye 1 mpaka 999 eventually makato yanampata (Provider anavuta kingi hapo ili aweze kulipia kule ambako haukukatwa theoretically ila practically ulikatwa)
 

May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
4,681
2,000
Ni bure sababu mtandao haukukati pale pale lakini hapo kumbuka wakala analipwa n.k. (kwahio hapo provider anakuwa kama ametoa mkopo ambao in the future utalipwa) Kumbuka hizi tozo Serikali wameweka kwamba mpaka yule anayeweka...
Ina maana Dokta wa uchumi hajui hii?.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom