Waziri Mwigulu: Sijasema fedha za AZAKI ipewe Serikali

Yaani Mimi nimejianzishia kiproject cha kufundisha ufugaji kuku wa kienyeji, nimekiombea hela USAID, wamenipa, kisha serikali inaniambia hizo hela nizipeleke Wizara ya uchukuzi, Kwa ajili ya kununua treni za mwendokasi! Au kununua ndege!! Au kulipia bwawa la Stigler??

Vipaumbele vya hii serikali ni nini??

Wao serikali iombee hela yenyewe Ku deal na hivyo vipaumbele vyake! Siyo kupitia AZAKI, shame!
Huyu Mwigulu nadhani anadhani hizo fedha unaweza badilisha matumizi kama yanavyobadilishaga pale Lumumba kuwapa wapiga kurà T SHIRT ,unaamua wapewe vilemba bila kuangàlia jinsia ya mpokeaji
 
Yaani Mimi nimejianzishia kiproject cha kufundisha ufugaji kuku wa kienyeji, nimekiombea hela USAID, wamenipa, kisha serikali inaniambia hizo hela nizipeleke Wizara ya uchukuzi, Kwa ajili ya kununua treni za mwendokasi! Au kununua ndege!! Au kulipia bwawa la Stigler??

Vipaumbele vya hii serikali ni nini??

Wao serikali iombee hela yenyewe Ku deal na hivyo vipaumbele vyake! Siyo kupitia AZAKI, shame!
Uko sahihi Waziri kajidhalilisha mbele ya USAID waweza hoji hata hiyo PhD yake

Waziri mzima wa fedha na uchumi hajui vitu vidogo kama hivyo kweli
 
Huyu Mwigulu nadhani anadhani hizo fedha unaweza badilisha matumizi kama yanavyobadilishaga pale Lumumba kuwapa wapiga kurà T SHIRT ,unaamua wapewe vilemba bila kuangàlia jinsia ya mpokeaji
Nadhani ni pesa za bajeti ya Serikali unazoweza kuzibadilisha matumizi unavyotaka
 
Kwani zetu?
Tunataka za nini!
Si zimetolewa kuendana na malengo yao?
Kwani maqlengo/vipaumbele vyao ni sawa na serikali?
Mambo mengine aibu tupu!
Mwigulu ange mu consult kwanza Raisi Mama Samia kabla kutoa hiyo Statement kwa USAID

Mama Samia kafanya kazi sana kwenye AZAKI anajua hayo mambo na ndiko aliiinukia

Mama Samia nKabla kuingia siasa alikuwa bosi kwenye moja ya AZAKI Zanzibar
 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amemaliza mkanganyiko wa taarifa kuhusu fedha za USAID na AZAKI ambayo ilionekana kutoeleweka vizuri na baadhi ya vyombo vya habari, wanaharakati na wadau mbalimbali.

Itakumbukwa kuwa juzi akiwa Dodoma alifanya kikao kwa njia ya mtandao na Mkurugenzi wa USAID kuhusu ushirikiano wa Shirika hilo la Marekani la Maendeleo na Serikali ya Tanzania, ambapo alitoa wito au pendekezo kwamba msaada wa fedha takribani Trilioni 3 ambazo USAID imepanga kuipatia Tanzania kupitia Asasi za Kiraia (AZAKI), zielekezwe kwenye miradi ya kipaumbele ya Serikali.

Kwa maneno mengine, Waziri wa Fedha hakumaanisha USAID ichukue fedha inazotaka Kuzipa AZAKI na kuipatia serikali bali AZAKI zitakazopokea fedha hizo izielekeze katika mipango na vipaumbele vya serikali.

Alitolea mfano kwamba katika sekta ya Afya, Serikali inajenga vituo vya afya na zahanati, AZAKI zinaweza kununua vifaa tiba. Kwenye Elimu, wakati serikali inajenga shule na madarasa, AZAKI zinaweza kununua vifaa vya kufundishia kama vile vitabu na mahitaji mengineyo. Hivyo hivyo kwenye sekta za Kilimo, Uvuvi, Mazingira n.k.

Akiambatanisha kipande cha video akiwa anazungumza kwenye mkutano huo na USAID, Waziri Nchemba amemaliza mkanganyiko kwa kuandika:

"Sio Usaid wachukue Fedha walizotaka kuwapa AZAKI na kuipatia Serikali; bali USAID wanaotoa fedha na AZAKI zinazopokea fedha, waelekeze nguvu zao katika miradi inayoendana sanjari na Dira ya Taifa, Mipango na Vipaumbele vya Serikali." Dkt. Mwigulu Nchemba.
---

UFAFANUZI ZAIDI

"Kama Waziri mwenye dhamana ya Fedha nina Wajibu wa kuwaeleza washirika wa Maendeleo kuhusu mifumo yetu ya Bajeti. Ndicho nilifanya katika mazungumzo na USAID. HATUNA NIA YA KUZICHUKUA FEDHA ZINAZOKWENDA KWA AZAKI isipokuwa ufadhili uendane na malengo yetu.

Naziomba AZAKI kuwianisha shughuli zao na malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na Mpango wa Maendeleo wa Miaka 5 ili sote kwa Pamoja, Serikali, Sekta Binafsi na Jamii kupitia CSOs tuvute pamoja katika kuleta Maendeleo ya Nchi yetu. Nawasihi DPs kuongeza Fedha kwa CSOs zetu.

Fedha ambazo washirika wa Maendeleo wanazipeleka moja kwa moja kwa Azaki zinasimamiwa na menejimenti/Bodi za Azaki kwa mujibu wa Sheria ya NGO. Fedha zinazotumiwa na Serikali zinapaswa kufuata Sheria ya Bajeti na Sheria za Fedha za umma. HATUJATAKA FEDHA ZA AZAKI ZIJE HAZINA."

Mwisho wa kunukuu.

Pia, soma=> Waziri Nchemba, ameiomba USAID, kuelekeza msaada wa dola bilioni 1.3, kwenye miradi ya kipaumbele ya Serikali ya Awamu ya Sita
Ni kwanini Marekani inatumia madalali kutoa the so called ‘Aid’?
 
🐒🐒🐒
U8LP.jpg
 
Tr 13 Tshs ni kama usd 5.5 million. Ni hela nyingi.. kama serikali haiwezi kudhibiti zinatolewa kwa nani na kufanya nini hiyo hela inaweza kua na athari kwa nchi.

Kazi yake inaweza kulemaza taifa kuendelea kisaikolojia kua tegemezi.

Pia hizo azaki zinaweza kugeuza hela hizo mradi wao wa kula hela inayokuja kama rushwa ili kuipenda na kuendeleza maslahi ya Marekani nchini.
Una roho ya kimaskini.
 
Back
Top Bottom