Waziri Mwigulu: Serikali imekusanya Tsh Bilioni 63 tozo miamala ya simu, zitajenga vituo vya afya 220 kwenye tarafa

the horse

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
652
441
Toka tozo za miamala ya simu ianze bilioni 63 zimekusanywa na tayari Serikali imeshapeleka fedha kujenga vituo vya afya 220 kwenye tarafa zote zisizokuwa na vituo vya afya kabisa.

Hakuna tarafa yoyote nchi nzima ambayo haitakuwa na kituo cha afya kwasasa. Kodi yetu imeleta matokeo, Watanzania tutembee kifua mbele kwa kujenga nchi yetu wenyewe. - Taarifa hii imetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe Mwigulu Lameck Nchemba "Madelu".

Bwanku M Bwanku

IMG-20210901-WA0019.jpg
 
Biashara za Mobile money zinakufa kila kukicha. Ajira zinapotea. Huku Luku huku mafuta. Mafuta yamepandisha na yanaendelea kupandisha gharama za maisha. We will soon collapse kama tusipokuwa makini. Nyie mdanganyeni tu Mama. By the way, tozo zilikuwepo kabla hata ya Mama na vituo vya afya vilijengwa.
 
Uko sahihi kabisa! Hii biashara kwa sasa imepooza ukilinganisha na zamani.
 
Biashara za Mobile money zinakufa kila kukicha. Ajira zinapotea. Huku Luku huku mafuta. Mafuta yamepandisha na yanaendelea kupandisha gharama za maisha. We will soon collapse kama tusipokuwa makini. Nyie mdanganyeni tu Mama. By the way, tozo zilikuwepo kabla hata ya Mama na vituo vya afya vilijengwa.
Mzee tunakomeshwa balaa
 
Watu wakishakuwa mawaziri wanaona Watanzania wote ni wapumbavu

Projection zao zinasema watakwenda kukusanya 1.2 trillion maana yake kwa wastani ni 100bil kwa mwezi

Wanadai matumizi yapo karibu 90% ya kabla ya tozo, hawasemi kama ni transactions au amounts.

Inakuwaje makusanyo yapo kwenye 40% ya target? Kwa mwendo huu, maana yake watakusanya around 400bil?

Nani atakuja kutueleza ukweli?
 
Kwani budget ya taifa inaangalia chanzo cha mapato ni nini na kupeleka sehemu ya makusanyo hayo kwenye miradi Fulani kama zima moto!? Uharaka wa allocation wote wa nini!? Hii yote si budgetary funds!?
 
Yaani anafurahia makusanyo bila kuangalia athari kwa wale waliojiajiri kupitia sekta hiyo, yaani it worse watu wamepunguza transaction kupitia simu na hivyo Kupunguza ajira ni mchumi gani huyu?
 
Hawa viongozi ni mufilisi kichwani mwao....wameshindwa kuallocate funds ktk rasilimali lukuki tulizonazo wamekimbilia kwetu,ni hatari sana kutugeuza wananchi ndo vyanzo vyao vya mapato bila kututengenezea mazingira mazuri ya kutengeneza fedha katika mizunguko yetu.Kwa lugha nyepesi ni kuwa sisi tumewekwa badala ya madini,bahari ,ardhi na mengineyo ya kutosha kujaza ukurasa wa A4
Kwa hili tuu wataangukia pua
 
Kama projection ya 1.2Trillion ilichakatwa kwa kuangalia miamala ya miaka ya nyuma ina maana miamala imepungua kwa chini ya 50% (chukulia mwezi wa kwanza walipata 43BL badala ya 100BL). Kwa hiyo tusubiri taarifa ya kupungua kwa mapato ya kampuni za simu kwani ile portion yao ya tozo (ukiacha ya serikali) nayo imepungua kwa asilimia hiyo hiyo (50%) na hivyo VAT(18%) itapungua (mapato ambayo hayakupaikana) na mwisho corporate tax pia itapungua. Kwa kuwa transactions zimepungua, watoa huduma (Mawakala) wanafunga huduma zao na kwa hivyo kuathiri ajira binafsi na usalama pia kwani wengine wanaweza kuingia kwenye shughuli za uhalifu.

Kwa kuwa hatuna hesabu ya mapato yatakayopotea kwa kampuni za simu, inashindikana kujua ukubwa wake(magnitude), inawezekana kodi ya serikali itakayopotea ikawa kubwa kuliko hizo 43BL anazojisifia waziri wetu as such ikawa ni kutwanga maji kwenye kinu. Busara itumike kuamua sasa kama wanafahanmu mapato yatakayopotea kwa serikali yatakuwa makubwa kuliko inavyonekana sasa kuwa tozo zina faida kwa serikali. Tuvute subira.
 
Binadamu wa bongo... hamna maana kabisa.
Mmelia lia wee! Hamkutaka jiwe awe Rais..... sawa Mungu kamuondoa lkn bado mnalia tuuuuu!!
Mara tozo
Mara mama sijui kala nini...
Hivi mtuambie mnataka nini?? Mridhike???
Msiposema sasa!! atakuja rugumya hatari...nasema mimi mnastahili.

sometimes nachelea sema jiwe nadhani aliwajua mlivo...kuwa buruza vile alijua mlivo matahaila!!

Yani nyie ni pasua kichwa majinga nyie. Ole wenu nipewe ka uwaziri tu.
Mtakoma nawambia. Naanza na hasa Bongo land..maji mtaita. maa!!

mshukuruni huyo Mama watu wengine hatuonwagi.....wkt wa jiwe nilidhani mko sahihi kuuumbe..wagonjwa nyie??....
 
Biashara za Mobile money zinakufa kila kukicha. Ajira zinapotea. Huku Luku huku mafuta. Mafuta yamepandisha na yanaendelea kupandisha gharama za maisha. We will soon collapse kama tusipokuwa makini. Nyie mdanganyeni tu Mama. By the way, tozo zilikuwepo kabla hata ya Mama na vituo vya afya vilijengwa.
Zife tuu ila tozo ziwepo palepale
 
Toka tozo za miamala ya simu ianze bilioni 63 zimekusanywa na tayari Serikali imeshapeleka fedha kujenga vituo vya afya 220 kwenye tarafa zote zisizokuwa na vituo vya afya kabisa.

Hakuna tarafa yoyote nchi nzima ambayo haitakuwa na kituo cha afya kwasasa. Kodi yetu imeleta matokeo, Watanzania tutembee kifua mbele kwa kujenga nchi yetu wenyewe. - Taarifa hii imetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe Mwigulu Lameck Nchemba "Madelu".

Bwanku M Bwanku

View attachment 1919364
wananchi wamemchapa kofi la uso. kwa miezi miwili 63bil ilhali katika hotuba alitamba kuwa atapata 12tr kwa mwaka yaani kila mwezi 1tr
 
Toka tozo za miamala ya simu ianze bilioni 63 zimekusanywa na tayari Serikali imeshapeleka fedha kujenga vituo vya afya 220 kwenye tarafa zote zisizokuwa na vituo vya afya kabisa.

Hakuna tarafa yoyote nchi nzima ambayo haitakuwa na kituo cha afya kwasasa. Kodi yetu imeleta matokeo, Watanzania tutembee kifua mbele kwa kujenga nchi yetu wenyewe. - Taarifa hii imetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe Mwigulu Lameck Nchemba "Madelu".

Bwanku M Bwanku

View attachment 1919364
Hivi tatizo ni majengo au huduma bora? Hapa nilipo kuna hospitali ya wilaya na ya tarafa lakini ukienda kupata huduma unaambiwa hakuna dawa, unaambiwa dawa kanunuwe pale!
Ushauri wangu ni kwamba ziboresheni kwanza hospitali na vituo vyote vya afya vilivyopo,nikimaanisha madawa nawahudumu wawepo Wa kutosha kabla ya kuongeza vituo vingine!.
 
Kodi zenye matokeo safi Sana, technically wanaopinga haya mambo huwa ni majitu ya mijini ambao wana uhakika wa huduma za afya na usafiri.

Ila ukienda Vijijini kura zote kwa mama.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom