Waziri Mwigulu: Serikali imekusanya Tsh Bilioni 63 tozo miamala ya simu, zitajenga vituo vya afya 220 kwenye tarafa

Navitafuta sana....sivioni. nadhani wajenzi wameenda kujenga porini au wamevificha. Wajenge sehemu ambayo tunaweza vifikia kwa urahisi. Vituo vya afya 220

Waache kumchonganisha Rais na Wananchi, Pia waache kumshauri vibaya.
Hawajajenga ndio wanajidai wametoa hela utafikiri washajenga. Tofauti na magufuli wenye meno wanangoja kula hizo hela. Hapo mama kama kweli ni kitu kimoja na magufuli ahakikishe walaji wanavunjwa meno.
 
Jiwe mwenyewe hao walaji walimshinda sembuse huyu mama?kifupi ccm na ulaji wa pesa za umma ni sawa na samaki na maji?!!ukiwatenganisha tu, kiumbe kimekufa!!mfano hata hiyo kamati iliyoundwa juu ya kupanda bei ya mafuta ni usanii tu, kwani tatizo wanalifahamu kuwani wingi wa tozo walizoweka kwenye kila lita moja ya mafuta ndio inapelekea mafuta kuwa juu hapa nchini!!Sasa wao watakwambia tu ohooo sijui soko la dunia ndio linaamua sisi hatuna la kufanya kweli?!!
 
Navitafuta sana....sivioni. nadhani wajenzi wameenda kujenga porini au wamevificha. Wajenge sehemu ambayo tunaweza vifikia kwa urahisi. Vituo vya afya 220

Waache kumchonganisha Rais na Wananchi, Pia waache kumshauri vibaya.
Hakuna hata kituo kimoja alichojengwa popote pale Tanzania zaidi ya miradi yote inayoonekana kuirithi kutoka kwa mtangulizi wake.
 
Navitafuta sana....sivioni. nadhani wajenzi wameenda kujenga porini au wamevificha. Wajenge sehemu ambayo tunaweza vifikia kwa urahisi. Vituo vya afya 220

Waache kumchonganisha Rais na Wananchi, Pia waache kumshauri vibaya.
Wewe mwepesi kweli mkuu. Tembea Tanzania nzima utaviona hivyo vituo vya afya usishinde nyuma ya keyboard ukategemea kuja kuviona hata sekunde moja.

Sasa Samia anatembea na wazungu, pesa zikipatikana zitaenda kufanyiwa kazi ya maana halafu wewe shujaa wa nyuma ya keyboard utakuja kuuliza pesa zipo wapi!?.
 
Wana Mwenge Jazz Paselepa waliimba, wewe ukisema mke gani we bwana wenzio wanamuona anapeendeza. Hamuoni umuhimu wa hivi vituo SI mpo mjini huduma tele mnabeza tu. Huko vijijini ni faraja kubwa Sana, wananchi wanateseka Sana kwenye hizi huduma muhimu. Mimi nilikuwa kati ya watu tuliombeza Sana Mh. Kikwete, lkn Kuna siku nilipata mgonjwa wa Sukari, alikuwa na hali mbaya Sana, na mjuavyo watu wazima wengi akiwa na Sukari lzm awe na pressure. Tulihangaika Sana Hindu Mandal bila suluhisho. Tulishauriwa tuende Muhimbili, hakuna aliyekuwa na hope na Muhimbili maana wakati ule private zilikuwa na sifa zote.
Muhimbili tulifanikiwa kupata clinic Safi Sana ya Moyo chini ya Dr. Kissenge, alitupa program nzuri Sana ingawa yeye SI dokta wa Sukari lkn aliweza kufanya mgonjwa wetu apate nafuu na Sukari yake ikashuka Sana, akawa Yuko normal. Sasa nikawa nikiona like jengo pale JAKAYA KIKWETE roho inanisuta nabakia kusema mnyonge mnyongeni haki yake mpe.
Mwendokasi nao ile barabara wakati inajengwa duh kelele hapa JF watu wanabeza kila mtu na utaalam wake, lkn hayooo yanapiga kazi though Kuna mapugufu kwenye uendeshaji lkn miundombinu ipo.
Kelele tena zipo kwenye hizi projects kubwa km umeme wa Mwalimu Nyerere kule rufiji watu wanaandika kabsaa hizo ni white elephant projects lakini siku zinakwenda miradi inaelekea ukingoni. Sgr nayo hiyooo! Inachanjq mbuga.
Juzi nimeona kwenye Facebook page ya mheshimiwa Eng. Manyaya kaweka muonekano mpya wa mji wa Mbambabay kule Nyansa, Kwanza full lami, usiku taa zinawaka yaani mji uko byee kabisa. Kwa wale wanaotoka pande hizo waulize Mambo yalikuwaje kabla na Sasa. Sehemu ya kwenda masaa matano unatembea siku mbili. All in all usiibeze serikali hasa inapojenga kule kwenu halafu wewe huna habari nako, hata kibanda Cha kuku hujajenga, tunajiona wa mjini Sana! Wakati wazee wetu wapo huko vijijini wanapata tabu.
Nnachowasihi furahieni hata serikali inawakumbuka kwa maendeleo otherwise nchi inaweza kuwa km Congo au Guinea kila siku mnanyang'anyana madaraka na wajeda!
 
Wewe mwepesi kweli mkuu. Tembea Tanzania nzima utaviona hivyo vituo vya afya usishinde nyuma ya keyboard ukategemea kuja kuviona hata sekunde moja.

Sasa Samia anatembea na wazungu, pesa zikipatikana zitaenda kufanyiwa kazi ya maana halafu wewe shujaa wa nyuma ya keyboard utakuja kuuliza pesa zipo wapi!?.
Hakuna vitu vipya alivyojenga zaidi ya kurithi alivyokuta katika hatua mbalimbali
 
Tembea usipinge usichokijua.
Mimi nafahamu kila mahali na kila wiki natembelea mikoa sio chini ya minne kwa hiyo nina ufahamu mpana sana kuhusi kinachojili huko kwenye mizizi ya wananchi. Rejea yote yaliyokuwa yakitangazwa enzi ya wamu ya tano ndio hayo hayo mnajitapa kwamba mmefanya ndio maana hamuelezei kwa vitendo kwa kuonesha 'live' kile unachokipigia chapuo.

*This is the beginning of the end
 
Endelea kuota mkuu kwa kusema kuwa huu ni mwanzo wa mwisho. Kila siku kwenu huu ni mwisho huku mkizeeka na mvi zikijaa vichwani.
 
Back
Top Bottom