Waziri Mwigulu: Serikali imekusanya Tsh Bilioni 63 tozo miamala ya simu, zitajenga vituo vya afya 220 kwenye tarafa

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
9,065
2,000
Hivi tatizo ni majengo au huduma bora? Hapa nilipo kuna hospitali ya wilaya na ya tarafa lakini ukienda kupata huduma unaambiwa hakuna dawa, unaambiwa dawa kanunuwe pale!
Ushauri wangu ni kwamba ziboresheni kwanza hospitali na vituo vyote vya afya vilivyopo,nikimaanisha madawa nawahudumu wawepo Wa kutosha kabla ya kuongeza vituo vingine!.
Hakuna dawa ni baadhi tuu huwa hazipo hata farmacy huwa hakuna dawa zote.

Shule za kata zilianza kwa majengo na huduma kujikongoja lakini as time goes ziliboreka.

Nyingi ya vituo vya afya vitaanza kwa ajili ya wamama wajawazito, watoto na wagonjwa wa nje,baada ya miaka 3 hivi vitaanza kutoa huduma nzuri zaidi maana vitaletewa wataalamu na majengo yataongezeka kwa ajili ya magonjwa mengineyo.
 
codes

JF-Expert Member
Jan 13, 2015
284
500
The worst goverment and worst finance minister to have ever found....,Nyie mnamkamua mtz kodi kila mahali(mshahara,petrol,miamala,mazao,luku) afu MNATAKA MAMA MWENYE NYUMBA ASIMWACHIE MZIGO WA TOZO ZA LUKU MPANGAJI?!!?....,Hivi Serikali inaujua ujeuri wa wamama wenye nyumba?!...,Eti msinunue umeme kisa Tozo....,"Atawaambia KAENI GIZANI/ONDOENI KABISA METER"...,Dr Mwigulu unakiaibisha chuo ulichosoma....,Yaani kichwani hufikirii alternatives sources of your budget zaidi BIBI ZETU MASKINI WA VIJIJINI/watz maskini??.....,PhD ya jalalani.
Toka tozo za miamala ya simu ianze bilioni 63 zimekusanywa na tayari Serikali imeshapeleka fedha kujenga vituo vya afya 220 kwenye tarafa zote zisizokuwa na vituo vya afya kabisa.

Hakuna tarafa yoyote nchi nzima ambayo haitakuwa na kituo cha afya kwasasa. Kodi yetu imeleta matokeo, Watanzania tutembee kifua mbele kwa kujenga nchi yetu wenyewe. - Taarifa hii imetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe Mwigulu Lameck Nchemba "Madelu".

Bwanku M Bwanku

View attachment 1919364
 
Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
9,065
2,000
Hivi tatizo ni majengo au huduma bora? Hapa nilipo kuna hospitali ya wilaya na ya tarafa lakini ukienda kupata huduma unaambiwa hakuna dawa, unaambiwa dawa kanunuwe pale!
Ushauri wangu ni kwamba ziboresheni kwanza hospitali na vituo vyote vya afya vilivyopo,nikimaanisha madawa nawahudumu wawepo Wa kutosha kabla ya kuongeza vituo vingine!.
Tatizo ni majengo na huduma japo za awali.Kwamba nisafiri km za kutosha kwenda kitafuta huduma tena kwenye barabara mbovu Kisa huduma ziko mbali .

Shule za kata zilianzaje? Tunaanza na majengo ya kuweza kutoa japo huduma za awali afu baada ya mda huduma zote zitapatikana.

Hata famasi hakuna dawa zote Mzee,kwani hapo hospital dawa unapewa bure? Si unanunua tena bei kubwa kuliko maduka ya nje,sema nyie wa bima ndio mnalia Lia Sana lakini sisi wa kulipia hatujawahi ona shida maana hatupewi bore hata ingepatikana hospital.
 
Rogojin The Idiot

JF-Expert Member
Jul 25, 2017
1,965
2,000
Biashara za Mobile money zinakufa kila kukicha. Ajira zinapotea. Huku Luku huku mafuta. Mafuta yamepandisha na yanaendelea kupandisha gharama za maisha. We will soon collapse kama tusipokuwa makini. Nyie mdanganyeni tu Mama. By the way, tozo zilikuwepo kabla hata ya Mama na vituo vya afya vilijengwa.

Halafu baada ya hapo? Nini kinafuatia?
 
Heijah

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,962
2,000
Ukweli nimemsikiliza leo kwa asilimia kubwa mpaka anamaaliza press yake sijamuelewa anaongea nini kweli kabisa. Amekazania vituo vya afya kila tarafa bila kusema athari anazowacha nyuma katika uchumi wa nchi, mara madesk ya shule kweli halmashauri wameshindwa kutatua shida hizi kwa mapato ya ndani wakati kila mwaka tunasikia pesa zimepigwa sana huko. Leo Tanzania baada ya miaka 60 tunategema double taxation kujenga vituo vya afya wakati tuliaminishwa sisi nchi tajiri sana tunapigwa tu. Sector ya mobile money inakuwa wameshaingia kati kuharibu kama walivyofanya huko nyuma kwenye korosho na hapa wataharibu mwisho wa siku watarudi kuzifuta. Mama Samia najuwa huwezi kusoma huu uzi lakini najuwa unafahamu malalamiko ya watu kuhusu hili janga na limewakuta watu wengi wa vyama vyote hili ni doa kubwa sana katika utawala wako toa maamuzi magumu kama Rais wa nchi hii futa sheria hii haraka.
 
Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
9,065
2,000
The worst goverment and worst finance minister to have ever found....,Nyie mnamkamua mtz kodi kila mahali(mshahara,petrol,miamala,mazao,luku) afu MNATAKA MAMA MWENYE NYUMBA ASIMWACHIE MZIGO WA TOZO ZA LUKU MPANGAJI?!!?....,Hivi Serikali inaujua ujeuri wa wamama wenye nyumba?!...,Eti msinunue umeme kisa Tozo....,"Atawaambia KAENI GIZANI/ONDOENI KABISA METER"...,Dr Mwigulu unakiaibisha chuo ulichosoma....,Yaani kichwani hufikirii alternatives sources of your budget zaidi BIBI ZETU MASKINI WA VIJIJINI/watz maskini??.....,PhD ya jalalani.
Magu aliwahi waambia kwamba ataamini maisha ni magumu siku mafundi nguo wakufunga ofisi,baa bombe hainyweki, wanaume mkiacha kuhonga na harusi au saluni za urembo zikiacha kufanyika.

Kama zote hizi zinaendelea ni ujinga tuu kuongea mambo ya hisia zako.Nyie ndio mlikuwa mnasema ooh mawakala watafunga ooh watu watahamia benk na porojo za kijinga nyingi.

Hadi sasa miamala inacheza mulemule na hakuna kilichobadilika.Katungeni uongo mwingine.
 
Ngokoki

Member
Jul 7, 2021
63
125
Hakuna dawa ni baadhi tuu huwa hazipo hata farmacy huwa hakuna dawa zote.

Shule za kata zilianza kwa majengo na huduma kujikongoja lakini as time goes ziliboreka.

Nyingi ya vituo vya afya vitaanza kwa ajili ya wamama wajawazito, watoto na wagonjwa wa nje,baada ya miaka 3 hivi vitaanza kutoa huduma nzuri zaidi maana vitaletewa wataalamu na majengo yataongezeka kwa ajili ya magonjwa mengineyo.
Tatizo lingine ni us
Tatizo ni majengo na huduma japo za awali.Kwamba nisafiri km za kutosha kwenda kitafuta huduma tena kwenye barabara mbovu Kisa huduma ziko mbali .

Shule za kata zilianzaje? Tunaanza na majengo ya kuweza kutoa japo huduma za awali afu baada ya mda huduma zote zitapatikana.

Hata famasi hakuna dawa zote Mzee,kwani hapo hospital dawa unapewa bure? Si unanunua tena bei kubwa kuliko maduka ya nje,sema nyie wa bima ndio mnalia Lia Sana lakini sisi wa kulipia hatujawahi ona shida maana hatupewi bore hata ingepatikana hospital.
Hata yale madawa kidogo yanapoletwa yanaibiwa, unakuta mhudumu wa kituo fulani cha afya anaduka lake la madawa pembeni,dawa zikija anapeleka kwake, sasa Mpaka hapo tutafika? Tafakari!
 
Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
9,065
2,000
Biashara za Mobile money zinakufa kila kukicha. Ajira zinapotea. Huku Luku huku mafuta. Mafuta yamepandisha na yanaendelea kupandisha gharama za maisha. We will soon collapse kama tusipokuwa makini. Nyie mdanganyeni tu Mama. By the way, tozo zilikuwepo kabla hata ya Mama na vituo vya afya vilijengwa.
Unaporopoka uwe unakuja na Takwimu vinginevyo nyie ndio huwa mnashitakiwa kwa ile sheria ya mitandao.

Mbona mimi nakoishi hakuna biashara iliyokufa? Kwa hiyo zinakufa kwenu tuu? Usipende kuropoka.

Toka mumeanza kuropoka hakuna hata kimoja kimwtokea serikali inasoma trend na Mwingulu kasema kabisa kwamba hata kabla ya tozo miamala imekuwa inacheza mule mule average ya mil.9-11 kutokana na mwezi sasa wewe unaeropoka uongo una Nia gani?

Tunawaamini waliosomea fani sio wapuuzi kama wewe wenye milengo ya kisiasa Kisa Mbowe yuko ndani.
 
Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
9,065
2,000
Tatizo lingine ni us

Hata yale madawa kidogo yanapoletwa yanaibiwa, unakuta mhudumu wa kituo fulani cha afya anaduka lake la madawa pembeni,dawa zikija anapeleka kwake, sasa Mpaka hapo tutafika? Tafakari!
Kwa nini hukutoa taarifa kama ulimuona mwizi? Usipolinda mali yako nani akulindie? Kukaa kimya tuu unashiriki wizi na inaonesha hata ungekuwa wewe ungeiba tuu.

Unadhani viongozi wapo kila mahali?
 
Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
7,955
2,000
Kwa hiyo miaka 60 mlikuwa hamjui tozo ndo zitaleta maendeleo nchini.....kama ni kodi zilikuwa zinakusanywa na tozo kwenye bidhaa kibao kama petroli zilikuwepo, au kwa sababu mmeingiza makato kinyemela kwenye miamala ya simu mkayaita tozo ndo sasa maendeleo yanaonekana. Kwa hiyo kimsingi kodi haileti maendeleo, ila tozo ya uzalendo ndo inayoleta maendeleo.

Badala ya kubana matumizi ya serikali mmekazana kuweka tozo kila mahali. Kwa nchi maskini kama Tanzania haiingii akilini serikali nzima kufanya anasa za magari ya kifahari, kutengeneza nafasi za kuteuana zisizo na tija na serikali kugharamika kulipa watu ambao hawazalihi chochote zaidi ya kuzunguka na ma VIIEITE kwa kisingizio cha waheshimiwa.

Kwa nchi zilizoendelea hususan ulaya pamoja na kutoa misaada kwenye nchi maskini hukuti serikali ikigharamia matumizi ya anasa ya magari ya kifahari kwa maofisa wake, binafsi nilishuhudia aliyekuwa waziri mkuu wa uingereza akipanda gari dogo aina ya saloon yeye pamoja na wasaidizi wake lakini bongo unakuta mkuu wa wilaya ametuna peke yake kwenye VIIEITE ambalo linakunywa mafuta kama maji. Bila serikali kubana matumizi mtaendelea kuhangaisha watu na mitozo yenu isiyoisha.
Ingetokea Nyerere akafufuka leo, basi angekufa tena ndani ya muda mfupi kwa mshtuko kwa namna hii nchi inavyoendeshwa..
 
BonT

JF-Expert Member
Oct 14, 2020
984
1,000
Juzi tu hapa tulikuwa tunaambiwa "Vituo vya afya vimejengwa nchi zima"!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom