Waziri Mwigulu Nchemba: Wapo wanaotamani tuvurugane kuharibu taswira ya nchi

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,506
H3H9417.jpg

Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba amesema kuwa Serikali inazuia kuwepo kwa maandamano ili kutoruhusu watu wachache wanaotamani Tanzania wavurugane kuharibu taswira ya nchi.

Akizungumza katika harambee iliyoandaliwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Usharika wa Masaka dayosisi ya Pare, wilayani Same, Mh. Nchemba amesema kuwa katika maandamano hayo wapo watu watakaofanya vitendo vya uhalifu ikiwemo wizi na hata kufyatua risasi ili ionekane kwamba nchi inaua watu.

"Wapo wanaotamani tuvurugane na tunapowaeleza wananchi wanaweza kujiuliza kwanini tunazuia maandamano wakati wapo watu wanaofanya mazoezi na ni kwa sababu hatutaki kuruhusu watu watuvuruge,’’ Dk Nchemba

Ameongeza kuwa wapo watu wenye mitazamo mibaya zaidi ambao wataiba na pia wataandaliwa watu watakaofyatua risasi ili ionekane watu wameuawa katika maandamano.

Amesisitiza kuwa lengo la kuzuia maandamano ni baada ya kuangalia kwa jicho la tatu maandamano hayo hivyo raia na vyama vya siasa wawaelewe kwani hawana nia ya kuminya uhuru wao ambao upo kwa mujibu wa katiba.

‘’Tunaangalia sura ambayo adui anaweza kupitia, wasione majira haya ni ya kawaida kuna mahali tumegusa hivyo hawafurahi na ndio sababu haya mambo yanatokea hivyo tunaomba msichukulie kuwa ni vitu vyepesi vyepesi bali mpanue mitazamo yenu mnapoona masuala haya yanapojitokeza,’’ ameongeza.

Chanzo: Muungwana
 
Kuna vitu vinatatiza sana. Hawa watu wana weledi wa kujua tupo kwenye kipindi cha hatari, wanaujuzi wa kujua matukuio yanayoweza kutokea lakini jambo dogo la kuwalinda wanaoandamana au washiriki wa kwenye mikutano hawawezi. Wanaamua kuzuia na kupiga marufuku.
 
View attachment 726037
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba amesema kuwa Serikali inazuia kuwepo kwa maandamano ili kutoruhusu watu wachache wanaotamani Tanzania wavurugane kuharibu taswira ya nchi.

Akizungumza katika harambee iliyoandaliwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Usharika wa Masaka dayosisi ya Pare, wilayani Same, Mh. Nchemba amesema kuwa katika maandamano hayo wapo watu watakaofanya vitendo vya uhalifu ikiwemo wizi na hata kufyatua risasi ili ionekane kwamba nchi inaua watu.

"Wapo wanaotamani tuvurugane na tunapowaeleza wananchi wanaweza kujiuliza kwanini tunazuia maandamano wakati wapo watu wanaofanya mazoezi na ni kwa sababu hatutaki kuruhusu watu watuvuruge,’’ Dk Nchemba

Ameongeza kuwa wapo watu wenye mitazamo mibaya zaidi ambao wataiba na pia wataandaliwa watu watakaofyatua risasi ili ionekane watu wameuawa katika maandamano.

Amesisitiza kuwa lengo la kuzuia maandamano ni baada ya kuangalia kwa jicho la tatu maandamano hayo hivyo raia na vyama vya siasa wawaelewe kwani hawana nia ya kuminya uhuru wao ambao upo kwa mujibu wa katiba.

‘’Tunaangalia sura ambayo adui anaweza kupitia, wasione majira haya ni ya kawaida kuna mahali tumegusa hivyo hawafurahi na ndio sababu haya mambo yanatokea hivyo tunaomba msichukulie kuwa ni vitu vyepesi vyepesi bali mpanue mitazamo yenu mnapoona masuala haya yanapojitokeza,’’ ameongeza.

Chanzo: Muungwana
nasikia huyu naye eti ana phd?
 
Kwa kuwa alishiriki kwenye ibada hiyo ya harambee, bila ya shaka alisikia ule waraka ukisomwa kwa waumini..
 
Angetoa basi na njia mbadala ya hayo maandamano, ki saikolojia binadamu ni kiumbe ambae hawezi kuridhika mpaka pale atakapohisi ana utulivu wa moyo, hata kama ukimpa mamilioni hawezi kutulia, na utulivu wa moyo huja baada ya binadamu kuhisi ameheshimiwa, amesikilizwa, amethaminiwa, na ametoa malalamiko na hasira zake moyoni....haya yote ni mambo madogo lakini usiyapuuze popote pale hata kama ni kwa house girl wako.
 
Mbona naongea kama layman sana huyu ni doctor(phd) kuna haja ya mjadala wa taifa kuhusu Elimu yetu duh......eti ni waziri ya wizara nyeti .....He lacks "intellectual arguments"
 
Yaani viongozi wa awamu hii wanajitekenya wanacheka wenyewe utasikia ooohh msichanye dini na siasa sasa huyu Mwigulu hapo anaongelea wapi...si kanisani kweli wamevurugwa.
Nadhani atakuwa ameondoka na kopi ya waraka wa askofu wake...
 
Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba amesema Serikali haizuii watu kuandamana ila maandamano yenye nia OVU ni lazima yadhibitiwe.

Dr. Mwigulu ameyasema hayo katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la KKKT wilayani Same.

Chanzo: Star Tv!
 
Teh kaniacha hoi tu hapo alipo ibukia kanisani kutoa michango .....

Kweli waraka umepenya penyewe
 
Nia ovu inaonekanaje? Nani wa kuiona? Udhibiti utafanyikaje? Itadhibitiwa nia au watadhibitiwa wenye nia?
Really?

Maandamano ya tarehe 26 April yalianza kuzungumzwa na Mange huko IG nadhani tokea mwaka huu uanze. Hapo mwanzoni haya yaliitwa MAPINDUZI. Lengo lao kuu la kwanza ni kutaka kubadilisha matokeo ya uchaguzi wa 2015. Yaani Magufuli na Shein wajiuzuru. Na bado haya yamebaki kama madhumuni ya haya maandamano.

Lakini isitoshe, mpaka leo hatumjui kiongozi au viongozi wa haya maandamano hapa nchini na hakuna alieomba ulinzi wa polisi.

Kuzipindua serikali za bara na visiwani sio NIA OVU?

Kuleta vurugu nchini kwa kufanya maandamano bila kuomba ulinzi sio NIA OVU?

Huu ni UHAINI na watakaohusika watafikishwa kwenye vyombo vya kisheria. This time adhabu sio miezi 5 jela kama aliyopata Sugu.
 
Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba amesema serikali haizuii watu kuandamana ila maandamano yenye nia OVU ni lazima yadhibitiwe. Mwigulu ameyasema hayo katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la KKKT wilayani same. Source Star Tv!
Kanisa likatae hela za Mwigulu haraka sana , ni hela zilizoloa damu ya Akwilina , arudishiwe mwenyewe .

Kanisa si kichaka cha wahalifu , huyu alitakiwa awe jela badala ya mtaani anakohangaika kuwatengenezea chadema kesi ya uhaini .
 
Back
Top Bottom