Elitwege
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 5,154
- 10,809
Mwanzoni wa mwaka 2019 bank ya dunia (world bank) iliitangazia dunia kuwa Tanzania imeingia uchumi wa kati mapema zaidi kwa miaka 5!
Kumbuka Tanzania ilitarajiwa kuingia uchumi wa kati mwaka 2025 lakini ikawahi miaka 5 kabla, bila shaka kuna wenye viwanda, wafanyabiashara na watanzania walijituma zaidi kwa kufanya kazi na kulipa kodi stahiki ndiyo maana tukafanikiwa mapema.
Lakini sasa baada ya kuingia awamu ya sita kabla hata ya kuwatambua na kuwapongeza walipa kodi walioifikisha nchi uchumi wa kati wamepuuzwa na kuanza kusikilizwa zaidi wafanyabiashara waliofungiwa biashara zao kwa kukwepa kodi.
Yani sasa hivi kila kiongozi anayesimama lazima asifie wakwepa kodi na kutaka biashara zao zifunguliwe.
Je ambao hawakuwahi kufungiwa viwanda na biashara zao kwa kuwa waaminifu wa kulipa kodi miaka yote mpaka tukaingia uchumi wa kati wanajisikiaje??
Anayelipa kodi na asiyelipa kodi wanaweza kushindana sokoni??
Namhurumia sana Mwigulu Nchemba amepewa target ya Trillion 2 kwa mwezi.
Lakini Sasa hivi kutoa receipt ya EFD machine imeanza kuonekana ni ulofa.
Kuna kundi la watu Iinajenga picha ya kwamba biashara zilizofungwa ni nyingi sana kuliko ambazo hazikufungwa.