Waziri Mwigulu Nchemba endelea kuchapa kazi, usirudi nyuma

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
327
414
Nakutia nguvu tena Mhe Mwigulu Lameck Nchemba "Madelu". Endelea kuchapa kazi usirudi nyuma. Wapo Watanzania wenzetu huko vijijini afya yao ni shida, barabara ni tabu n.k.

Ubunifu huu wa tozo unaenda kuokoa mamia kwa mamia ya watu wetu. Wapo watu nchi hii kazi yao ni kupinga tu sasa tukiwasikiliza hatutafika, hakuna jema kwao yani hata ufanyeje maisha yao ni kupinga kupinga.

Hivi vituo vya afya 220 na madarasa nchi nzima vikikamilika kwasababu ya ubunifu wako huu wa tozo aibu zitawajaa na utakuwa umeokoa wengi sana mamia kwa mamia.

We Kaka chapa kazi tukaokoe maisha ya wengine hasa kule vijijini. Usirudi nyuma, endelea kumsaidia Mhe Rais kwa nguvu zako zote. Sisi tuliozaliwa vijijini tunajua uchungu wa shida za afya, barabara, maji n.k

Usirudi nyuma, mjenga nchi ni mwenye nchi mwenyewe. Hakuna maendeleo yasiyo na maumivu. Mie sijawahi kuyaona. Tujenge nchi yetu.
 
Nakutia nguvu tena Mhe Mwigulu Lameck Nchemba "Madelu". Endelea kuchapa kazi usirudi nyuma. Wapo Watanzania wenzetu huko vijijini afya yao ni shida, barabara ni tabu n.k. Ubunifu huu wa tozo unaenda kuokoa mamia kwa mamia ya watu wetu. Wapo watu nchi hii kazi yao ni kupinga tu sasa tukiwasikiliza hatutafika, hakuna jema kwao yani hata ufanyeje maisha yao ni kupinga kupinga. Hivi vituo vya afya 220 na madarasa nchi nzima vikikamilika kwasababu ya ubunifu wako huu wa tozo aibu zitawajaa na utakuwa umeokoa wengi sana mamia kwa mamia. We Kaka chapa kazi tukaokoe maisha ya wengine hasa kule vijijini. Usirudi nyuma, endelea kumsaidia Mhe Rais kwa nguvu zako zote. Sisi tuliozaliwa vijijini tunajua uchungu wa shida za afya, barabara, maji n.k

Usirudi nyuma, mjenga nchi ni mwenye nchi mwenyewe. Hakuna maendeleo yasiyo na maumivu. Mie sijawahi kuyaona. Tujenge nchi yetu.
Wewe si mpiga Kiwi wa viatu vya DC Iramba? Nani asiyekujua unafki na kujipendekeza vimekujaa mpaka unaona aibu
 
Back
Top Bottom